Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

First, let me declare kwamba mimi ni member wa muda mrefu humu JamiiForums na nimependa kuja nah hii ID mpya ili kuweza kuficha utambulisho wangu wa hapo mwanzo, ili kuepeuka mambo kadhaa kutoka kwa member ambao nimebahatika kuonana/kukutana nao.

Naitwa Priscallia (si jina langu halisi) na umri wa miaka 29 na ni mtumishi wa serikali katika mamlaka fulani hapo nyumbani Tanzania kwa sasa nipo nchi X nikisomea shahada ya juu ya mambo fulani fualni pia ni muathirika wa virusi vya UKIMWI.

Anyway, kwa ufupi ilikuwa ni mwezi wa 6 mwaka 2014 kipindi nipo chuo mwaka wa mwisho ambapo nilianza kuhisi homa na mafua makali kwa muda wa wiki moja baadae nilienda hospitalini kufanya vipimo na baada ya vipimo ikagundulika niko na typhoid ambapo nilipewa dawa nikaanza dose na baada ya kumaliza zile dalili zote zilipotea.

Ila baada ya kumaliza UE mwezi mmoja baadae nilipokuwa field ile hali ya mafua na homa zikanirudia na safari hii kilichonishtua ni kuongezeka kwa baadhi ya dalili kama vile kupoteza hamu ya kula, kutapika na baadhi ya rashes katika baadhi ya sehemu ya mwili wangu, niliamua kutumia baadhi ya dawa na tubes kwa muda wa wiki kadhaa lakni sikuona mabadiliko yoyote nikaamua kwenda hospitali ili kuchukua vipimo upya, nakumbuka ilikuwa ni mwezi wa saba (7) mwishoni kuelekea wa nane (8) baada ya kuonana na daktari na kumueleza nilivyokuwa najisikia (consultation) daktari akaniandikia baadhi ya vipimo kama vile choo, mkojo na damu baada ya muda fulani majibu yalipotoka yote yalisoma negative.

Baada ya majibu hayo, dokta akataka kunichukua vipimo vya HIV na akaniuliza kwa upole “Kama nilishawahi kuchukua vipimo vya ukimwi hapo kabla?” nikamjibu kwa kujiamni kuwa nilipima mwaka mmoja nyuma baada ya kuachana na aliekuwa mpenzi wangu na majibu yalikuwa Negative.

Akaniuliza tena kwa sasa upo katika mahusiano nikamjibu kwa ufasaha kuwa "NDIO" nikaenda mbali zaidi nikamwambia mahusiano haya yana miezi mitano (5) sasa na mwanzo tulipoingia katika mahusiano tulikuwa tunatumia kinga ila tulipozoeana na baada ya mwenzangu kunihakikishia kuwa yuko sawa (HIV negative) tukajikuta tukishiriki tendo bila kutumia kinga kama ilivyokuwa hapo mwanzo.

Baada ya mazungumzo hayo na daktari nikakubali kuchukuliwa damu kwa mara nyingine ili kuweza kujua status yangu ya HIV, baada ya muda majibu yalirudi nikaitwa kwenda kuonana na daktari nilipokuwa naingia daktari alikuwa akinitazama kwa huruma na hakuonesha ule uchangamfu wa mwanzo nilipoingia ofisini kwake. Katika mazungumzo akaniambia kwa upole kuwa anashindwa afikishe vipi majibu yaliyoko mezani kwake kwangu hapo mapigo ya moyo yalibadilika na hofu ilianza kuingia ndani yangu, ndipo hapo akaniambia ya kwamba majibu yamerudi na kwa masikitiko makumbwa vipimo vinaonesha mimi ni muathirika wa virusi vya ukimwi.

