Ushuhuda: Siku mbili bila kulala, huu mtindo wa kulipana pesa bar naomba uundiwe vikao bungeni

Ushuhuda: Siku mbili bila kulala, huu mtindo wa kulipana pesa bar naomba uundiwe vikao bungeni

Midnight

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2021
Posts
229
Reaction score
681
Nisiwachoshe sana, Sasa ilivyokuwa baada ya wife kutangulia kuhesabiwa, mimi nilipaswa kufuatia nyuma yake kwa maagano ya kumalizia kazi za watu nilizozianza kisha mapema sana tarehe 25 niwe village hata kwa kutumia magari ya magazeti. Nazungumzia kuanzia juzi hiyo!! Sasa bwana huu mtindo wa kulipana pesa bar naomba uundiwe vikao bungeni, maana unarudisha nyuma uchumi wa nchi na maendeleo ya mtu mmoja mmoja.

Ilikuwa mapema tu saa mbili mzee mwenzako mwili wangu nikaupaki hapo maeneo ya Tabata kuna bar fulani hivi simpo simpo hivi lakini nyoko sana kukufilisi hiyo. Nazungumzia Mr Wine, ehh panaitwa Mr wine, baada ya mfukoni kuwa njema si ndio nikasema nijifariji kidogo na japo tu Serengeti lager tu.....ehhh mara vuup gari za wasiojulikana hizooo, plate namba hazieleweki, tinted hadi kwenye side mirros, na askari wa ulinzi ndani, hapo sasa ikawa gambe tu gambe kila mmoja anajiona TISS ni weka kitu, sambazia vitu raia, mi- bar maid chenchi hairudishi, kudai 1000 buku mbili za nini sasa, nijishushie heshima Mimi!!?

Kuja kushtuka saa kumi na moja hii, yule boss wangu alienilipia pesa bar Mungu amsamehe sana. Kupitia usafiri wake tukaona tuhame kiwanja Sasa, Ila kuna jamaa yake anakaa Bunju, ikabidi tumsogeze hadi simu 2000 pale. Kufika simu 2000 Sasa na mipombe si gari tukaiingiza kule zinapopaki daladala na ikiwa hapo ni makosa sana pale. Faster tu wazee hao na mtambo wao wa kudhibiti matairi, chap ikabidi tushuke tulichafue jiji kidogo maana si unajua nguvu ya pombe bwana, bahati yetu mbaya sana muda si muda tukadhibitiwa vilivyo, Ila mziki haukuwa mdogo aisee.

Wale jamaa wa simu 2000 nawachukia mimi nyie!! Yaani mnajifanya Kama matrafki? Na mnachukua rushwa kwa kila anaejichanganya maeneo yenu, siku yenu ipo.

Tukamwacha mshkaji hapo ahabili daladala za Bunju, nasi safari ikaanza upya, wakati huo watu wapo makanisani wanasali kumshukuru Mungu, sisi tunatafuta bar iliopo wazi tukaziabudu safari lager, Serengeti, Kvant na nyinginezo zozote zitakazo kaa mbele yetu, maana tumekuwa magari ya taka Sasa. Jamani habari ni ndefu sana Ila kwa kifupi wife katangaza tuachane kutokana na nilichokifanya, naombeni ushauri wenu wakuu na wanaotaka kuniona nipo Tabata hapa jina la bar kapuni kwa usalama wangu.
 
Wife ametangaza muachane kisa haujaenda safari au kisa umekunywa pombe? Pole mzee.
 
Wife ametangaza muachane kisa haujaenda safari au kisa umekunywa pombe? Pole mzee.
Kwanza sijaenda ukweni, imeonekana nimefanya dharau. Simu sipokei ikaonekana nachepuka.
 
Back
Top Bottom