#COVID19 Ushuhuda wa Mchungaji Godwin Chilewa kuhusu COVID-19: Je, tunamficha nani, kwanini na kwa Faida gani?

Huyu jamaa ni mzushi kwa kuzingatia nukuu ya maneno yake mwenyewe kisa anaishi Marekani

Nukuu "...ukizingatia kuwa nilianza kuumwa nikiwa kwenye ndege........"

Mpaka hapo tuhuma anazozitoa kuhusu Tanzania ni chuki binafsi maana virusi vinaweza kufanyakazi kati ya siku moja na siku kumi na nne hivyo kuugua kwake akiwa tayari yuko ndani ya ndege na kwamba amekiri wakati akiwa bado akivinjari kwenye mitaa ya nchi ya Tanzania alikuwa ni mzima basi ugonjwa aliupata ndani ya ndege.
Wacha kelele, kwanza hiyo maabara ya kupima wagonjwa wa Covid mnayo?

Nimemuelewa vizuri sana analosema majibu ya Corona mnayotoa ni ya uongo, yes ni uongo, kwasababu mlishasema kwenu hakuna Covid sasa iweje mtu aliekuja akiwa mzima aondoke na ugonjwa?

Mnapiga pesa za watu dola 100 kuwadanganya mnawapima kumbe mnawaibia tu pesa zao mpeleke kwenye miradi yenu isiyoeleweka.
 
Binafsi nlipoanza kupata such symptoms nilikimbilia kutumia tuba asilia pamoja na hizo za kufukiza nyungu. Lkn hazijasaidia na zilinipelekea shida ya upumuaji kwa vile wadudu waliendelea kushambulia kifua na mapafu.

Niliporudi kwa doctor aliniambia niache kujifukiza mara moja ni hatari kwa pumzi.
Rafiki kujifukizia ni mbinu ya viongozi wetu ya kuua watu ndiyo maana wao wakiugua hawajifukizii bali wanakimbilia matibabu ya kisasa huko Nairobi na India.
 
Nimesoma hadi machozi yamenitoka.... Mungu wa mbinguni atupiganie . Corona ni mbaya sio ya kufanyia mzaha
Imagine Corona inasababisha kisukari,presha na damu kuganda.Sasa assume kuwa Corona imekupiga halafu umepatwa na hizo presha,kisukari na damu kuganda halafu unakomaa na kupiga nyungu!!!😭😭😭
 
Rafiki kujifukizia ni mbinu ya viongozi wetu ya kuua watu ndiyo maana wao wakiugua hawajifukizii bali wanakimbilia matibabu ya kisasa huko Nairobi na India.
Kuna yule aliyejifukizia hotelini akaenda kudondokea mjengoni.
Hahahahahahahahahahaha...........
 
Mkuu umetoa ushauri mzuri ila naomba na Sisi tukushauri
Mkuu Corona imekusumbua sababu hufanyi mazoezi. Anza kufanya mazoezi.
Huu ugonjwa haumuathiri mtu anayefanya kazi za kushughulisha mwili, mfano wakulima,wabeba mikokoteni, wanamichezo, waendesha bodaboda,machinga etc
Ukisikia mtu anashambuliwa na Corona, ujue huyo mtu ni wale watu wa kuchukuliana na gari mpaka ofisini, akifika anakaa kwenye kiti mpaka anatoka, then anarudi nyumbani na kukaa kuangalia TV.kama unaishi aina ya hayo maisha, ukipata Corona inakumaliza.
Ila wazungu baada ya kugundua kwamba wanamichezo hawaathiriki na Corona ndio maana michezo inaendelea kama kawaida duniani kote. Wachezaji wa mipira siku hizi hata wakifunga magoli wanakumbatiana na majasho yao kama kawaida sababu wameshajua Corona haina impact kwao
NOTE:
Tangu Corona ianze 2019, hakuna mwanamichezo aliyefariki dunia, na hakuna mwanamichezo aliyewahi kuzidiwa na Corona na kupelekwa hospitalini.
Wanamichezo wanaiona Corona kama mafua tu, wakipata Corona wanajitenga ili wasiambukize wenzao ila huwezi kusikia wanaenda hospitalini kuwekewa oksijen
Tusitumie kigezo hicho kuacha kudhibiti maambukizi ya corona kwakuwaambia watu wafanye mazoezi ili corona isiwadhuru sana

Sio kila mtu ana uwezo wa kufanya mazoezi kuna watu wengine miili yao hairuhusu kufanya zoezi
 
Wallah hii ni vita ya kiuchumi...... ni vita kabisa inaonekana hata kwa macho... tunaona kabisa ni vita tu ya kiuchumi wala si jambo jingine lolote. hii corona ni tu mafua tu wala siyo issue kuuuuubwa kihivyo.
 