Hakika ile siku ilikuwa mbaya sana katika maisha yangu, I go into shock. I did'nt think of anything rather than I’m going to die nililia sana siku ile, dokta alinimbeleleza sana siku ile akaniambia nisihohofu/nisijali kila kitu kitakuwa sawa na kwamba huo sio mwiosho wa maisha yangu. Siku ile nilijiuliza maswali mengi kichwani mwangu kwanini mimi? Kwanini imetokea kwangu? Tena kwa wakati huu ambapo nilikuwa ndio nimemaliza masomo yangu ya shahada nilijisika vibaya mno.

Baada ya hapo nilimpigia simu yule mwanaume ambaye pia alikuwa ni mwalimu wangu huku nikilia nikamwambia kila kitu, alionekana kusikitika/kushangaa na muda mwingi alikuwa akijichanganya sana katika mazungumzo na muda mwingine alikuwa hana cha kunijibu na kubaki kimya.

Nilimblock kwa muda wa miezi kadhaa hapo sasa nikawa nawaza nitawaambia nini wazazi wangu nikawa sina jinsi maana wao ndio familia yangu, baada ya siku 5 niliwambia kuwa kuna jambo nataka niwaeleze hivyo wakawa nashauku ya kujua baada ya chakula cha usiku nilivunja ukimya nikawaambia sikuwa na jinsi ya kuficha tena kuhusu hali yangu. Nakumbuka mama yangu na mdogo wangu wa kike walilia sana ila nashukuru hapo baadae waliamua kukubaliana na hali halisi ingawa Baba na kaka yangu walisikitika sana ila mwisho wa siku walinisamehe pia.

Ilinichukua muda sana kukubaliana na hali ile but mwisho wa siku ilibidi iwe hivyo. Because I knew now I am not going to die, in fact in pretty good health, more stronger, confidence and having a good life. Kufupisha story ni kwamba baadae, tuliwasiliana na huyo mwalimu wangu alikiri kuwa yeye ndio aliniambukiza nilimsamehe na nilikuja kugundua kuwa hata mke wake alimpteza kwa ugonjwa huo baada ya kuugua kwa muda mrefu pia na nikiri wazi alikuwa ana upendo wa dhati kwangu maana baada ya kuhitimu masomo yangu alinitafutia kazi katika mamlaka fulani ambapo nipo nafanya kazi hadi leo hii.

Mwisho, ningependa kuwaasa wadogo zangu waliopo vyuoni hasa hawa waliopo mwaka wa kwanza wasiwe wepesi kurubuniwa maana hawa ndio wahanga wakubwa maana mara nyingi ugeni wa chuo na exposure zinawachanganya sana hawa wadogo zangu na mwisho wa siku huishia kufanya mapenzi bila kutumia mipira na hivyo hujikuta wakiharibu afya zao.

Pia na kwa wale dada zao waliopo mwaka wa pili na kuendelea pia muwe makini sana, najua wengi wenu huwa mnaishia kuingia katika mitego ya mahusiano na walimu wenu wa chuo,mkumbuke hawa ndio waathirika wakubwa hivyo mjitahidi sana kabla ya kukutana kimwili mhakikishe mnapima kwanza afya zenu na ikiwezekana mtumie mipira maana huwezi kumjua muathirika kwa kumuangalia kwa macho.

Lastly, kuna vijana baadhi nilikutana nao humu ndani they were good guys lakni niligundua wengi wao hawajali afya zao na wanaongozwa sana na sexual desire, maana unakuta mwanaume mko nae faragha baada ya mzunguko wa kwanza from nowhere anataka muende peku au katikati ya tendo anavua mpira kwa makusudi, wanajijua watakuwa mashahidi nilikuwa nawakatilia katukatu maana nilikuwa nawajali sana.

All in all ukimwi upo, mjitahidi mlinde afya zenu maana Afya ni mtaji. Ahsanteni niwatakie mchana mwema.

Priscallia.
Oooh its courage enough to expose u'r status and this might be merit in one way or another, km hutojali njoo PM kuna habari njema ningependa tushee, thank you !!
 
