Puyugu 01
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 573
- 455
Tarehe 12/03/018 majira ya SAA 12:30 jioni hapa mtaani kwetu alionekana mama wa makamo ajulikanae kwa jina la mama Emmy akirukaruka na kwa furaha huku akikumbatia miti, kuibusu na kuikatia mauno, baada ya kusitisha furaha yake kwa muda, alisikika akisema nimepigiwa simu na Millard Ayo akinitambulisha kuwa nimeshinda TATU MZUKA kiasi cha Tsh. 3,000,000/=, Eeeh Mungu ahsante sana kwa kunipa million 3, alisikika akisema.
Baada ya Ushuuda huo, niliona akina mama rika kama lake, akina Dada na akina kaka walivyohamasika kwa kucheza mchezo huo wa TATU MZUKA kitu ambacho kimesababisha kuleta taharuki kubwa hapa mtaani pamoja na kuwahusia kuwa hiyo ni kamari na ni haramu hamutakiwi kujihusisha nayo hawataki kunielewa.
Jee, niwasaidieje hawa majirani zangu? mana hawasikii Hadhana wala Kengere ya Kanisa kisa TATU MZUKA.