Usia wa Baba

Usia wa Baba

Joined
Jul 6, 2024
Posts
97
Reaction score
72
WANANGU WOTE
ZINGATIENI
ELIMU KWA MAANA ELIMU NDIYO MAISHA YENU MAZURI YA KESHO YENU
KUIKOSA ELIMU NI MATESO KWA MAISHA YENU YA KESHO.

Tukisoma Kitabu Cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 148
Mwl Julius Kambarage Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema
Elimu ni Kama Mlima mkubwa unaofika mawinguni ,
Kila unavyopanda ( mlima) ndivyo unavyoona vizuri Zaidi Upeo wa macho yako .
Tusipoazimia kujielimisha
Tutaachwa nyuma Tena Uhuru wetu utategemea tu huruma za watu wengine na Mataifa mengine ( na Wala) sio Uwezo wetu Sisi wenyewe.
Mwisho wa kunukuu
Tukisoma Biblia Takatifu
Waraka kwa Waebrania 3:7-8 unatueleza
Kwa hiyo Kama anenavyo Roho Mtakatifu leo ,
Kama Mtaisikia sauti yake,
Msifanye migumu mioyo yenu Kama wakati wa kukasirisha siku ya kujaribiwa katika jangwa.
Mwisho wa kunukuu
Jambo la kuzingatia ni kwamba
Ukizembea masomo
Maisha yako yatakuwa Magumu na mabaya yasiyokuwa na matumaini ya kesho yako .
Watu waliosoma
Kuna Nyakati
Watatumia Ujinga wenu wa kuto kusoma kuwaaminisha ya kuwa wao na ninyi mko sawa
Wasomi watawaambieni ya kuwa ninyi msiosoma na wao waliosoma wote mko sawa mbele ya Sheria .
Ajabu
Kwa Ujinga wenu wa kukataa kusoma
Mtakuwa mkiwashuhudia wasomi walisema mko sawa mbele ya Sheria wao wakisigina sheria bila ya kuchukuliwa hatua ila ninyi mliokataa Elimu mkikosea hata kosa linalostahili Kupewa onyo tu hamtafanyiwa hivyo Bali mtachukuliwa hatua Kali na mbaya ili mzidi kujazwa hofu
Na hofu zitawajaa kwa vile mtakuwa hamna uwezo wa kujenga hoja kwa sababu ya Makosa yatokanayo na kuidharau Elimu.
Mkiiweka juhudi katika masomo huku mkimtanguliza Mwenyezi Mungu mbele mjuwe kesho ya maisha yenu ni njema ,ninyi na vizazi vyenu vijavyo kwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Binaadamu
Ukikosa Elimu ujuwe watu wenye Elimu watatumia ujinga wako Kama kisa Cha kukunyonya na kujitajirisha wao.
Mwl Julius Kambarage Nyerere aliwahi kunukuliwa katika Kitabu Cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 153
Mwl Nyerere aliwahi kusema
Taifa ambalo watu wake hawajifunzi ( na) Wala hawaitumii Elimu Yao litabaki nyuma na kuwa maskini Daima.
Mwisho wa kunukuu
Leo hii tunashuhudia
Baadhi ya Mambo ya wasomi kukiuka Viapo vyao na kisha wao kwa wao kulindana huku wasiokuwa na Elimu wakiishi kwa huruma za wenye Elimu ambao Baadhi hujificha Kwenye kujitamkisha neno Mwenyezi Mungu huku wakiwa sio watu wa haki.
Na wasomi hao hutumia utaratibu huu kuwaaminisha Wasiosoma kuwa wao ni wenzao.
Tukisoma Biblia Takatifu
Hosea 4:6 maandiko Matakatifu yanatueleza
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa Mimi nami nitakukataa wewe
Mwisho wa kunukuu
Tuukwepe Mtego wa kukataliwa na Mwenyezi Mungu kwa kuitii Elimu na kusoma kana kwamba tutaishi Milele .
Watu walioikataa Elimu huishia kuwa watu Duni katika Maisha na kutumikishwa na watu walio na Elimu wakifanywa Machawa ambao kwa ugumu wa maisha wanaoupitia huwafanya hata kuukana Uzalendo na kuushikilia uchawa ambao huwafanya kuonekana Kama watu wenye changamoto ya akili kwani hata waonapo katiba na sheria za nchi zikivunjwa wao husimama upande wa watu waovu wavunjao Mifumo kwa faida Binafsi wasio na ucha Mungu Kwenye mioyo Yao wanye kujitamkisha maneno ya Mwenyezi Mungu kuwalaghai wasio na elkmu ili kuendelea kuwaonea.
Ni vtema wanangu kulijuwa hili.
Watu walisoma na kufaulu huwa watu wenye uelewa mpana wa kufanya Mambo makubwa yaachayo alama Kwenye hii Dunia .