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]Weee umenijuliaa wapi mimi???? Sijawahii gonga demu wa jf hata kimasiharaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Umeamua kuruka viunzi hapa,[emoji3] [emoji3] ,na ulivyo na masikhara ya kula matunda huenda ushakula tayari,usikanee[emoji3] [emoji3]
 
Kabla huu uzi haujafutwa au kufungwa, nachelea kusema "una roho mbaya kuwaambukiza binadamu wenzio" maksudi. Mungu akusamehe
 
Priscallia,
Ila ungekuwa umeguswa ungeleta kwa ID yako wanayoijua uliotembea nao humu JF. Ili wajue mstakabali wa afya zao.Incase walikupiga peku peku. Walinde wenzako.
Asante kwa kukazia mkuu, hata nilimwambia huko juu kuwa lait kama angekuwa shujaa na mpenda afya za watu wengine angekuja na ID yake ili tumjue.

Watu wanamwita shujaa sasa ushujaa wake uko wapi kama anakuja na id mpya,

Mimi simuiti shujaa.
 
Pole sana na jitahidi kufwata maelezo ya wataalamu wa afya.
Lakini kuna sehemu moja umenishangaza uliposema ulijua una maambukizi na bado ukaendelea tembea na watu wa JF na bado una mahusiano na Prof. ulikua na nia gani hasa?

Kingine nimepitia comment zako za huko nyuma kuna sehemu ulidai ukiwa chuo ulidate na majamaa wawili kwa mpigo inasikitisha.

Mi nakuomba utulie kwa sasa maana si tayari ushajijua uko katika hali hiyo kama vipi tulia tu na Prof. hawa vijana wengine utawaangamiza kwa makusudi na itakua ni dhambi.
 
Pole sana kwa matatizo, mtu Ana Ukimwi anakula pekupeku kwa mdada wa umri mdogo.

Wadada wa chuo wanapenda kupata A, B+ Hapa ndipo wanapoingia kwenye matatizo ya kuliwa.
 
We Dada isije ikawa ni harakati za kupunguza watu kuja pm[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].... Maana naelewa psychology kidogo wewe kama kweli umelala na wanaume humu Jf there was no way upate courage ya kuja kuandika uzi kama huu... Lakini all in all umetupa somo now days Ukimwi hauongelewi kama zamani.. Alafu wakumbushe na Mdudu Mwingine yule anaitwa Hepatitis B.. Huyu sahivi anasambaa kwa kasi sana hapa nchini na kuyu anahatari sana maana nae ni kirusi...[emoji855][emoji855][emoji855]

First, let me declare kwamba mimi ni member wa muda mrefu humu JamiiForums na nimependa kuja nah hii ID mpya ili kuweza kuficha utambulisho wangu wa hapo mwanzo, ili kuepeuka mambo kadhaa kutoka kwa member ambao nimebahatika kuonana/kukutana nao.

Naitwa Priscallia (si jina langu halisi) na umri wa miaka 29 na ni mtumishi wa serikali katika mamlaka fulani hapo nyumbani Tanzania kwa sasa nipo nchi X nikisomea shahada ya juu ya mambo fulani fualni pia ni muathirika wa virusi vya UKIMWI.

Anyway, kwa ufupi ilikuwa ni mwezi wa 6 mwaka 2014 kipindi nipo chuo mwaka wa mwisho ambapo nilianza kuhisi homa na mafua makali kwa muda wa wiki moja baadae nilienda hospitalini kufanya vipimo na baada ya vipimo ikagundulika niko na typhoid ambapo nilipewa dawa nikaanza dose na baada ya kumaliza zile dalili zote zilipotea.