[QUOTE="Mlatinoh king, post: 38084082, member: 3313Ila mi kwangu tatizo Ni jinsi Serikali inavokataa haya maswala ya sayansi kwa kiburi Tena hadharani.....!!!!
Na Sasa WHO ime exclude Tanzania na Burundi kwnye mpango huo was chanjo ya Covid....!!!

That may not be problem..
Lakini hili swala linanipeleka mbali kuwaza hivi hiki kiburi tulichokionesha mpaka mataifa pamoja na WHO kutuacha tujiendeshe tunavoona Sanaa, je siku ikija kutokea serious disease ingine kabisa tofauti na hii hapa Bongo tutawaomba WHO kutupa msaada tukiwa na sura za aina ipi......!!!!

Kuna njia nyingi za kukataa matibabu na sio kosa kisheria lakini sisi tumeyakataa matibabu kwa kiburi na kejeli nyingi Sana.

Let's see
[/QUOTE]
Nakubaliana na yote hayo, WHO sio nchi, ni taasisi ya mataifa yote duniana, so haifanyi hisani bali ni wajibu wake.
 
Nilijua utakuja na pumba za aina hii! You are not educated at all. There is a slim difference between you and the learned nots because you know to write!
Ahsante sana mkuu huyu jamaa ni takataka huwa anapenda kuandika ujinga mpaka kwenye serious issues
 
Tusitumie kigezo hicho kuacha kudhibiti maambukizi ya corona kwakuwaambia watu wafanye mazoezi ili corona isiwadhuru sana

Sio kila mtu ana uwezo wa kufanya mazoezi kuna watu wengine miili yao hairuhusu kufanya zoezi
Sio wote, lakini wengi wanaoamini hawawezi kufanya mazoezi ndio hasa wanaotakiwa kufanya mazoezi maana mazoezi yako ya aina nyingi.
 
[QUOTE="Mlatinoh king, post: 38084082, member: 3313Ila mi kwangu tatizo Ni jinsi Serikali inavokataa haya maswala ya sayansi kwa kiburi Tena hadharani.....!!!!
Na Sasa WHO ime exclude Tanzania na Burundi kwnye mpango huo was chanjo ya Covid....!!!

That may not be problem..
Lakini hili swala linanipeleka mbali kuwaza hivi hiki kiburi tulichokionesha mpaka mataifa pamoja na WHO kutuacha tujiendeshe tunavoona Sanaa, je siku ikija kutokea serious disease ingine kabisa tofauti na hii hapa Bongo tutawaomba WHO kutupa msaada tukiwa na sura za aina ipi......!!!!

Kuna njia nyingi za kukataa matibabu na sio kosa kisheria lakini sisi tumeyakataa matibabu kwa kiburi na kejeli nyingi Sana.

Let's see

Kiburi cha kukataa ushauri wa WHO na sayansi kimemrudia Jiwe mwenyewe, saa hizi sijui yuko kwenye lile container la Muhimbili anajifukiza?
 
Nimeugua Covid 19, nikatibiwa na kupona (Jina la Bwana lihimidiwe). Kuugua kwangu kumenisaidia kujifunza mengi, na kubaini uongo mwingi wanaoambiwa watu wetu ili kuwapooza, badala ya kufanya jitihada ya dhati ya kuwalinda, na kuwaokoa na janga la COVID 19. Ni kwa sababu hii nimeona vema kuandika machache kuhusu ugonjwa huu.

Nianze kwa kuweka bayana kuwa naishi nchini Marekani, lakini niliambukizwa Covid-19 nchini Tanzania nilikokuwa nimeipeleka familia yangu kusherehekea siku kuu ya Christmas na mwaka mpya.

Tuliwasili Tanzania tarehe 6 Desemba 2020 tukitokea Houston. Siku mbili kabla ya kuondoka Marekani, mimi na familia yangu tulipimwa na kuthibitishwa hatukuwa na virusi vya Covid-19 kigezo muhimu cha kuturuhusu kutoka nje ya nchi. Baada ya kuwasili Tanzania tulikaa Dar es Salaam, tukazungukia vivutio vya utalii vya Serengeti na kumalizia likizo yetu Zanzibar.

