The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Serikali kupitia Hotuba ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2026/2027 inapendekeza kupunguza ushuru wa forodha kwa magari yanayotumia nishati ya umeme nchini. Ushuru huo unashushwa kutoka asilimia 25 ya sasa hadi asilimia 10 kwa magari yote yanayoingizwa nchini yaliyo chini ya makundi ya HS Codes 8702.40.19, 8702.40.22, 8702.40.29, 8702.40.99, 8703.80.90, na 8704.60.90.
Lengo kuu la maboresho haya ya kikodi ni kuhamasisha uwekezaji na matumizi ya teknolojia ya nishati ya umeme katika sekta ya usafirishaji nchini.
Hatua hii inatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa mafuta ya petroli na dizeli, hatua ambayo si tu kwamba itasaidia kulinda mazingira dhidi ya uchafuzi wa hewa, bali pia itapunguza gharama za uendeshaji kwa watumiaji wa vyombo hivyo vya usafiri.