Kwanza nikupe hongera mwana JF mwenzangu kwa wazo lako zuri la kibiashara.
Soko la magari hapa bongo bado ni zuri sana - usafiri ni wa shida sana siku hizi, na ukizingatia watu wengi, hata wale wenye mwaka mmoja kazini wana uwezo wa ku-afford economic cars ... so you will have plenty of market here.
Kwa maelezo yako, naweza kuhisi kwamba wewe haupo haba bongo - correct me if I am wrong ... na hili linaweza likazua vipingamizi vingi kibiashara, ukitegemea na utaratibu wa nchi yetu - rushwa bandarini, TRA .... haya nitayachambua zaidi baadae.
Kabla sijakupa mchakato kwa kukokotoa ushuru, kuna vitu vichache lazima uvifahamu ili uweze kufanikiwa vizuri kwenye hiyo biashara yako.
Watanzania wengi ni watu wanaopenda vitu vizuri hata kama hawana hela au uwezo wa kuvimiliki - so ushishangae kwanini mchina anasoko zuri la simu feki hapa kwetu.
"Bei" ni kitu cha muhimu sana - ukileta gari ukaweka malipo yako yote + faida, unaweza kushangaa hupati wateja kwa sababu ya bei. Watu wengi wamekua wajanja siku hizi na wanaagiza magari wenyewe toka Japan - so ni lazima uwaonyeshe ni "kwanini wanunue kwako na si kuagiza toka japan" - hapa jibu zuri ni "Bei nafuu, kuepuka usumbufu, kupoteza muda na risk nyinginezo"
Sasa turudi kwenye "Bei". Wafanya biashara wengi wanaingiza magari kinyemela. Ukweli ni kwamba, ukiingiza gari kihalali, ukaweka gharama zote ulizoingia na faida yako - bei inakuwa juu sana na "price tag" zako zitatishia watu! So, uwanja huu ni mpana na kuna technique kibao. Mimi sifanyi biashara ya magari, ila nafahamu watu wanaofanya hii biashara - kuna mzee mmoja ana yard hii njia ya bagamoyo road - kuna kipindi alikuja na gari 140 - usiulize gari moja iliingia kwa sh ngapi!
Na magari mengi unayoyaona kwenye car yard, sio yote yametoka japan - mengine yananunuliwa hapa hapa - yanakarabatiwa na kubadilishwa digits za speedometer - then mchezo unaendelea kama kawaida.
So, sisemi nawewe ufanye hivyo - just kwa sababu unataka uingie kwenye hii ngoma, ni vyema kujua wenzako wanafanyeje ili ujue jinsi ya kuwapiku kibiashara.
Hata hapo bandarini na TRA, kuna ujanja wake - ila sijui wanafanyeje. Business partner wangu yeye ana clearing and forwarding company - na pia huwa anaagiza magari na kuuza. Nilipotaka kununua gari, aliniambia nilipie CIF, then likifika bandarini nimwachie hiyo kazi.
Sijui aliliota kivipi - ila gharama zilikua ndogo kuliko nilivyodhani - so I think kuna kitu wanafanya, kutoa hongo au ujanja fulani hivi ambao hajawahi kuniambia.
Hapa napoandika hii e-mail, kuna Toyota RAV4 inabadilishwa piston rings, inatoa moshi si mchezo! Cha ajabu ina JAAI Test, na imepita bandarini. Gari kama hii sijui hata imepitaje pitaje, ila ndio itawekwa show room na kuna mtu atabamizwa bei - Tanzania hiyo!
Those are just few handy tools of the trade - mambo yapo mengi na mengine mi siyajui vizuri!
Sasa nije kwenye kukokotoa mapato.
Sina uhakika kama kuna tofauti ya ushuru kati ya magari ya Luxury na ya kawaida ... nadhani wataalamu zaidi hapa JF wataelezea hili.
Kwa magari yenye umri zaidi ya miaka kumi, kuna "Dumping Fee" 20%.
So mchakato ni kama ifuatavyo:
Parameters:
CIF = Cost Insuarance & Freight
DFR = Dumping Fee Rate (0% if less than 10 years old, 20% otherwise)
EDR = Exercise duty rate 25%
IDR = Import Duty rate (5% if < 2000cc, 10% otherwise) Hapa ndio nadhani unaanisha Luxury na Econonic cars.
VATR =VAT Rate 18%
Import duty fee = CIF x IDR/100
Dumping fee = (CIF + ID) x DFR/100
Exercise Duty fee = (CIF + ID + DF) x EDR/100
VAT = (CIF + ID + DF + ED) x 18/100)
Hizo ndio gharama uncle.
Kwa kifupi, TRA wanatumia Cummulative arthmetic, which means fee ya kwanza inaongezewa kwenye previous cost kabla ya kutumika ku calculate fee nyingine.
Order ya calculation ni
1) Import Duty
2) Dumping Fee
3) Exercise Duty
4) VAT
So, kama gari umelinunua $1000 CIF, cc 2300, la mwaka 1998.
Import Duty (ID) = 10% x $1000 = $100
Dumping Fee (DF) = ($1000 + $100) x 20% = $220
Exercise Duty (ED) = ($1000 + $100 + $220) x 25% = $330
VAT = ($1000 + $100 + $220 + $330) x 18% = $297
So, umeshajua ni kwanini watu wanatoa rushwa? Kama gari ni ya CIF $10,000? Pata picha!
Nadhani tupo pamoja!