Siku mbili kabla ya kuondoka Tanzania tulikwenda hospitali ya Muhimbili kupima covid-19 ili tuweze kupata cheti cha kuturuhusu kutoka nchini kwa mujibu wa taratibu na maagizo ya wizara ya afya. Mimi na familia yangu (mke na watoto watatu) tulilipa dola mia tano ($500) gharama za vipimo hivyo. Tarehe 14 January tulipokea majibu na vyeti kuwa sote tulikuwa ‘Negative’ na kesho yake tarehe 15 January 2021 tuliondoka kwa ndege kurudi Marekani. Cha ajabu ni kuwa nilianza kuumwa nikiwa kwenye ndege.

HALI YA TANZANIA
Ukiwasikiliza viongozi wetu wanapozungumzia ugonjwa wa covid-19 utasikia wakisisitiza suala moja tu “Piga nyungu” na tumia kinywaji cha tangawizi, limao na vitunguu swaumu kuongeza kinga ya mwili wako. Maneno haya yaliyoanzia kwa wanasiasa, na kubebwa na wataalam wa afya yamesambaa kama moto katika nyasi kavu na kisha kuzama katika mioyo ya watu wengi wenye imani na viongozi wao.

Ukitafakari kwa kina utagundua kuwa kampeni hii ya kuvutia imewafanya watanzania kuitua mzigo serikali kwa kuamini wanaweza kujitibu wenyewe, hawapaswi kuisumbua wala kuihoji serikali kuhusu HATUA za dhati inazochukua katika kupambana na maambukizi mapya, kufungua vituo vipya vya tiba ya COVID-19, Kuboresha matibabu ya COVID 19, na au kushughulikia suala la chanjo

Swali la kujiuliza ni je! Nyungu inatibu? Na je! ni kweli kuwa kinywaji cha tangawizi, limao na vitunguu swaumu vinaweza kukuponya endapo utapata maambukizi makali ya COVID 19 ?

UGONJWA COVID-19.
Siku mbili baada ya kuwasili Marekani, hali yangu ilikuwa mbaya sana; mwili na mifupa yote ilikuwa ikiniuma vibaya sana, kichwa kilikuwa kikigonga kana kwamba kinataka kupasuka, na joto la mwili wangu lilikuwa juu mno kiasi cha nyuzi joto 103 F na lilikuwa haliteremki. Nilipelekwa katika kituo cha kupimia virusi hivyo na kubainika kuwa ni POSITIVE. Mara moja familia yangu, jamaa na marafiki toka Tanzania wakanishauri kupiga nyungu na kutumia tangawizi, vitunguu swaumu na vidonge vya vitamin lukuki vinavyopatikana hapa. Nilifanya hivyo kwa siku mbili mfululizo, huku nikiendelea kutumia vidonge vya kushusha homa bila mafanikio.

Siku ya tatu hali ilikuwa mbaya sana. Licha ya homa kutoteremka kabisa, nilianza kushindwa kupumua, na blood pressure yangu ilikuwa imepanda kuliko kawaida. Mke wangu akanikimbiza Methodist Hospital, mojawapo ya hospitali kubwa zinazoheshimika nchini Marekani. Nikapokelewa na kulazwa, nikawekewa Oxygen na kupewa dawa za kushusha homa, kisha kazi ya uchunguzi wa kitabibu ikaanza.

Kwanza manesi walichukua sampuli zaidi ya kumi za damu na kuzipeleka maabara. Muda mfupi baadae nilifanyiwa X-ray ya mapafu, na baadae nikafanyiwa CT scan ya mapafu kuangalia undani wa maambukizi. Vipimo vyote vilikuwa tayari baada ya saa moja hivi, na daktari akaja kunipa maelezo ya hali yangu:

JINSI COVID-19 INAVYOUA
Labda nisisitize hapa kuwa virusi vya Corona humshambulia kila mtu kwa namna tofauti. Mashambulizi hayo huweza kuwa mabaya sana (severe) au madogo tu (mild) kutegemea hali ya ki afya ya mtu mwenyewe, uwezo wa mwili wake katika kupambana na maradhi, na aina ya vijidudu vilivyomshambulia. Hata hivyo kutokana na hali halisi ya watanzania, wengi wanaweza kuangukia katika kundi hatarishi.

Baada ya kupokea matokeo ya vipimo vyangu Daktari alianza kwa kunipooza kuwa “You’re in good hands, so don’t worry, you will be fine“ kisha akaendelea kunieleza ukweli mchungu ambao natamani kila mtu aufahamu na kuzingatia.

