Ushuhuda: Vitu vidogo vinaweza maanisha mambo makubwa kwa wengine

WENYELE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,433
Reaction score
1,442
Katika hii dunia tunayoishi, unaweza ukamfanyia mtu kitu kidogo tu lakini ukabaki ndani ya historia ya maisha yake.

Jioni hii nikiwa nimejipumzisha na familia yangu ikawa imeingia sms kutoka kwa kijana aliyemaliza mtihani wake wa chuo wa mwisho akinishukuru.

Mnaweza mkakosoa shida zake za r/l hii ni kutokana na athari ya lugha yake mama lakini mimi kuiona nimefarijika kujua kuwa msaada niliyompatia ulikua na thamani (Nimemsaidia kutola Form I hadi kamaliza chuo).

Kushukru ni jambo la heri

Screenshot_20220719-223552_Messages.png
 
Kuna kijana hajabahatika kumuona mama yake kwa miaka 11, nikaingiwa na imani nikasema ngoja nimpe laki na nusu aweze kwenda kijijini kwao kwao. Huyu kijana sina undugu nae hata kidogo ila nimemfahamu tu mtaani. Picha linaanza kakaa week moja anataka kurudi Dar, nikamweleza hela ngumu mie nimejinyima ili wewe uweze kwenda kumsalimia mama yako. .

Niliwaza sana inakuaje akifariki au inakuwaje mama yake akifariki this will be so painful. Kila anachovaa nimemnunulia mimi kwa hela yangu kwani alikuwa na kazi akafilisika mapema. Leo karudi Dar kaja kunisalimia usiku huu lakini cha ajabu mbali na kuwa hata zawadi alizopeleka nyumbani nimemnunulia mimi hakuja hata na chungwa au embe la zawadi kutoka kwao. Ila sio kwamba nilimsaidia ili aniletee zawadi hapana sikutegemea kitu nachotaka kusema unafurahi kuona mtu anajua mchango wako kwakwe. Hii inakupa moyo wa kuendelea kumchangia wengine wapo kukunyonya kama kupe. .

Hayo tu.
 
Usihukumu chukulia poa, huwezi kujua kakutana na yapi na Hawezi kukuambia... All in all saidia pale ambapo unaweza
 
Siwezi kumuhukumu nazungumza kitu ambacho nakijua. Neno Asante linaweza kuwa na maana kubwa kuelewa mtu anajua mchango wake kwako. Sifanyi kumhukumu wala kutaka shukani nilichosema ni kuwa yeye ni aina ya watu ambao hawawezi tambua unaweka nini ndani yake. Sijaona ubaya wa nilichoandika. .
 
Mafanikio ya mtu yapo kwa mtu.
Hakuna kitu utafanya kwa moyo radhi na Mungu asibariki.
Kuna binti wa kazi,aliilea familia moja kwa zaidi ya miaka 10. Ile familia ilimpa offer ya kwenda kuongeza elimu kwa level yoyote atakayopenda.
Alianzia ni QT,akafika mpaka chuo.
Leo tunapoongea,ni mke wa mtu mzito sana hapa nchini.
Ile familia inaneemeka kupitia mgongo wa binti,leo kuna mtoto yupo nje kimasomo kwa ufadhili wa mume wa mdada.

Wapendwa wema auozi,tuwatendee wengine wema,tutalipwa muda tusio taraji.
 
Katika hii dunia tunayoishi, unaweza ukamfanyia mtu kitu kidogo tu lakini ukabaki ndani ya historia ya maisha yake.

Jioni hii nikiwa nimejipumzisha na familia yangu ikawa imeingia sms kutoka kwa kijana aliyemaliza mtihani wake wa chuo wa mwisho akinishukuru.

Mnaweza mkakosoa shida zake za r/l hii ni kutokana na athari ya lugha yake mama lakini mimi kuiona nimefarijika kujua kuwa msaada niliyompatia ulikua na thamani (Nimemsaidia kutola Form I hadi kamaliza chuo).

Kushukru ni jambo la heri

View attachment 2297121
Uliyofanya ni ibada kubwa sana. Vitabu vyote vya dini vinahimiza kusaidia wenye uhitaji. Mkuu, Mungu akuzidishie mafanikio na kukuongezea mara dugu ya uliyotoa. Amen.
 
Siwezi kumuhukumu nazungumza kitu ambacho nakijua. Neno Asante linaweza kuwa na maana kubwa kuelewa mtu anajua mchango wake kwako. Sifanyi kumhukumu wala kutaka shukani nilichosema ni kuwa yeye ni aina ya watu ambao hawawezi tambua unaweka nini ndani yake. Sijaona ubaya wa nilichoandika. .
Wewe huweziona ubaya, lakini ukizama kwa ndani baadhi ya sentensi ni kama malalamiko fulani hivi indirectly.
 
Unaweka maneno mdomoni mwangu. .

Huyu kijana alikuwa analewa mpaka anazimia for three hours, nimemsimamia aache pombe sijui kama anakunywa au la. Nimemlisha almost everyday nampa hela ya kula na hana kazi kwangu. Ameanza kwenda kanisani hilo nimefurahi. Sasa mie nikimzungumzia ni kwa sababu namjua. Hebu nieleze ni wapi nimelalamika?

Mimi nimefundishwa na baba na mama yangu hata ukipewa hela unasema asante. Sikusemakuwa nahitaji asante iola kiheshima ni lazima mtu ujifunze kushukuru. Rudi soma nilichoandika. Mbona hakusema asante vitu vingi na nimemwezesha, nachomanisha lazima ujue mtu anatambua mchango wako maishani mwake inakupa moyo wa kuona anaelekea unapotaka kumwongoza. Kama hujaelewa tena nachoandika basi potezea. .
 
Yote kwa yote tusaidie pale tunapoweza, nakumbuka kipindi flani napiga mishe ila kuna jamaa alitoka kilwa huko akaja mjini kusaka life ila mungu hakumbariki alikuja ofisini kuniomba kazi ili nimpe hadi nauli yake ya kilwa itakapotimia arudi kwako, huyu jamaa alinivutia sana na nilimpitia siku ile japo kuna washikaji nai walichangia ila ile shukrani aliyoitoa ilitoka kwenye kilindi cha a moyo wake sina kumbukumbu kama niliwai kupata shukrani kiasi kile hadi leo picha ya yule mshkaji ipo kwenye mboni zangu
 
Back
Top Bottom