Usichague ya kusikia dhidi ya umpendaye, hata mabaya yake yasikie

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
USICHAGUE YA KUSIKIA DHIDI YA UMPENDAYE, HATA MABAYA YAKE YASIKIE✍️

Sababu kubwa ya kushindwa kumsamehe ni kwa sababu ulimuona kwa upande mmoja tu hukutaka kujua ya upande wake wa pili na hata uliposikia ulijua anazingizishiwa.

Tunakwama sana hapo pale tunapopenda tunamuulizia kwa yale tunayotaka kuyasikia tu na ikitokea unaambiwa yale usiyotaka kusikia basi utapinga vikali.

Ukomavu ni kumpenda hata baada ya kujua mazuri na mabaya yake kisha ukachagua mazuri yake ikiwa tu yanazidi mabaya yake.

Ni udhaifu sana kujipa upofu wa kutataka kujua mabaya yake na kitachotokea ni kuwa utajipa UPOFU ila kuna siku utajionea mwenyewe na hapo UTASHINDWA KUKABILIANA NA HALI HIYO.

Kuna usemi wa kihenga usemao UPOFU KWENYE MAHUSIANO HUWA UNAISHA SIKU UKIPIGWA TUKIO sasa usisubiri ufike huko wewe fahamu upande wake mbaya kisha Jiambie kweli utaweza kumpenda bila kuathiriwa na upande wake mbaya?

#mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako.
 
Kwanza kwanini uulizie mambo yake? Kama upo naye katika uhusiano utayajua yote, na uamuzi ni wako mwenyewe baada ya kuyajua.

Binafsi mambo yake kabla yangu sio shida zangu, tunaanzia tulipoanzia.
 
familia yenye amani na furaha unaijenga kwa mikono yako mwenyewe ..usisikize ya majirani
 
Usikie ya nini? Umshindwe kwa uyaonayo,akutendeayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…