Ushuhuda: Nilichokiona kwa mtoto wa kichaga, anza kufunza mwanao mapema

Ushuhuda: Nilichokiona kwa mtoto wa kichaga, anza kufunza mwanao mapema

Sokoro waito

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2014
Posts
2,201
Reaction score
2,599
Hamjambo wadau wapenda maendeleo,

katika pita pita zangu za kuongeza ujuzi wa maisha, niliwahi kusoma kitabu cha RICH DAD POOR DAD kilichoandikwa na ROBERT KIYOSAKI, jambo mojawapo nililojifunza ni jinsi RICH DAD alivyowafundisha kazi Kiyosaki na rafiki yake ilhali wakiwa watoto wa umri mdogo kabisa (walipokuwa wanafunzi wa darasa la 4). Mwanzoni walidhani alikuwa akiwanyanyasa kumbe alifanya vyema kuwafunza kazi na jinsi ya kutengeneza pesa, leo hii wako vizuri kiuchumi kwasababu walipewa msingi mzuri wa elimu ya pesa.

Turudi kwenye mada, jirani na ninapoishi kuna familia ya kichaga imejenga mji wa kuishi na fremu za maduka, juzi nikaenda kwa duka lao kununua mahitaji kadhaa ila nilipofika sikumkuta muuzaji mtu mzima kama nilivyozoea badala yake nikamkuta mtoto mdogo wa kike mwenye umri usiozidi miaka minane.


Akanikaribisha vizuri nami nikamsihi amfate mama yake kuja kunihudumia dukani lakini cha ajabu yule mtoto wa kike akaniuliza kwani wataka nini nikuuzie? Nikamjibu kwa swali, utajua kunirudishia chenji? Mtoto akakubali 'ndiyo nitaweza' .


Bhasi nikampatia elfu 2 nikamwambia anipe vocha ya elfu moja na soda moja ya chupa, yule mtoto akanihudumia kwa usahihi kabisa na chenji akanirudishia vyema.


Nikabaki kushangaa jinsi alivyofunzwa vyema yule mtoto mdogo, ila nikajifunza kuwa ukitaka mwanao apende biashara na kujishughulisha mfunze mapema kabisa, ukitaka mwanao awe na mafanikio ya kifedha baadae bhasi mfunze maana ya pesa na jinsi pesa inavyofanya kazi bado angali mdogo.


Funza mwanao aijue pesa angali mdogo.
 
Hilo kawaida uchagani ukiwa kijijini asubuhi unaamshwa ukakate majani ya mbuzi au ng’ombe
 
Wachaga ni wabantu wenzetu hivyo wanaweza kuwa mfano mzuri wa kuigwa katika eneo hilo. Ila kama kuna jamii ya watu mahihiri katika kuwafunza watoto wao biashara na mambo ya fedha ni WAHINDI! Labda tu kwa kuwa hawa-interact sana na wabantu ndio maana hatuoni hilo jambo linaoneka kwa matendo yao hasa sehemu zao za biashara!
 
Aaahh kuna
  • TRA je alikupa risiti ya mashine
  • kuna service levy je anaweza kujibu
  • kuna Bibi afya hizo soda alifuta na tissue au ulichukua takeaway na chenji ukarudishiwa
tuacheni Promo enzi hizi ni za Magu, biashara ina changamoto nyingi kwa sasa dukani hatumuweki mtu basi ni wa kuuza tu, kuna utapeli kwenye Vocha mpaka M Pesa na electronic money zote
 
Aaahh kuna
  • TRA je alikupa risiti ya mashine
  • kuna service levy je anaweza kujibu
  • kuna Bibi afya hizo soda alifuta na tissue au ulichukua takeaway na chenji ukarudishiwa
tuacheni Promo enzi hizi ni za Magu, biashara ina changamoto nyingi kwa sasa dukani hatumuweki mtu basi ni wa kuuza tu, kuna utapeli kwenye Vocha mpaka M Pesa na electronic money zote
Kazi yako naona kuvamia nyuzi za watu na kutoa upupu, jaribu kua na positive thought kidogo itakusaidia.
 
Mungu anisamehe.

Niliishi mtaa mmoja hivi kuna mzee ana duka wauzaji walikua ni watoto wawili wa kike na kiume kutoka kijijini.

Walikua hawajui kurudisha chenji.

Hivyo mimi na mshkaji wangu ukuwi ilikua tukifulia tunaenda na elfu mbili tunanunua mkate na vocha au soda.

Utashangaa chenji elfu sita mia nne.

Tukiwa mcharo tunaenda maduka mengine. Ukuwi tuombe Mungu tusamehewe.
 
Sawa Mkuu, hamna jamii ngumu kuishi kama hiyo unayoizumgzia ukikosa fedha,

Utadharauliwa na wazaz waliokuzaa, wakwe mashemeji. Ni hatari sana hyo jamii

Mtu anakuwa mtu kwa sababu ana kitu.
 
Hahahaaaa
Mtoto wako atafuata matendo yako na sio ushauri wako.

Watoto wa kihindi si kwamba hufuata ushauri wa wazazi wao bali matendo yao.

Sasa wewe asubuhi unaamka unaenda kumfanyia mwanaume mwingine kazi unategemea nini?Mtoto wako na yeye atakuwa ataenda kuwafanyia watu kazi zao na watakuwa wana mlipa.

Huwezi mfundisha mtoto wako biashara ilihali asubuhi ukiamka unaenda Ku implement dream za watu wengine. Never.

Anza wewe mtoto atakufuata tu. Hutahitaji kumfundisha biashara make atacopy kutoka kwako automatical
 
Maana yake
20180724_213139.jpg
 
Unashangaa mtu mwanae amesoma English medium akamaliza la saba badala ampeleke hata akajifunze kurengeneza keki, au maandazi anamkimbiza pre form 1

daaah
 
Mungu anisamehe.

Niliishi mtaa mmoja hivi kuna mzee ana duka wauzaji walikua ni watoto wawili wa kike na kiume kutoka kijijini.

Walikua hawajui kurudisha chenji.

Hivyo mimi na mshkaji wangu ukuwi ilikua tukifulia tunaenda na elfu mbili tunanunua mkate na vocha au soda.

Utashangaa chenji elfu sita mia nne.

Tukiwa mcharo tunaenda maduka mengine. Ukuwi tuombe Mungu tusamehewe.
Ungetia na address ya ilo duka ili nasisi tukiishiwa tuende tukaongezewe change hahahahaha (ila dhambi jamani)
 
hata sisi wakinga tunafundishwa pesa tukiwa wadogo kabisa.
 
Kazi yako naona kuvamia nyuzi za watu na kutoa upupu, jaribu kua na positive thought kidogo itakusaidia.
kafungue jukwaa lako nguruwe wewe
Maana ya Jukwaa huru ni nini sijakujibu wewe wala coment yako
rudi kwenye Mada
huwezi usichangie soma post sepa
hujawa moderator unikataze kutoa maoni yangu JF
NI MCHANGO GANI UMETUWEKEA HAOA TANGU UJIUNGE JUZI????
 
Back
Top Bottom