Alinieleza kuwa virusi vya covid-19 vilikuwa vimepenya katika mapafu na kunisababishia pneumonia. Hali hii ilikuwa inaendelea kuwa mbaya kwa kadri muda ulivyokuwa ukienda na ndiyo iliyokuwa ikinifanya nishindwe kupumua.

Virusi vya corona vinasababisha damu kuganda hivyo aliniambia upo uwezekano nikapata blood clots ndogondogo (miner) au mbaya (severe) kwenye ubongo, moyo au mapafu. Akafafanua kuwa endapo damu itaganda kwenye ubongo hawatakuwa na uwezo wa kufanya lolote “ there is nothing we can do” isipokuwa kama ni kwenye mapafu au moyo wanaweza kuishughulikia (We can do something).

Mapigo ya moyo wangu (BP) yalikuwa juu mno hali iliyoleta wasiwasi kuwa naweza kupata kiharusi. Mapigo hayo yalipandishwa mno na maumivu ya mwili, pamoja na homa kali iliyokuwa haiteremki. Ilibidi niwekwe kwenye uangalizi maalum.

Jambo lingine ni kuwa virusi vya corona huweza kukuletea KISUKARI cha muda. Hii ina maana hata kama wewe huumwi, wala hujawahi kuwa na historia ya ugonjwa wa kisukari, Covid-19 inaweza kupandisha sukari ya mwili wako kwa kiwango cha kukuua. Hali hiyo huongezeka zaidi endapo utapewa madawa aina ya steroids kukusaidia kupunguza athari ya covid (inflammation) katika mapafu.

Mapafu na mwili mzima kujaa maji ni tatizo lingine kubwa linaloweza kukuondoa duniani haraka. Virusi vya corona husababisha viungo vya mwili (body organs) kuhifadhi maji ya ziada. Kwa sababu zile siku mbili za mwanzo nilikunywa maji mengi ya tangawizi na limao, mwili wangu ulikuwa tayari umehifadhi maji mengi kuliko inavyotakiwa hali iliyoyapa mapafu ugumu wa kufanya kazi yake.

Daktari pia alinishangaa na kunionya vikali kuhusu suala la kupiga nyungu (kujifukiza) baada ya mimi kumuuliza kama hiyo ilikuwa “first aid sahihi” Aliniambia kuwa kitu nilichofanya kilikuwa kutaka kujiua mwenyewe (sucide) na alishangaa nimewezaje kunusurika. Alifafanua kuwa covid-19 hudhofisha mapafu, na kupunguza kiwango cha hewa ya Oxygen inayoingia katika mzunguko wa damu na kwenda kwenye ubongo. Zile dakika tatu au tano unazojifunika na kujifukiza mvuke hupunguza zaidi kiwango cha hewa safi inayoenda katika ubongo wako hali inayoweza kusababisha kuanguka ghafla na kufa. Alisisitiza mgonjwa wa Covid-19 anahitaji oxygen sio mvuke.

MATIBABU
Ili kukabiliana na hali niliyokuwanayo Daktari alinifanyia mpango wa matibabu ufuatao:

Aliagiza nipewe madawa ya kupambana na bakteria kwa ajili ya kuua wadudu walioingia kushambulia mapafu na kunipa pneumonia. Dawa hizi nilipewa kwa kuchomwa kwenye mishipa (drip).

Aliagiza nipewe plasma (damu ya mtu mwingine) aliyeugua ugonjwa wa corona na kupona. Plasma ya mtu hiyo kwa vile tayari ina antibodies zilizoweza kupambana na virusi vya corona na kuvishinda ilionekana itaweza kuusaidia mwili wangu kuimarisha mapambano na vijidudu hivyo.

Aliagiza nipewe dawa mpya ya kupambana na virusi vya corona iitwayo Remdesivir iliyoonesha ufanisi katika kupambana na ugonjwa huo. Mgonjwa hupewa dawa hii kupitia mishipa ya damu (drip).

Kushusha mapigo ya moyo na kuendelea kudhibiti hali hiyo nilipatiwa dawa za aina mbili tofauti (moja asubuhi na nyingine jioni) huku wauguzi wakifuatilia kwa karibu hali inavyoendelea.

Aliagiza nipewe dose ya steroids mara mbili kwa siku ili kusaidia kupunguza inflammations katika mapafu. Hili lilienda sambamba na madawa ya kushusha homa niliyopewa kila baada ya masaa manne.

