Ushuuda wa TATU MZUKA waleta hamasa mtaani kwetu.

Puyugu 01

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
573
Reaction score
455
Tarehe 12/03/018 majira ya SAA 12:30 jioni hapa mtaani kwetu alionekana mama wa makamo ajulikanae kwa jina la mama Emmy akirukaruka na kwa furaha huku akikumbatia miti, kuibusu na kuikatia mauno, baada ya kusitisha furaha yake kwa muda, alisikika akisema nimepigiwa simu na Millard Ayo akinitambulisha kuwa nimeshinda TATU MZUKA kiasi cha Tsh. 3,000,000/=, Eeeh Mungu ahsante sana kwa kunipa million 3, alisikika akisema.

Baada ya Ushuuda huo, niliona akina mama rika kama lake, akina Dada na akina kaka walivyohamasika kwa kucheza mchezo huo wa TATU MZUKA kitu ambacho kimesababisha kuleta taharuki kubwa hapa mtaani pamoja na kuwahusia kuwa hiyo ni kamari na ni haramu hamutakiwi kujihusisha nayo hawataki kunielewa.

Jee, niwasaidieje hawa majirani zangu? mana hawasikii Hadhana wala Kengere ya Kanisa kisa TATU MZUKA.
 
Ni tangazo au
 
Naona Sasa Mmeamua Kuja Na Huku Kufanya Production

Sawa Bhana Hongeren
 
Tarehe 12/03/018 majira ya SAA 12:30 jioni hapa mtaani kwetu alionekana mama wa makamo ajulikanae kwa jina la mama Emmy akirukaruka na kwa furaha huku akikumbatia miti, kuibusu na kuikatia mauno.
Miti inakatikiwa mauno!
 
3 M hongera zake
Me nilishinda 10 elfu. [emoji1] [emoji2] [emoji2] [emoji119] [emoji119] [emoji119]
 
Probability ya 1 in a milion ni hatar sana....yaaan 1/1000000 daah,na mtu anaamin atashinda,na hapohapo wachakachue,aisee hal ni mbaya,the only real gamblin ni betting tu ya michezo,ambayo mi nakula deile na naliwa deile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…