Usichokijua kuhusu Usingizi

Usichokijua kuhusu Usingizi

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
1_20241121_030804_0000.png


Kulingana na ripoti ya CDC, inaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya watu wote waliopo duniani hawapati Usingizi wa kutosha.

Kutengeneza mazoea ya kulala kwa wakati kunaweza sababisha kuboresha hali yako ya afya na kupata Usingizi Bora kwa ujumla.

Kuna formula inaitwa 10-3-2-1-0 hii ni kanuni muhimu kwenye kukusaidia Akili na mwili wako kujiandaa kupumzika na kulala salama bila shida yoyote.

⚙️ Ndani ya masaa 10 kabla kulala Upaswi kunywa kahawa:
unywaji wa kahawa unaweza pelekea kuvurugika mzunguko wako wa kulala unapofika mda wa kulala. Kikombe kimoja cha kahawa uchukua masaa 3 - 7 kukaa mwilini hivyo ili mwili uweze kuiondoa uchukua saa 10.

2_20241121_030804_0001.png


⚙️ Masaa 3 kabla ya kulala usile chakula kingi au pombe:
Matumizi ya pombe upelekea mtu kukosa Usingizi Bora kwani usababisha kuamka mara kwa mara usiku.
3_20241121_030804_0002.png


Pia epuka kula ndani ya masaa 3 kabla ya kulala kwani ulaji wa vyakula vya mafuta mengi, kukaanga na sukari upelekea kukosa Usingizi kwa wakati.

⚙️Masaa 2 kabla ya kulala hakuna kazi za ziada:
Kumaliza kazi zako na kupumzisha Akili yako kabla ya kulala kutasaidia kuweza kuboresha ubora wa Usingizi wako kwa kutuliza Akili yako baada ya Kazi.

4_20241121_030804_0003.png


⚙️lisaa 1 kabla ya kulala usipende kuangalia mwanga:
Unashauri kutotumia simu, kompyuta, tablet au kifaa kingine chochote lisaa limoja kabla ya kwenda kulala. Ikiwa una tabia ya kutumia simu ndo ulale basi uifanya Akili yako kushindwa kuwa imara.

5_20241121_030804_0004.png


Jitahidi unapolala ukaweka Alarm basi zisiwe nyingi kwani itakupelekea kuwa mvivu wa kuamka hakikisha Alarm Moja tu i
natosha kukuamsha.
 
Kuna wale ambao kusinzia hadi wawe wameshikilia simu juu kwa juu kitandani mpaka wadondokwe.
 
Uhakika bro tumekupata
Rayns huwa unalala saa ngapi??

Saa kumi mkuu, af naamka saa 4...
Ila hapo kwenye masaa 3 kabla ya kulala usile chakula kingi nitalifkiria maana milo yenyewe miwili tu😂
 
Back
Top Bottom