Aliagiza nichomwe sindano za insuline ili kudhibiti sukari iliyokuwa ikipanda hovyo. Ingawa mimi sina historia ya kisukari, wala ukoo wetu hatuna historia ya kisukari, covid-19 ilinipa kisukari cha muda, na kama nisingeenda hospitali kutibiwa nisingejua kabisa. Nilichomwa sindano hizo kila siku kwa muda wa siku sita niliokuwa nimelazwa hospitali.

Aliagiza nichomwe dawa ya kuyeyusha damu (blood thinners) ili kuzuia uwezekano wa damu kuganda (blood clots) katika ubongo, moyo na mapafu. Sindano hizi nilichomwa tumboni, mara mbili kwa siku, kwa muda wa siku sita.

Kwa vile viungo vya mwili (body organs) zilikuwa zimejaa maji ya ziada, aliagiza nichomwe diuretic ili zinisukume kwenda haja ndogo mara nyingi kupunguza maji mwilini. Sindano hizi nilichomwa mara mbili kwa siku kwa siku sita.

Kutokana na wingi wa madawa niliyokuwa nikitumia daktari pia aliagiza nipewe vidonge maalum vya kuzuia tumbo lisiathirike na kutengeneza vidonda vya tumbo.

Pengine utajiuliza kwa nini nimechukua muda kuelezea mlolongo wa matibabu nilioupata katika nchi ya dunia ya kwanza, huku nikijua kuwa si rahisi kwa mtanzania wa kawaida kuyapata? Naomba nieleweke hapa kuwa lengo langu ni kuwafumbua macho walio wengi kuwa ugonjwa wa covid-19 si wa mzaha, madhara yake ni makubwa, na hautibiki ki rahisi kama viongozi wetu na wataalam wa afya wanavyodai, na kusisitiza kuwa kupiga nyungu, na kikombe cha tangawizi au chupa chache za dawa za asili zinaweza kumponya mgonjwa wa covid-19. Huu ni uongo mbaya unaoshambulia maeneo tofauti ya mwili, na kuweza kukupa magonjwa mengine ambayo hujawahi kuugua. Hebu fikiria madhara anayoweza kupata mtu kwa kunywa kikombe cha tangawizi yenye sukari pasipo kujua kuwa covid-19 imeshampa kisukari!

HADAA KWA WAGENI
Jambo lingine linalonikera ni hadaa ya kijinga inayofanywa kwa wageni na wasafiri. Mwanzoni mwa mwezi Januari 2021 serikali kupitia waziri wake wa fedha iliyoa agizo la kutaka watu wote (Pamoja na watalii) wanaotaka kutoka nchini kupimwa covid-19 (Kwa gharama ya USD 100) na kupewa cheti cha kuthibitisha usalama wao. Agizo hilo lililoonekana kama lenye umuhimu na lengo la kuzuia kusambaa kwa maambukizi mapya limeishia kuwa kitega uchumi ka Taifa. Wengi wa wageni wanaopimwa kama ilivyoelekezwa hawapewi majibu sahihi, na kwa wakati kama inavyotakiwa. Hii ni kwa sababu wapimaji wamepewa maelekezo kutoweka bayana kwamba Tanzania kuna Covid-19 na hivyo kulazimika kutoa majibu ya uongo.

Ukweli huu unaweza kuthibitishwa kwa kufuatilia idadi ya wasafiri toka Tanzania wanaougua covid-19 mara tu baada ya kuwasili katika nchi wanazokwenda (Final destinations). Nikiwa hospitali ya Muhimbili nilikutana na wageni kadhaa waliokuwa wakilalamikia kupigwa danadana kwa majibu yao. Pamoja na hilo mimi mwenyewe pia nilipimwa na kupewa majibu ya uongo kuwa ni sina vijidudu vya corona (Negative) wakati kumbe nilikuwa na virusi hivyo. Namshukuru Mungu kuwa uongo wao uliniwezesha kurudi Marekani, na kupata tiba stahiki. Hata hivyo nasikitika kwani sijui uongo huo ulisababisha kuwaambukiza watu wangapi ukizingatia kuwa nilianza kuumwa nikiwa kwenye ndege.

HADAA YA TIBA ASILIA
Kama nilivyoeleza hapo juu, hivi sasa viongozi na wataalam wetu wa afya wamejikita katika kuhimiza upigaji nyungu, na matumizi ya dawa asilia. Lakini je! hizi dawa zinatibu kweli au ni placebo tu? Bila shaka mtu yeyote mwenye akili timamu atatambua kuwa kinachoendelea ni utaratibu wa kuwatoa hofu watanzania, kwa placebo na maneno ya faraja. Lakini je, nchi inafanya nini kumuokoa mtanzania?

