Ushuhuda; Uuzaji wa bidhaa bila kuwa na pesa

Ushuhuda; Uuzaji wa bidhaa bila kuwa na pesa

Asante sana mkuu bado naendelea na faida inaingia vzr tu jana nimetoka kusafirisha mzigo wa zaidi ya laki nne mteja aliniomba nimfanyie shopping
Kuna runaotaka kujifunza Mkuu naomba tupe mbimu bas
Mimi sio mchoyo mkuu akihitaji kujua na kujifunza na yeye anakaribishwa sana. Nipo tayari kumpa ujuzi ila rule no.1 asiwe na tamaa hata kidogo
 
Habari zenu wakuu.

Leo nataka nilete ushuhuda kuna kitu nimekifanya na nashukuru kimenilipa tena kwa mara ya kwanza kabisa.

Leo nilienda kkoo kufanya research za biashara nikapiga picha baadhi ya vitu na kuvitupia mtandaoni. Wala sikua na hela ya kulipia.

Haikupita hata saa moja nikapokea simu watu wanahitaji. Wakanitumia hela pamoja na bidhaa wanayohitaji nami bila hiyana nikanunua kwa hela yao na kubaki na faida yangu nzuri tu.

Mzigo wao baadhi nishawatumia wengine nawatumia kesho. Na harakati zinaendelea pale pale. Kuna uzi hapa ulinifunua ndo chanzo cha mimi kuamua kujitupa huko.

Asante sana wakuu kwa uzi wenu
This eroventurhbe! 'dynamicsd4d,'dics tic "tuu t
 
Back
Top Bottom