USHUHUDA: Watanzania tuwe wakweli juu ya ufugaji wa kuku

Kak
Tena usipojipanga kwenye chakula utasema umelogw maana kuku wanakula hatari kama viwavi unaeza nunua gunia la pumba ukatengeneza chakula manina hat mwezi gunia halitoboi daah,hakuna jambo rahisi chini ya jua
Mkuu lkn walikupa faida?!!
 
Tatizo sio la watanzania tatizo ni la kwako, umeshindwa kung'amua huo ufugaj wako kwa hizo gharama utaufanyia wapi na unaanza na Kuku wangapi? Kwa huo mtaji unaouzungumzia maana yake unataka kuanzia na mradi Mkubwa kidogo lakin mtu anayetaka kuanza angalau na Kuku 10 au 20 hawezi kutumia mtaji huo au hata Kuku 50 mtaji huo ni mkubwa, Mimi nilitengeneza banda la fut 5 kwa 6 likawa na floor mbili kwa sh. 250000/=, nilinunua kuku 12 wa miez mitano walianza kutaga kwa sh. 12,000/=@ walitaga mayai nikakusanya trei moja ndani ya siku 4 nikaenda kutotolesha nikapata vifaranga 26 ambavyo nilivilelea mpaka vikakua, kwa mtindo huo huo nilifikisha Kuku 60 walipokuwa nikawauza wote, kuna changamoto ilinikabili, chakula wanakula ndio lakin kama unawafungia bila kuwaruhusu hapo watakukost, kwahiyo ni vile unachukulia,mambo ndo yanavyokuwa
 
Tatizo letu tunataa faida ya fasta fasta ndo shida yaani unataka ufuge ndani mwezi uanze kula faida hicho kitu hamna utaishia kusema waongo, cha kuelewa ni hiki kila mradi una changamoto zake ila ukiamua ni kupambana nazo
 

Mkuu naomba Msahada tutani EM.1 ndo nini?
 

Mkuu unafugia maeneo gani nikutembelee, mimi nipo Dsm
 

Ahsante sana mkuu
 
Mkuu naomba unijuze hiyo EM. 1 ni nini hata kama ni pm
Napenda sana kufuga kuku na ninao kama 50 hv we nimekuelewa sana ila mleta mada kwa kweli hapend watu wafuge me nmetengeneza banda na kununua kuku wale wenye mwezi mpaka miezi 2 hata laki sidhani kama ilifika mpaka ss kuku wanajitegemea chakula wenyewe mana nauza mayai nawachukulia vyakula
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ufugaji wa kuku ni uwekezaji kama ulivyo uwekezaji mwingine. Hivyo lazima ujipange kimtaji na uwe tayari kukabiliana na hasara yoyote itakayojitokeza.
sio kukabiliana na changamoto, ufugaji kuku wa jienyeji ni biashara unaanza na hasara mkononi. Kifupi hakuna kuku wa kienyeji mjini, wapo vijijini. Mazingira ya mjini hayatoshelezi kuwapa nafasi ya uasilia. Matokeo wanafugwa kama wa kisasa na ubora wa nyama na mayai kuwa duni.
 
Wafugaji wa ndege ( hasa Kuku) serious naona hawajachangia kabisa kwenye huu uzi.
Kiufupi niwashauri wanaotaka kufuga kiuhalisia na wakaona faida ya ufugaji wa ndege hasa Kuku wa Kienyeji, Mayai pure( layers) au chotara, angalau Uwe na Kuku wengi waliofikisha umri wa kutaga ndipo utaona faida ya ufugaji huu tofauti na hapo inakuwa unaishi na ndege....nazungumzia economies of scale....
Ufugaji wa kuku ni uwekezaji, ni biashara yenye tija ikiwa utaiona hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…