Ila baada ya kumaliza UE mwezi mmoja baadae nilipokuwa field ile hali ya mafua na homa zikanirudia na safari hii kilichonishtua ni kuongezeka kwa baadhi ya dalili kama vile kupoteza hamu ya kula, kutapika na baadhi ya rashes katika baadhi ya sehemu ya mwili wangu, niliamua kutumia baadhi ya dawa na tubes kwa muda wa wiki kadhaa lakni sikuona mabadiliko yoyote nikaamua kwenda hospitali ili kuchukua vipimo upya, nakumbuka ilikuwa ni mwezi wa saba (7) mwishoni kuelekea wa nane (8) baada ya kuonana na daktari na kumueleza nilivyokuwa najisikia (consultation) daktari akaniandikia baadhi ya vipimo kama vile choo, mkojo na damu baada ya muda fulani majibu yalipotoka yote yalisoma negative.

Baada ya majibu hayo, dokta akataka kunichukua vipimo vya HIV na akaniuliza kwa upole “Kama nilishawahi kuchukua vipimo vya ukimwi hapo kabla?” nikamjibu kwa kujiamni kuwa nilipima mwaka mmoja nyuma baada ya kuachana na aliekuwa mpenzi wangu na majibu yalikuwa Negative.

Akaniuliza tena kwa sasa upo katika mahusiano nikamjibu kwa ufasaha kuwa "NDIO" nikaenda mbali zaidi nikamwambia mahusiano haya yana miezi mitano (5) sasa na mwanzo tulipoingia katika mahusiano tulikuwa tunatumia kinga ila tulipozoeana na baada ya mwenzangu kunihakikishia kuwa yuko sawa (HIV negative) tukajikuta tukishiriki tendo bila kutumia kinga kama ilivyokuwa hapo mwanzo.

Baada ya mazungumzo hayo na daktari nikakubali kuchukuliwa damu kwa mara nyingine ili kuweza kujua status yangu ya HIV, baada ya muda majibu yalirudi nikaitwa kwenda kuonana na daktari nilipokuwa naingia daktari alikuwa akinitazama kwa huruma na hakuonesha ule uchangamfu wa mwanzo nilipoingia ofisini kwake. Katika mazungumzo akaniambia kwa upole kuwa anashindwa afikishe vipi majibu yaliyoko mezani kwake kwangu hapo mapigo ya moyo yalibadilika na hofu ilianza kuingia ndani yangu, ndipo hapo akaniambia ya kwamba majibu yamerudi na kwa masikitiko makumbwa vipimo vinaonesha mimi ni muathirika wa virusi vya ukimwi.

Hakika ile siku ilikuwa mbaya sana katika maisha yangu, I go into shock. I did'nt think of anything rather than I’m going to die nililia sana siku ile, dokta alinimbeleleza sana siku ile akaniambia nisihohofu/nisijali kila kitu kitakuwa sawa na kwamba huo sio mwiosho wa maisha yangu. Siku ile nilijiuliza maswali mengi kichwani mwangu kwanini mimi? Kwanini imetokea kwangu? Tena kwa wakati huu ambapo nilikuwa ndio nimemaliza masomo yangu ya shahada nilijisika vibaya mno.

Baada ya hapo nilimpigia simu yule mwanaume ambaye pia alikuwa ni mwalimu wangu huku nikilia nikamwambia kila kitu, alionekana kusikitika/kushangaa na muda mwingi alikuwa akijichanganya sana katika mazungumzo na muda mwingine alikuwa hana cha kunijibu na kubaki kimya.

Nilimblock kwa muda wa miezi kadhaa hapo sasa nikawa nawaza nitawaambia nini wazazi wangu nikawa sina jinsi maana wao ndio familia yangu, baada ya siku 5 niliwambia kuwa kuna jambo nataka niwaeleze hivyo wakawa nashauku ya kujua baada ya chakula cha usiku nilivunja ukimya nikawaambia sikuwa na jinsi ya kuficha tena kuhusu hali yangu. Nakumbuka mama yangu na mdogo wangu wa kike walilia sana ila nashukuru hapo baadae waliamua kukubaliana na hali halisi ingawa Baba na kaka yangu walisikitika sana ila mwisho wa siku walinisamehe pia.

