Pole sana Mkuu
Upo mtindo mwingine wa kuisajili gari katika malipo ya siku ya sh 2500 bila ridhaa wala kutaarifiwa
Unakuta ulipark mahala kwa muda mfupi, lakn mtu wa maegesho sijui kwa maksudi au kuhakikisha hesabu yake ya siku inatimia anakusajili ktk mfumo huo, hapo ina maana gari yk hata kama inasimama kwa muda tu na huwa waipark ndani (mathalani ofisi zenye maegesho yao) basi we bill inakuwa yaongezeka.
Mpaka siku ukimpata mtu wa maegesho muungwana anakwambia ndugu umesajiliwa ktk kifurushi cha siku cha 2500, unajua hilo? Unabaki unashangaa tu na mbaya zaidi huwezi kumjua aliekusajili na wao hawajuani hvy mpk uende ofisini nako huko kuna danadana bhasi taabu tu
Kwa kweli kumiliki gari kwa mjini changamoto si mafuta ila gharama ndogo ndogo ambazo hazipo hata katika hesabu yako kama hizi, bado maegesho si salama sana nk. Mamlaka husika zifanyie kazi haya