Hebu tikiulize, kwanini serikali haiweki bayana mipango yake ya muda mrefu na muda mfupi katika kupambana na ugonjwa huu? Kwa nini waziri wa afya asisimame kuwaambia watanzania kuwa imefunguliwa center kubwa ya kuhudumia wagonjwa wa corona, na wote wanaougua ugonjwa huo watapelekwa huko kupatiwa matibabu stahiki? Kwa nini serikali haisemi tangu ugonjwa huu ulipoanza imeingiza nchini mashine ngapi za kuwasaidia wagonjwa mahututi kupumua? Kwanini haisemi imetumia kiasi gani kuagiza madawa ya kisasa kama Remdesivir na mengineyo? Kwa nini hata haizungumzii au ku promote matumizi rahisi ya plasma katika kutibu ugonjwa huo? Kulikoni?

HITIMISHO
Ni dhahiri kuwa kuna tatizo kubwa katika kushughulikia ugonjwa huu kuliko wengi tunavyojua. Ni vema watanzania wote tukatafakari upya na kuwahoji viongozi wetu ili walieleze taifa ukweli. Waseme ni kitu gani kinachowazuia kwenda sambamba na jumuia ya kimataifa, pamoja na mashirika kama WHO katika kupambana na ugonjwa huu. Ni hatua gani wanachukua katika kuboresha matibabu ya covid 19 katika hospitali zetu, na kwa kutumia taaluma ya kisasa badala ya mitishamba.

Mimi binafsi ningependa kujua kama serikali kupitia wizara ya afya imewahi kuagiza na kusimamia matumizi ya plasma na dawa aina ya Remdesivir kwa wagonjwa wa corona nchini. Mpaka sasa muungano huo umeonesha uwezo wa kuwasaidia wagonjwa wa covid-19 ikiwa pamoja na mimi mwenyewe..

Hili ni jukumu letu sote.
Uwe na amani

Kwa nini unasema Corona uliipatia Tanzania? Si ulipimwa Muhimbili uka onekana negative? Mbona familia yako wote hawakupata?
"You are in good hands, so don't worry" uliyoambiwa na daktari wako ukamuamini (yaani kukutoa woga kwanza), waTanzania wote (taifa lote) liliambiwa hivyo na raisi wetu - ameendelea kututoa woga.
Hivi ulisha ugua malaria na ukaenda hospital huko marekani? Mbona watakuchukulia kama mtu wa kufa hapo hapo! Hivyo Nakushauri - unavyo onekana kwenye picha, immune yako ni ndogo sana, kwanza kwa sababu ya uzee, vyakula unavyo kula, maisha yako ya mswahili kukaa kwa wazungu na WOGA! hivyo ulikuwa hustahili kusafiri wakati wa gonjwa hili. Utakuwa (wewe) umelieneza Tanzania.
 
Una uhakika zimefanyiwa tafiti? If yes, weka publication result hapa za research hiyo.
Maisha ya mwafrika, dawa, mavazi, vyakula, malazi (aina ya ujenzi wa nyumba), kulima na kupanda (na misimu) - vyote hivyo vimefanyiwa utafiti siku nyingi na waafrika wenyewe. Nikupe mifano michache - wagogo nyumba zao ni flat, wahaya nyumba zimechongoka paa. Na mengine mengi, hivyo usidharau kwamba hakuna utafiti uliofanyika - katika ujenzi sehemu yenye ukame na yenye mvua nyingi unajulikana paa litakuwaje.
Na yote hayo hayana any publication in the building & settlement journal.
Utabiri wa hali ya hewa pia - unajulikana kienyeji.
 
Kubwa jinga wewe!
 
tuko kwenye modern days. unlike huko nyuma wasomi hawakuwa wengi, si wote hawakujali publications.
in modern world ya sasa,ukisema umegundua kitu fulani, lazima uonyeshe proof kua its true.

zama zimebadilika.
however sipingi vumbuzi za kiafrika.
 
huyo atakuwa jinamizi, sisi hatuna corona wasijaze ujinga wao kwetu..mbona hata timu zetu zinakuja huko kucheza mipira...na wengi wakipimwa huonekana hawana hivyo virus..pia na hata wakigundulika kuwa navyo fasta huwa wanapona.
 
Back
Top Bottom