Ilinichukua muda sana kukubaliana na hali ile but mwisho wa siku ilibidi iwe hivyo. Because I knew now I am not going to die, in fact in pretty good health, more stronger, confidence and having a good life. Kufupisha story ni kwamba baadae, tuliwasiliana na huyo mwalimu wangu alikiri kuwa yeye ndio aliniambukiza nilimsamehe na nilikuja kugundua kuwa hata mke wake alimpteza kwa ugonjwa huo baada ya kuugua kwa muda mrefu pia na nikiri wazi alikuwa ana upendo wa dhati kwangu maana baada ya kuhitimu masomo yangu alinitafutia kazi katika mamlaka fulani ambapo nipo nafanya kazi hadi leo hii.

Mwisho, ningependa kuwaasa wadogo zangu waliopo vyuoni hasa hawa waliopo mwaka wa kwanza wasiwe wepesi kurubuniwa maana hawa ndio wahanga wakubwa maana mara nyingi ugeni wa chuo na exposure zinawachanganya sana hawa wadogo zangu na mwisho wa siku huishia kufanya mapenzi bila kutumia mipira na hivyo hujikuta wakiharibu afya zao.

Pia na kwa wale dada zao waliopo mwaka wa pili na kuendelea pia muwe makini sana, najua wengi wenu huwa mnaishia kuingia katika mitego ya mahusiano na walimu wenu wa chuo,mkumbuke hawa ndio waathirika wakubwa hivyo mjitahidi sana kabla ya kukutana kimwili mhakikishe mnapima kwanza afya zenu na ikiwezekana mtumie mipira maana huwezi kumjua muathirika kwa kumuangalia kwa macho.

Lastly, kuna vijana baadhi nilikutana nao humu ndani they were good guys lakni niligundua wengi wao hawajali afya zao na wanaongozwa sana na sexual desire, maana unakuta mwanaume mko nae faragha baada ya mzunguko wa kwanza from nowhere anataka muende peku au katikati ya tendo anavua mpira kwa makusudi, wanajijua watakuwa mashahidi nilikuwa nawakatilia katukatu maana nilikuwa nawajali sana.

All in all ukimwi upo, mjitahidi mlinde afya zenu maana Afya ni mtaji. Ahsanteni niwatakie mchana mwema.

Priscallia.
 
Pole sana,

Ila huyo jamaa sidhani kama alikupenda, kama alikupenda asingekugusa hata, means alikua anasambaza,
Ila hao vijana unaosema, kama kweli ulikua unawajali sana kwanini uwakubali au kutoa tahadhari kabla,kama unaogopa kujulikana basi ungewakataa kabisa, sababu ukiwakubali utaumiza mamia,

Ila kama kweli unawajali unge,watahadharisha mapema au kuwakataa,
kwanini hukuwatahadharisha au kuwakataa, means nawewe unasambaza(simaniishi vibaya) ndio maana umewakubali bila ya kuwapa tahadhari, bora utulie labda yupo atakayekupenda kweli,

kuliko kuwakubali Hao wanaojiita mabaharia, kwanini nimesema mabaharia sababu mtu anayejitambua hawezi kutongoza AVATAR au kitu ambacho hukijui historia yake hata kukiona basi, Na haya ndio malipo ya mtu asiyejitambua, Na inavyoonyesha hawa mabaharia hawatulii Na boti moja kila itakayopita wamo, Na hizo boti nazo akiingia Baharia mwingine naye yumo vilevile, huyo Baharia alietoka boti hii Anaenda boti nyingine Na hiyo boti nayo IMO,

kumbuka Yule Baharia wa kwanza kabisa alietoka boti mbovu naye kashapita boti kama nne hizo boti nne nazo zinaendelea kusambaza ni mzunguko usiyokwisha, chanzo ni boti moja tu. MTAANI NA HUMU ndio bahari ya Hindi, Mwisho MMU inageuka mHmIuV,kama ni kweli, nisamehe kama nimekuudhi, Ila sio kwa nia mbaya,

