Ushuru wa Maegesho: Sitaki kuamini kama uhuni huu wa TARURA una baraka ya Serikali

Ushuru wa Maegesho: Sitaki kuamini kama uhuni huu wa TARURA una baraka ya Serikali

Pole sana Mkuu

Upo mtindo mwingine wa kuisajili gari katika malipo ya siku ya sh 2500 bila ridhaa wala kutaarifiwa

Unakuta ulipark mahala kwa muda mfupi, lakn mtu wa maegesho sijui kwa maksudi au kuhakikisha hesabu yake ya siku inatimia anakusajili ktk mfumo huo, hapo ina maana gari yk hata kama inasimama kwa muda tu na huwa waipark ndani (mathalani ofisi zenye maegesho yao) basi we bill inakuwa yaongezeka.

Mpaka siku ukimpata mtu wa maegesho muungwana anakwambia ndugu umesajiliwa ktk kifurushi cha siku cha 2500, unajua hilo? Unabaki unashangaa tu na mbaya zaidi huwezi kumjua aliekusajili na wao hawajuani hvy mpk uende ofisini nako huko kuna danadana bhasi taabu tu

Kwa kweli kumiliki gari kwa mjini changamoto si mafuta ila gharama ndogo ndogo ambazo hazipo hata katika hesabu yako kama hizi, bado maegesho si salama sana nk. Mamlaka husika zifanyie kazi haya
Hili lakuwekewa gharama za cku nzima wakati umepark kwa hata nusu saa lipo Sana na hata ukienda kwenye ofisi zao, ushirikiano ni mdogo Sana. Kuna kipindi niliandikiwa nimepark slip way wakat tangu huu mwaka umeanza sijawahi fika huko. Unaweza kupark gari saa 11 jioni na mwisho ni saa 12 jion lkn utaandika gharama ya kutwa. Labda ujiongeze ukipark tu unampa jero yake, hapo hutoandikiwa. Inakera Sana kwa kweli
 
jana nmeangalia gari yangu ambayo toka niinunue haijawahi kukanyaga hata posta,au kkoo sabab napendaga sana kuingia mjini na boda.

nmekuja kukuta nina deni la 60k mpaka nikashtuka vibaya sana nikaangalia gari ambazo siko ofisini gari zote 22 zina madeni ya tarura mpka ile ilosajiliwa week ilopita
 
Mie nimekutana na mkeka huu hapa j3 wiki hii
20220926_134010.jpg
 
Kuna wengine wanaandika tuu number.. ukiangalia unakuta una tickets za sehemu ambazo hujawahi kufika kabisa
 
Back
Top Bottom