Frumence M Kyauke
JF-Expert Member
- Aug 30, 2021
- 630
- 1,262
Kuna baadhi ya watu wanadhani shetani ni jambo dogo, ile ni nguvu kubwa iliyoshinda binadamu wote. Utakapojaribu kuingia kwenye ugomvi na yeye ndipo utatambua kuwa unajaribu kupigana na jambo usiloweza. Kwa reference fupi, wapo mitume waliojaribu kupambana naye wakaishia kupata adhabu kali zisizoelezeka.
Wakwanza ni Yesu, mwana wa Mungu alipojaribu kupambana nae aliishia kusulubishwa. Ayubu mcha Mungu alipata kipigo kikali sana alipomcha Mungu, Adam na Hawa pamoja na utashi wao wote walitiwa kwenye 18, mitume ikiwemo Stephano walipigwa na mawe mpaka kufa walipoingia kwenye vita na shetani.
Unaposema unataka vita na shetani labda pepo ila sio shetani aliyemsulubisha Yesu, vinginevyo utaishia kuchapwa kipigo kitakatifu.
Jiulize je, kama Yesu na nguvu zake zote alisulubishwa vibaya sana wewe atakufanyia jambo gani?