Chagueni kusoma kwa bidii muwe Kama vile mmetumwa na Kijiji kwenda kusoma kwa Niaba ya wanakijiji ili kesho yenu ije iwe njema ikwepe mateso ya Baadhi ya Wasomi watumiao Ujinga wa watu Wasiosoma Kama kisa Cha wao kutengeneza maisha Mazuri ya wao na vizazi vyao vya kesho.
Waliosoma wote Wana maisha Mazuri
Wasiosoma wanaishi kwa mateso ya kufanywa
Vikaragosi
Vibaraka na vijibwa vya Wasomi.
Tukisoma Kitabu Cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 100
Mwl Julius Kambarage Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema
Hatukukubali hata punje moja kuwa Kuna watu fulani walioumbwa kutawala na wengine kutawaliwa
Mwisho wa kunukuu
Wanangu mkiikataa Elimu
Hamtajywa lolote lililo andikwa Kwenye ilani katiba kanuni miongozo na taratibu za kimfumo
Mtatawaliwa tu na kutegemea huruma za wapindishaji wa haki ambao hamtakuwa na uwezo wa kuzitetea kwa vile hatakuwa na Elimu na hivyo kulazimika kuwa vikaragosi vya wakubwa.
Tukisoma Kitabu Cha Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania uk 84
Mwl Julius Kambarage Nyerere aliwahi kuandika
Kukubali kufanywa vikaragosi vya Viongozi ni dalili ya woga
Si dalili ya heshima
Woga na heshima ni vitu viwili tofauti
Mwisho wa kunukuu
Wanangu mkiikataa Elimu mtakuwa vibaraka wa kuamrishwa kufanya lolote hata Kama nafsi yako haiko radhi na Jambo lile.
Tukisoma Kitabu Cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 104
Mwl Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema
Tumekataa Tanzania kuwa kivuli au kibaraka wa nchi nyingine.
Lakini tumekataa pia Mtanzania kuwa kivuli au kibaraka wa Mtanzania Mwingine.
Mwisho wa kunukuu
Ukosefu wa Elimu hupora Uhuru wa mtu na kumfanya kuwa Kama kijibwa koko mbele ya mwenye Elimu akitia huruma kuhurumiwa na mwenye Elimu .
Tukisoma Kitabu Cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 118
Mwl Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema
Daima hatutakubali kuwa vivuli wa vibaraka au vijibwa vya watu wengine au Taifa jingine.
Mwisho wa kunukuu
Niwaombe saana Wanangu
Yakwepeni mateso
Sikiliza sauti ya Mwenyezi Mungu inayokutaka uzingatie Elimu .
Achaneni na Mambo yote yasiyoitukuza Elimu.
Tukisoma Biblia Takatifu
Mithali 4:13 maandiko Matakatifu yanatueleza
Mkamate saana Elimu
Usimuache aende zake
Mshike ( hiyo Elimu)
Maana Yeye ( Elimu ) ni uzima wako.
Mwisho wa kunukuu
Baba wa Taifa hili la Tanzania
Mwl Julius Kambarage Nyerere
Aliwahi kunukuliwa Kwenye Kitabu Cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 153 akisema
Elimu ni kitu ambacho Sisi sote tunapaswa kuendelea nacho toka siku ya kuzaliwa mpaka siku ya kuiacha Dunia.
Mwisho wa kunukuu
Hata ndugu
zetu wenye Imani ya Kiislam wanaiamini Elimu
Tukisoma Kitabu Cha Sunnah za Mtume Mohammad SAW kiitwacho
Tarjuma ya Sahihi Al Bukhari uk 61 Kitabu Cha Elimu 3
Maandiko Matakatifu yanatueleza
Waumini wenye Elimu Wana daraja kubwa Zaidi kuliko wasio na Elimu hapa Duniani na kesho huko Peponi.
Mwenyezi Mungu hakupaswa kumuamrisha Mtume wake ( Swallallahu Alaihi Wasallam) amuombe kumzidishia kitu chochote ( kingine) isipokuwa Elimu.
Mwisho wa kunukuu
Baba wa Taifa la Tanzania
Mwl Julius Kambarage Nyerere
Tukisoma Kitabu Cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 150
Mwl Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema
Tumuombe Mwenyezi Mungu Atusaidie kuishi ili tujifunze Mambo mengi Zaidi juu ya Maajabu yake katika Ulimwengu huu tunaoishi na tujipatie faida za maisha haya sisi Wenyewe ,
Watoto wetu
Na nchi yetu.
Mwisho wa kunukuu


Ndimi

Baba yenu

Mathias Mugerwa kahinga
 
Back
Top Bottom