Jerlamarel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2021
- 843
- 2,525
"Upendo wa Kirumi" ni kisa cha kielelezo cha mwanamke, Pero, ambaye alimnyonyesha baba yake, Cimon, kwa siri baada ya kufungwa na kuhukumiwa kifo kwa njaa.
Picha hii ya mwanamke akimnyonyesha mzee ndani ya Selo aliyokuwa amefungwa iliuzwa kwa Euro 30 Milioni sawa na Bilioni 69.5 Fedha ya TZ. Picha inaweza onekana ni ya kawaida lakini ina rekodi kubwa ya historia nyuma yake.
Mwanaume masikini unayemuona kwenye picha alihukumiwa “Kifo Kwa Njaa” kwa kosa la kuiba mkate kipindi cha utawala wa Louis wa XIV huko Ufaransa.
Huyo Mwanamke alikuwa ni binti yake wa pekee na ndiye pekee aliyeruhusiwa kutembelea Selo hiyo, aliruhusiwa kumtembelea kila siku lakini kwa zuio kubwa kabisa la kutokuingia na chakula katika kumuona huko.

Baada ya miezi minne (4) kupita, Huyu mzee alikuwa bado mzima na hata dalili ya kupungua uzito haikuonekana. Mamlaka zilitatanishwa na hali hiyo ikabidi waanze kufanya upelelezi kwa mtembeleaji wake.
Jambo lililowashtua katika upelelezi huo ni kumuona binti huyo akimnyonyesha baba yake mpaka anashiba kabisa, mjukuu akishiriki ziwa na babu yake.
Jambo lililowashtua katika upelelezi huo ni kumuona binti huyo akimnyonyesha baba yake mpaka anashiba kabisa, mjukuu akishiriki ziwa na babu yake.
Majaji walitambua ukaribu na upendo wa juu kabisa wa binti kwa baba yake, Wakamsamehe baba huyo na kumuachia huru.