JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kuhariri ni kazi muhimu sana kwenye tasnia ya kupasha habari. Nakala ambayo haijahairiwa si vyema kutumwa kwa umma kwa kuwa mara nyingi huwa na makosa kutokana na waandishi kufanya kazi kwa haraka sana.
Timu ya uhariri, inayoitwa pia dawati la wahariri, inafanya kazi kubwa ili kuhakikisha kuwa nakala inakuwa safi.
Kuhariri andiko kabla ya kutuma kwa umma ni muhimu kwa sababu:-
Nakala iliyohaririwa vizuri huwa na muundo unaosomeka vizuri na hutimiza lengo la kupasha watu habari.
Huepusha uwezekano wa kutuma andiko lenye makosa yanayoweza kugharimu chombo cha habari.
Inahakikisha ujumbe ulioandikwa unalingana na kile kilichokududiwa kusemwa.
Husaidia kuambatanisha na kuboresha ufanisi wa maandishi.
Kuunda mtiririko mzuri wa mawazo na kutengeneza mantiki.
Upvote
0