#COVID19 Ushuhuda wangu kuhusu janga la COVID-19

#COVID19 Ushuhuda wangu kuhusu janga la COVID-19

Mimi wimbi la tatu lilinipa kash kash niliporejea kutoka kanda ya ziwa nikajisikia viungo kama vimelegea, nikakosa appetitle na uwezo wa kuhisi harufu na baadaye nikawa nakohoa na kutoa makohozi (productive cough), matibabu niliyotumia ni nyungu na sometimes dawa za paracetamol....sasa huwa najiuliza, inakuwaje nichanje wakati nimeshapata natural infection? Jambo ambalo nataka nielimishe watu ni kuwa asilimia kubwa sana ya watanzania hadi sasa wameshakuwa exposed kwa virusi vya korona, hivyo kuchanja ni useless, labda kama mabeberu watwambie hiyo chanjo ina kitu gani cha ziada hadi ichanjwe kwa watu ambao walishapata uambukizi?
Tuchukue tahadhari muhimu mkuu, ishu ya chanjo ibaki uuamuzi binafsi, Lakini watu wanapoteza maisha
 
Wewe jamaa unatumia kichwa kufuga nywele tu ,,Ni ukoo mmoja na yule Elitwege Ni hasara kwa Taifa watu Kama nyinyi.
Bora umemwambia Ukweli kabisa, aendelee kufanya kejeli Ila mwisho wake huwa mbaya Sana
 
Ilikua mwaka Jana kwenye wimbi la pili. Nilianza kujisikia homa yenye ganzi baada ya kutoka kwenye sherehe ya send off. Baadaye nikajisikia pua zimeziba mfano wa mafua makali.

Nikaenda pharmacy nikanunua termisatan nikijua ni malaria. Huku nikila malimau , tangawizi .

Strange enough hali ikazidi kua mbaya. Nikaanza kuishiwa nguvu. Wanao nizunguka wakanitengeneza mchanganyiko wa mjani nijifukize. Tatizo nilikua mbishi kwenda hospital.

Baaya ya kupiga nyungu nikaanza kukohoa damu. Nikawaomba jamaa zangu wanikimbize hospital.

Hospital oxygen saturation ikasoma 47% . nikaogopa sana. Nikawekwa kwenye oxygen for two weeks.

Covid ni hatari. Hata baada ya kutoka hospital. It took me a moth to Regain my strength. Namshukuru Mungu nilipona.
Complications nilizo experience.
1 . conjunctivitis
2.hemorrhoids
3. Vidonda kooni
4. Skin rashes
5. Complete loss of smell and taste
Namshukuru Mungu nilipona

Dah polee sana mkuu.
 
Wewe jamaa unatumia kichwa kufuga nywele tu ,,Ni ukoo mmoja na yule Elitwege Ni hasara kwa Taifa watu Kama nyinyi.
Nyinyi madalali wa chanjo lazima twende sambamba.

Taifa la watu wajinga wajinga wanaojali pesa za wazungu kuliko uhai wa mtu ni taifa la wendawazimu.

Mimi ninashughulika na wendawazimu wa mitandaoni kama wewe ambao mnalazimisha kujaza watu HOFU na VITISHO vya KIFO.

Hafi mtu hapa, na wala HAKUNA CORONA.

Hizi ni hadithi za propaganda tuu!! Hakuna lolote.
 
Habari ndugu zangu wana Tanganyika na Zanzibar!

Poleni kwa magumu tunayopitia, pia hongereni kwa zawadi ya uhai!

Najua humu JF familia kubwa tunaweza shirikishana Mambo mengi, leo naomba tushirikishane kuhusu Corona.

Wapo waliougua na kufariki( R.I.P), wapo waliougua na kupona, wapo waliouguza ndugu, jamaa, rafiki wakafariki Lakini wapo waliouguza na mgonjwa akapona,

Kwa phase zote 3, wimbi la 1, 2 Hadi hili la 3.

Naomba tujaribu kushirikishana uhalisia, ushuhuda wa corona ktk muktadha niliojaribu kuelezea hapo juu.

Kwangu Mimi ninao ushuhuda 2.

MOSI! Katika wimbi la kwanza tulimpoteza jirani yetu, yule Mzee ni mstaafu wa Serikali, alikuwa anaafya njema tu, alikuwa anapenda kujumuika jioni kwenye Bar fulani kupata kinywaji na kucheza Draft, corona ilivyoanza mzee akasitisha kuhudhulia Bar

Lakini baada ya muda km siku 3 akaanza kuhisi kuumwa, ikaamua aondoke kwenda Dom, kufika huko Hali ikawa mbaya zaidi, kalazwa na kupewa mtungi wa gesi.

Kabla ya kifo siku moja alikuwa vizuri kidogo na aliweza kuongea na simu, Lakini Hali ikabadilika ghafla na kupelekea kifo,
Ilikuwa majonzi Sana.

PILI!! Hii Ni wimbi hili la tatu, wiki hii ktk kundi letu la WhatsApp kuna memba moja akatuambia tumuombee maana changamoto ya upumuaji imemkabili.

Tukachukulia kawaida, jana imetoka taarifa yule memba umauti umemkuta,

Hakika Ni huzuni Sana, kifo kipo lakini kifo chakuona unakielekea kinauma zaidi.

Naomba tushirikishane/ ku-share matukio au ushuhuda kuhusu corona Kama umeugua au umeuguza vipi Hali ilikuaje?

  • Ulianza/ alianza kujisiakiaje Hadi kujua Ni corona?
  • Changamoto zipi ulipitia Hadi kuanza kupata nafuu?
  • Je, ulipata matibabu gani?
  • Kama ulikuwa hospital vipi Hali kwa Wagonjwa wenzio?
  • Je, ilikuchukua muda gani kupona na kurudi ktk Hali ya kawaida?

Kupitia ushuhuda wako tunaweza saidia wengine pia, corona IPO ndugu zangu, na watu wanakufa!

Karibuni sana wakuu!
Kwani Magu anasemaje huko motoni.
 
Unaenda nao sambamba humu wakati chanjo zimeshafika kwenye vituo 500+, Unaakili kweli Wewe? Kazuie vituoni huko ukanyooshwe!
 
Back
Top Bottom