Miaka 5 mbele inaonekana kuwa wazi kabisa kwa binadamu yeyote anaefuatilia muenendo wa nchi yetu mama nchi ya Tanzania.
Mimi ni miongoni mwa vijana wanaotamani kusoma masomo yake nchi zilizoendelea tangu utotoni lakini mpaka wakati huu nafasi imekua ngumu kupatikana inaezekana kwa sababu ya ufaulu,pesa au sababu nyingine nisizozijua au zilizo nje ya uwezo wangu
NINAIONA TANZANIA BORA KUPITIA USHUSHUSHU WA UJUZI
Mimi ni Moja ya wasomaji wazuri wa historia na ufuatiliaji wa michakato ya kiserikali. Nimekuwa nikitamani kusoma nchi zilizoendelea kwa sababu ujuzi walionao ni mkubwa kuliko wetu kwenye nyanja nyingi WATANZANIA tunaithamini TANZANIA na kuipenda nchi yetu lakini ninaamini mpo na mimi kuwa tunazidiwa ujuzi na wenzetu wa nchi zilizoendelea.
Kwa vile tumezidiwa ujuzi, TANZANIA inahitaji kuwaweka wazi wasomi waliopata nafasi za kwenda nchi hizo kuwa inahitaji ujuzi halisi kutoka nchi hizo zilizoendelea yaani mtu aende masomoni akijua anahitaji kurudi akiwa Bora kwenye ujuzi wa fani yake ikiwezekana awe Bora zaidi ya wale walioko nchini kule. Lakini pia TANZANIA inahitaji kumuonesha kumhitaji kwa kumpatia nafasi ya ajira arudipo nchini Ili kuhamishia ujuzi alioupata kwenye sekta za Kiserikali.
Wakati nikifuatilia mikanda mbalimbali ya sinema na kusoma vitabu, nimegundua umakini mkubwa wanaoweka watu wa bara la Asia katika kuzalisha watu walio hodari kwenye sekta binafsi. Mtoto akipaswa kuwa mrithi wa kampuni anapelekwa Ulaya au America kuchukua ujuzi kule na anarudi akiwa Bora Sana anaendesha kampuni kwa ustadi ulio bora zaidi na makampuni yao hukua pia. Katika kitabu kimoja alichokiandika Yericko Nyerere niligundua kuwa masomo nje ya nchi ni Moja kati ya sera zilizotumiwa vizuri na nchi zilizoendelea miaka ya hivi karibuni.
NCHINI KWETU USHUSHUSHU WA UJUZI UPOJE
Kwa Sasa suala la ushushushu wa ujuzi naweza kusema halijatiliwa mkazo nikiwa na maana kuwa ndio serikali kupitia balozi mbalimbali na Wizara ya Mambo ya Nje kwa ujumla wakishirikiana na sekta binafsi wanatoa nafasi za masomo nje ya nchi, lakini nafasi hizo ni chache na hazijazingatia usawa kwenye fani mbalimbali.
Ni kweli kabisa serikali katika kupunguza gharama za masomo hayo inapaswa kuzingatia fani zenye mahitaji makubwa kwenye nchi yetu kama fani za Tehama, Afya, Ukandarasi, Kilimo na nyinginezo lakini pia serikali yetu haipaswi kusahau kuwa hata hizi fani zisizopewa kipaumbele kwa wingi zinaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya taifa letu.
Nitatoa mfano kwenye sekta ya urushaji wa maudhui na utengenezaji wa maudhui nikiwa na maana content creators, producers na watengenezaji wa vipindi vya televisheni. Watu wengi wakati wa mapumziko yao hupenda kuangalia vipindi vya runinga na sinema, kama kuna wakati umewahi kuangalia sinema ya vitendo ya nchi zilizoendelea halafu ukawekewa sinema ya vitendo ya nchi yetu utaona utofauti mkubwa. Na pia kama utaangalia kwa wakati Mmoja mechi ya ligi ya EPL na NBCPL utagundua kwamba Kuna utofauti mkubwa wa urushwaji wa matukio ya Moja kwa Moja kwa nchi hizi mbili. Tofauti inabaki kuwa ni ujuzi kwa maana kuwa baadhi ya studio na vituo mbalimbali vya runinga na redio tayari vina vifaa Bora zaidi, lakini utakuta editing iliyofanyika ni Ile inayokatisha tamaa kabisa ambayo hata mtoto mdogo anasema hii ni editing.
Ninaamini Kila mmoja anakubaliana na mimi kuwa sinema, na runinga ni eneo linaloweza kuingiza pesa nzuri sana katika nchi yetu kama likiwekewa maanani pia kwahiyo serikali na sekta binafsi ikijali suala la ujuzi kwa usawa kwa fani nyinginezo Tanzania yetu itabadilika
NINI KIFANYIKE
Siku Moja nikiwa nafanya mazungumzo yangu na rafiki yangu Mmoja MTANZANIA anayesoma India shahada ya kwanza ya sheria niliwahi kumuuliza swali Moja kuwa "aliwahi kupata nafasi ya kukutana na uongozi wa nchi kabla ya kuondoka Tanzania au baada ya kufika India Ili kumhimiza kuiba ujuzi kwa nguvu zote"? Rafiki yangu yule alikataa, nikajiambia kimoyomoyo ningepata nafasi ya kuishauri wizara kwa kuwa idadi ya wateule wanaopata nafasi za kwenda kusoma nchi zilizo juu yetu kiuchumi sio kubwa sana ningeweka program ya kutoa mafunzo mkakati ya kuhakikisha kuwa wanaoenda kule wanaenda kwa fani zao pendwa kabisa na wanaiba ujuzi wa nadharia na vitendo kwa Hali ya juu na Wizara inawasikiliza kwa mahitaji yao punde wakimaliza masomo yao.
Pia ningehakikisha kuwa watu hao wanafuatiliwa maendeleo yao shuleni kwao hatua kwa hatua na kuhakikisha wanaleta manufaa, hili jambo lingeleta wataalam wazuri zaidi na wangefanya kazi wenyewe katika miradi mingi mikubwa kwa midogo.
Lingine ni kuhakikisha serikali haipotezi ujuzi kwa kukosekana ajira kwa vijana hao na pia kutafuta namna ya kumudu mishahara ya vijana waliopata kua Bora katika nchi zilizoendelea kwa maana wengi hushawishiwa na mishahara minono ya nchi za huko na kusababisha kuwakosa katika nchi yetu.
Suala lingine ni kubadili mfumo wa elimu katika nchi yetu kufuata mifumo ya vitendo kwa wingi kuliko nadharia ikiwezekana kijana wa Kitanzania asomee fani anayoona yupo na upendo nayo tangu akiwa katika umri mdogo Ili kujenga uelewa mkubwa hapo
Uchumi wa juu Tanzania unawezekana Serikali ni watu watu ni nguvukazi waliopewa dhamani wasikilize watu.

Upvote
10