Usibadili gari yako kutoka kawaida kwenda push start

Usibadili gari yako kutoka kawaida kwenda push start

Mkuu gari ina reflect personality ya mwenye gari kwa mfano picha za hizi JZX110 hivi ni sawa sawa ila zina reflect personality 2 tofauti...

View attachment 1929792

View attachment 1929793

View attachment 1929794

View attachment 1929795

View attachment 1929796

View attachment 1929797

View attachment 1929798
Modification ambayo siwezi kuifanya kwenye gari yangu ni ya kujaza hayo maplasticks around the car bottoms (BodyKits).
Wala kuweka rim design za hio purple ama nyeupe angalau hio chrome imekaa decent kidogo ila maplastick its a big no! Ma ngao pia its a big No!
 
Zile rubber zunasaidia mlango wako usikwangue rangi ya gari lililopaki karibu na wewe endapo nafasi ni finyu pale unapofungua mlango...
Pia ni urembo japo sizipendi hata kidogo...
Zingekuwa atleast nyembamba basi binafsi rangi ikichubuka tutapaka upya haina shida ila siweki ule upuuzi😅
 
Modification ambayo siwezi kuifanya kwenye gari yangu ni ya kujaza hayo maplasticks around the car bottoms (BodyKits).
Wala kuweka rim design za hio purple ama nyeupe angalau hio chrome imekaa decent kidogo ila maplastick its a big no! Ma ngao pia its a big No!
Tuanzie hapa una gari gani mzee? Usikute gari yako haissupport mods..hizo..
 
Usibadili gari yako kutoka funguo ya kawaida kwenda push start..hii ni kwa sababu unapunguza usalama wa gari lako ambapo ni rahisi sana kuliwasha kwa kuunga waya tu

Kwa kawaida gari inapotoka kiwandani iwe push start ama kawaida imewekewe ulinzi maalum wa mfumo wa ku lock steering unapoizima gari ..ambapo mfumo huo ni mfano wa kufuli la chuma ambapo huwezi kuivunja mpaka ufungue na funguo husika ndipo linafunguka na linapofunguka steering ndipo inakua huru kuzunguka unapokata kona.

Gari zinazokuja na push start zina mfumo wa kufuli la umeme ambalo hufunguka automatically pale ambapo antenna za ndani zinaponasa mawimbi ya kielektroniki ya funguo ama remote ya gari husika na hufunga pale unapozima gari.

Kwa gari ya kawaida kufuli hufunguka unapochomeka na kuzungusha funguo wakati uapotaka kuwasha na hulock pale unapozima gari na kuchomoa funguo

Sasa basi kwa sababu gari ya kawaida isio push start kufuli lake hufunguliwa tu na funguo yake ya mechanic ukitaka kufunga mfumo wa push start utalazimika kuchomeka funguo kwanza kutoka lock ya kufuli.. hivyo kwa sababu hiyo wanaofunga wanalazimika kuondoa kabisa kufuli la ku lock steering na kuiacha ikiwa free .muda wote kitu ambacho kwa usalama wa gari lako umeshapungua kwa asilimia 50

Tatizo la pili ni kua kwa sababu wanaondoa kabisa kufuli na kufuli ndio lina connector za umeme zinazowasha gari na kuweka switch on na acc wanakata waya na kuziunganisha kwenye mfumo?wa push start (kumbuka mfumo huu sio rasmi hivyo una mapungufu mengi) ili mfumo huu uunganishwe na mfumo wa gari..Sasa basi kuna uwezekano mtu asie mwema akatumia zile waya zilizokatwa na akaziunganisha gari itapiga starter na itawaka pia na kuna uwezekano akaondoka nalo kiulaini sana

Kumekuwa na kesi za watu wengi kuibiwa magari sana ,ni muhimu sana kuzingatia usalama wa gari lako na ulizi usifanye mambo kwa kuiga huo ndio ukweli yana gharama kubwa sana za kiusalama. Ushauri Kama unatamani gari la push start ni bora uuze ulilokua nalo ununue lenye mfumo wa push start iliotoka nalo kiwandanani

Kwa ushauri wa mifumo ya funguo tafadhali tembelea page yetu instagram.com/smart_keys_tz
Simu namba 0657587593

Tunafanya programming ya funguo za sensor na remote za push start kwenye mfumo ulokuja na gari.

Kwa waliopoteza na wanaohitaji za spea kwa magari aina zote.

/-View attachment 1920439

sent from HUAWEI

Zipo Security na Alarm systems ambazo ni advanced, Ingawa they are a bit complicated kwenye installation, in such a way siyo kila mtu ataweza kufanya.

Achana na hizi mtu anatoa lock gari yake badala yake inatoka kwenye gari ya mtu mwingine ambaye naye ana mfumo kama huo.
 
Back
Top Bottom