Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Tangu utaratibu wa ushuru wa maegesho uondolewe TARURA na kupelekwa katika halmashauri umegeuka kuwa wizi wa wazi wa serikali dhidi ya wananchi wake.
Mawakala wa halmashauri wanaohusika na kukusanya ushuru huo kwa kuvitoza vyombo vya moto vilivyoegeshwa wanafanya hivyo kimyakimya bila kuacha risiti yoyote lakini pia mwenye chombo cha moto hapati hata SMS ya kumtaarifu kuwa ameandikiwa ushuru wa maegesho.
Matokeo yake huyu mwananchi anashtuka ana madeni makubwa ambayo haujui yametoka wapi, na mbaya zaidi amepigwa na faini za kiendawazimu juu yake.
Utaratibu huu wa kijambazi kabisa pia unawawezesha mawakala wa halmashauri wanaotumiwa kukusanya ushuru huo kutoza ushuru mara nyingi watakavyo, yaani anaweza kuwa amelala zake nyumbani anarudia kuzitoza namba za magari aliyoyatoza jana.
Lakini pia mmiliki wa chambo anaweza kuwa amepaki sehemu moja kwa dakika 20 kisha akakuta umeandikiwa hata mara tano, na atakuja kujua kuwa uliandikiwa ikiwa ‘too late’ maana hakuna cha risiti wala SMS yoyote kumtaarifu kuwa ameandikiwa ushuru wa maegesho.
Kero hii imekithiri sana kwenye halmashauri za jiji la Dar es Salaam, labda kutokana na pressure za kufikia malengo ya makusanyo ya mapato.
TAMISEMI liangalieni hili, halmashauri zenu na mawakala wao wa kukusanya ushuru wanaichafua serikali kwa huu ujambazi wa mchana kweupe wanaoufanya.