Ushuhuda wa breakthrough!

Wewe mchungaji wa kilokole humpati mtu
wala hulazimishwi. sijawahi kuwa mchungaji, na sitegemei kuwa mchungaji, ila nilichoandika ni cha kweli, God is my witness. na sikulazimishi kuamini au hata kukiamini chenyewe. kitu pekee nimefanya ni kutapika kilichoko moyoni mwangu ili watu wajue ukuu wa Mungu. ndio maana sijaelekeza mtu aende kwenye kanisa lolote hata lile ninalosali ili pengine ufikiri mimi ni mchungaji nadanganya ili kupata waumini, Nooo, nimeandika kitu kilichoko moyoni mwangu, na siku nilipoandika tu nina amani sana kwasababu hata haikuwa lazima kwangu watu wote wasome au waamini hii kitu, hata mtu mmoja tu angesoma na kuamini anatosha. cha kushukuru Mungu watu wengi sana wameona na kusoma hivyo nimenawa mikono, damu yao haidaiwi mikononi mwangu. Jina la Bwana libarikiwe. kwa taarifa yako mimi ni mwanasheria, wala si mchungaji.
 
Mungu mkubwa,pia anatendea watu wake mambo makuu,sio pesa tu,baraka za Mungu wote zinatujaalia,angalia Mimi hajanipa Pesa kama hizo nimepata ya kula tu,ila unajua kikubwa alichonipa??Uhai na afya Njema...and hayo mawili we take them for granted,huwezi kusikia mtu ana Bragg kua bukheriii...Mungu wangu mkubwa Sana, Asante kwa afya tele.
 
Nakubaliana nawe kuwa unapotoa zaka unabarikiwa katika kazi na mapato usipotoa kipato kinayeyuka tu bila kujua kimeenda wapi na mambo ya kiuchumi yanakwama tu bila hata sababu za kueleweka Mungu si mwanadamu hata aseme uongo alisema leteni zaka kamili ghalani na huwa habadiliki hivyo zaka ni muhimu Jana, leo na hata milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…