Ushuru wa gari kutoka Zanzibar

Ushuru wa gari kutoka Zanzibar

mabwiku

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
447
Reaction score
390
Msaada wadau, Kuna Gari nimeipenda ipo zanzibar na muhusika anasema Gari imekaa Miaka 2 kule, ni cc 1800 Toyota celica, nilipomuuliza kuhusu kodi akasema haizidi 2m kitu ambacho nimepata mashaka, kwa wajuzi naomba kueleweshwa kuhusu hili swala.
 
Mkuu kodi utakayopigwa utajilaumu Jiwe hataki maskhara kabisa kwenye pesa...kama vipi nenda ukajiridhishe.
Sawa mkuu sababu nasikia Gari ikiwa zenji imetumika kwa muda mrefu kodi inashuka.
 
Mkuu narudia tena Jiwe hana utani na hela...wapemba wanamuelewa vizuri nakupa mfano mdogo tu.

Kontena na la futi 40 la spea za pikipiki kodi kwa Zanzibar inacheza 5-7Milioni lakini huku Bara ni 40Milioni...Zenji magari rahisi lakini tatizo kuyatoa kule kodi ni noma baba ake.
Sawa mkuu sababu nasikia Gari ikiwa zenji imetumika kwa muda mrefu kodi inashuka.
 
Msaada wadau, Kuna Gari nimeipenda ipo zanzibar na muhusika anasema Gari imekaa Miaka 2 kule, ni cc 1800 Toyota celica, nilipomuuliza kuhusu kodi akasema haizidi 2m kitu ambacho nimepata mashaka, kwa wajuzi naomba kueleweshwa kuhusu hili swala.
pitishia Bagamoyo
 
Gari ni namba ipi Zenji? Anakudanganya hauwez kuwa Mill 2, ni zaid ya hapo, chukua kadi ya gari nenda nayo tra zanzibar then watakupa bei ya ushuru linalodaiwa ili kulitoa Zenji sababu wataangalia imeingia lini Zenji na ililipiwa sh ngap kodi
Baada ya hapo njoo bara waulize gari itatakiwa sh ngap ili iingie bara, tra wa hapa bara watataka kuona zanzibar imelipiwa au italipiwa sh ngap then nao wanaweka amount yao ambayo itakuwa juu zaidi ya zanzibar
Hayo yote unaweza Kufanya kwa kuuliza tu system ya TRA zanzibar then unakuja bara bila kulipia gari kwanza
 
Mkuu narudia tena Jiwe hana utani na hela...wapemba wanamuelewa vizuri nakupa mfano mdogo tu.

Kontena na la futi 40 la spea za pikipiki kodi kwa Zanzibar inacheza 5-7Milioni lakini huku Bara ni 40Milioni...Zenji magari rahisi lakini tatizo kuyatoa kule kodi ni noma baba ake.
Hili ni miongoni mwa "kero za muungano" lakini kiuhalisia, limekuwa na upotoshaji mkubwa. Gari ikitoka Zanzibar kwenda bara inalipiwa DIFFERENCE ya ushuru. Ushuru wa Zanzibar ni 40% ya ushuru kamili unaolipwa bara.
 
Gari ni namba ipi Zenji? Anakudanganya hauwez kuwa Mill 2, ni zaid ya hapo, chukua kadi ya gari nenda nayo tra zanzibar then watakupa bei ya ushuru linalodaiwa ili kulitoa Zenji sababu wataangalia imeingia lini Zenji na ililipiwa sh ngap kodi
Baada ya hapo njoo bara waulize gari itatakiwa sh ngap ili iingie bara, tra wa hapa bara watataka kuona zanzibar imelipiwa au italipiwa sh ngap then nao wanaweka amount yao ambayo itakuwa juu zaidi ya zanzibar
Hayo yote unaweza Kufanya kwa kuuliza tu system ya TRA zanzibar then unakuja bara bila kulipia gari kwanza
Zanzibar - ZRA
Tanzania - TRA

Sent from my SM-A720F using JamiiForums mobile app
 
Tafuta agent mwenye uzoefu wa kusafirisha magari kutoka znz kuja bara, atakupa mchanganuo wa garama zote kwasababu ziko nyingi usiangalie hiyo difference peke yake. Nilikua nikiishi znz nikanunua gari ambalo nilitumia zaid ya miaka 3, nilipoamua kurudi bara haikua rahisi kusafirisha lile gari japokua nilifanikiwa kulisafirisha.
 
UMETUACHA NJIANI KAKA...KWANI USITULETEE MCHANGANUO KWA GARI YAKO TUJARIBU PIGA HESABU
 
Hesabu hua iko hivi:

Kama hio celica ilivyoingia Zanzibar kodi ililipiwa Mil 3 na wkt huo kwny calculator ya TRA Celica hio celica kodi yake ni mil 6 then unalipia Mil (6-3)=3

Kifupi unalipia ile 'difference.'
 
Msaada wadau, Kuna Gari nimeipenda ipo zanzibar na muhusika anasema Gari imekaa Miaka 2 kule, ni cc 1800 Toyota celica, nilipomuuliza kuhusu kodi akasema haizidi 2m kitu ambacho nimepata mashaka, kwa wajuzi naomba kueleweshwa kuhusu hili swala.
Tatizo la magari toka Zanzibar unalinunua pamoja na jini lake....utashangaa unaendesha uko peke yako unasikia mtu anaongea na wewe au anakohoa toka chini ya chassis.
 
UMETUACHA NJIANI KAKA...KWANI USITULETEE MCHANGANUO KWA GARI YAKO TUJARIBU PIGA HESABU
Garama za znz
1. Kibali cha polisi
2.Meli
3.Wharfage
4.ZRB
5.ZMA
6.Difference ya kodi

Garama Dar
1.Wharfage
2.Agent fee
3.Kodi tena na usajili baada ya TRA ya dar kupokea file lako kutoka znz
 
Back
Top Bottom