Naomba niwatie moyo wote wanaotafuta kazi bila mafanikio .
Wakati nimemaliza degree yangu miaka ya nyuma kidogo, nilikaa kwa muda wa miaka miwili bila kupata kazi, Kila ninapopeleka application siitwi, ila nakumbuka niliitwa katika shirika moja kubwa tu lisilo la kiserikali kwa ajili ya interview.
Nilifika kufanya usahili na tulikuwa Kama watu Saba na walikuwa wanataka Mtu mmoja katika nafasi tuliyoomba.
Nakumbuka nilijiandaa Sana katika intervew hiyo, na niliamin lazima nitaitwa kuanza kazi, kutokana na jinsi nilivyojibu maswali yangu.
Nilisubiri kuitwa kazini bila mafanikio, baada ya Kama mwezi nikarudi kuuliza vipi Kama washaita, nikapewa jibu la tayari mtu ashaanza kazi, niliumia sana mpaka niliokuwa naongea nao walinionea huruma.
Mmoja wa niliokuwa naongea nao akanambia Kama ungeweza Kuna nafasi moja ila sijui kama unaweza kuifanya ni office attendance na mshahara ni laki tatu.
Kwa jinsi nilivyokuwa na uhitaji wa kazi na kwamba nimesota nyumbani bila kazi na maisha ya kukaa nyumban yalivyo magumu nikamwambia niko tayari kuifanya mpaka wakashangaa nikaambiwa nirudi kesho yake kuanza kazi.
Wakuu nilianza kazi Kama muhudumu wa office bila aibu yoyote japo yataka moyo, lakini nilifanya tena kwa ufanisi mkubwa, nilikuwa na adabu, Kila aliyenituma wengine niliwazidi elimu, nilienda , watu walinipenda na kunisifia ufanyaji wangu kazi.
Baada ya miezi mitatu amini usiamini niliajiriwa hapo kwa nafasi inayoendana na elimu yangu, nilishukuru sana na kuamini sometimes Mungu anataka ujishushe ili akuinue.
Hivyo, nakutia moyo ndugu yangu unaetafuta kazi sometimes jishushe ile Mungu akuine.
Najua uzi ni mrefu ila kuna cha kujifunza.