Ushuru wa forodha: Trump aweka shinikizo kwa Korea Kusini na Japani

Ushuru wa forodha: Trump aweka shinikizo kwa Korea Kusini na Japani

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatatu, Julai 7, ameahidi kutoza ushuru wa forodha wa angalau asilimia 25 kwa nchi kadhaa, zikiwemo Japani na Korea Kusini, washirika wawili wakuu wa Asia. Kwa Washington, hii inakusudiwa kuhimiza washirika wake wengine kutia saini mikataba ya biashara haraka iwezekanavyo.

===
Rais Donald Trump siku ya Jumatatu(7/7/2025) alitangaza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Japani na Korea Kusini, pamoja na viwango vipya vya ushuru kwa nchi zaidi ya kumi ambazo vitaanza kutumika tarehe 1 Agosti, 2025.

Trump alitoa taarifa hiyo kwa kuposti barua kwenye mtandao wa Truth Social zilizoelekezwa kwa viongozi wa nchi husika, akiwatahadharisha wasijibu kwa kuongeza ushuru wao la sivyo Marekani itaongeza ushuru zaidi.

Katika barua zake kwa Waziri Mkuu wa Japani Shigeru Ishiba na Rais wa Korea Kusini Lee Jae Myung, Trump alisema kuwa ikiwa wataongeza ushuru wao, kiwango hicho kitaongezwa juu ya asilimia 25 alizoweka.

Ingawa barua hizo si makubaliano rasmi ya kibiashara, ziliashiria kushindwa kwa mazungumzo ya ana kwa ana. Trump alisisitiza kuwa lengo lake ni kufufua viwanda vya ndani na kufadhili punguzo la kodi alilosaini tarehe 4 Julai.

Waziri Mkuu wa Japani alieleza kuwa uamuzi huo ni “wa kusikitisha sana” lakini bado kuna nafasi ya majadiliano. Wizara ya Biashara ya Korea Kusini ilisema itaharakisha majadiliano ili kufikia makubaliano kabla ya tarehe ya mwisho.

Nchi kama Myanmar na Laos zitatozwa ushuru wa asilimia 40, Cambodia na Thailand 36%, Serbia na Bangladesh 35%, Indonesia 32%, Afrika Kusini na Bosnia 30%, na Kazakhstan, Malaysia na Tunisia 25%.

Trump alisema kuwa viwango hivyo vinaweza kubadilika kulingana na uhusiano na nchi husika. Ushuru huo mpya umeibua hofu ya kuyumba kwa masoko ya fedha na hatari ya mdororo wa uchumi.

Mpaka sasa, Trump amefanikisha mifumo miwili tu ya makubaliano ya biashara kati ya aliyodai kuwa 90 ndani ya siku 90. Marekani ilikuwa na nakisi ya biashara ya dola bilioni 69.4 na Japani, na bilioni 66 na Korea Kusini mwaka 2024.

Trump pia ametangaza ushuru wa asilimia 25 kwa magari, asilimia 50 kwa chuma na alumini, na asilimia 10 kwa bidhaa kutoka nchi wanachama wa BRICS kama China, Urusi, India, Afrika Kusini na nyingine.

Hii ni ishara kwamba mikataba ya awali aliyoingia na Japani na Korea Kusini wakati wa awamu yake ya kwanza haikutimiza matarajio ya utawala wake.

Pia soma >>> China yamuonya Trump juu ya ushuru, yatishia kulipiza kisasi
 
Naona Trampu anashindwa kula na vipofu naona anaamsha walio lala kabla hajamaliza anachokitaka
Yetu 👀🤔....
 
Back
Top Bottom