Japo hii kama chai,
Natamani kila mtu Angekua anajitambua. Sababu haya ndio yanaendelea bila sisi kujua na yanaendelea kutokea HUMU na MTAANI pia,

Ushauri
Kaka,dada Usijipe moyo Kacheck afya yako kwanza, Kama hujui afya yako, nakuambia ukweli hao mabaharia na hizo boti wote hazijui Nini kinaendelea kisa wanaogopa kupima, unajua kwanini wanaogopa, jibu unalo, usiingie kichwa kichwa hizo za kuvaliwa hazizuii 100% jiamini peke yako (kuwa makini na afya yako afya ndio Kila kitu duniani ukiipoteza kurudi ni sawasawa ufanye maswali 50 ya math/hesabu , umalize ndani ya dk5)baada ya kupima tafadhari kama tayari usiongeze mwingine, labda mtu anayejua Hali yako na anayekupenda kwa dhati na anayejitambua ambaye sexy ni kitu Cha mwisho kwenye mapenzi, ila ukiongeza baharia au boti moja tu

(kumbuka sifa za mabaharia na boti)utaumiza makumi, mamia, na maelfu,
Kama bado tafuta mke ingiza ndani, kama umri hauruhusu huyo girlfriend wako hakikisha unapima kwanza kisha mnagandana mpaka ndoa, OA kisha baki njia kuu, muwe mnapima Mara kwa mara, piga kazi watoto wasome vizuri.
Mimi Sio mfia dini, ni ubongo wako unaoshindwa kuuongoza.

Amka Anza kujitambua. Ujinga wako Ni fursa kwa wengine wao wanatajirika, wewe huku unakufa maskini kwa kununua vidonge maisha yako yote, na lazima utanunua si unataka kuishi, sawa sawa na kulipia uhai wako mwenyewe, tabu yote ya nini kwanini usitulie, ule maisha yako kwa furaha kamili, kuliko kulipia maisha yako, huku ukiwa na kisasi na Kila mtu.

Amka Tujitambue mara 3000.
Tony Stark.
 
Uzuri wa HIV huwa haiambukizi waliokwisha ambukizwa. Inaambukiza wapya kila siku.

Lakini huku niliko HIV ikifika naamini UPEPO WA KISULISULI sio mchezo.
 
Msiogope jamani ngoma haiui kabisaa! Kinachoua ni magonjwa nyemelezi na njaa. Yaani kutokuwa na uhakika wa matibabu na kula. Ukishakuwa na uwezo wa kutibu magonjwa madogo madogo na kujiepusha na magonjwa makubwa makubwa unaweza jikuta unapinda mgongo na kuchafuka kichwa kama Lowassa. Ila chunga sana ukiwa na ngoma omba usipatwe na kisukari. Onyo: usifanye ngono zembe ipo siku dawa za a.r.v zitaadimika kwa sababu yoyote ile kama vikwazo vya kiuchumi, vita nk..... Alisikika kijana mmoja toka pande za Makete wanakoishi watu wasioiogopa ngoma kabisaa!
 
asante kwa kutoa angalizo, sijajua jamii ya kike humu ndani inanichukuliaje. Mimi nimeguswa kwa namna moja ndio maana nimeamua kwa dhati kuleta uzi huu ili kuwafumbua macho baadhi ya members both ME na KE ila nimeishia kusemwa sana.

Naongea kweli kutoka moyoni, muwe makini sana na baadhi ya Wanawake/wanaume humu ndani mostly wale maarafu wanaona kama nawaharibia mambo yao lakni hapana, Mungu akijaalia nitakuja na uzi mwingine kuwafungua macho zaidi. Na wengi siku za hivi wamebadili ID zao wamekuja na ID mpya ukiwa makini ni rahisi kugundua wanajua walichowafanyia baadhi ya member humu ndani. Inaumiza
Dada ushanitisha mi Kuna member namizimia humu sana aisee .

Halafu maarufu ila sikubali lazima nimpate aniambukize tu kwakweli [emoji28]
 
Back
Top Bottom