Usidharau hatua zako ndogo bali ziunganishe kwa nidhamu ili upate umbali mrefu

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
471
Reaction score
1,217
Kama wasemavyo maisha ni hatua ndivyo ilivyo japo inahitaji nidhamu na subira ya juu sana kuunganisha hizo hatua ili upate umbali mrefu.

Ukimuona mtu yupo mbali kwenye jambo fulani kuna uwezekano mkubwa alianza na hatua ndogo ndogo ambapo zikiwekwa pamoja ndio huo umbali alionao sasa.

Kudharau hatua ndogo ni nidhamu mbovu itakayokukwamisha kufikia hayo malengo yako makubwa uliyonayo na dharau hiyo ndio mwanzo wa kupoteza subira kwa sababu utataka uanze leo na ufike kesho.

Kuna watu wengi tu mpaka leo bado wanasubiri mitaji mikubwa ndio waanze ila wale ambao walianza na mitaji midogo waliyokuwa nayo tayari wako mbali sasa ila wewe unaendelea tu kusubiria upate huo mtaji mkubwa ndio uanze.

Wapo waliojaliwa kuanza kwa hatua kubwa (wachache) na kuna sisi ambao huo uwezo mkubwa hatuna bali tunatakiwa tuanze na tulichonacho kwa nidhamu ili tufike tunapotarajia

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako
 
Mhm kibongo bongo , kama sio mwanasiasa upige dili za kikax tu kinyume na hapo uzuge na hizo hatua ndogo ila ndani yake unajua wap unapiga kibingwa, yani nyuma yako kuwe na kundi kubwa linalia juu ya hizo hatua zako😆
 
Wewe Jamaa Noma!
 
Muogope Mungu
 
Kama wasemavyo maisha ni hatua ndivyo ilivyo japo inahitaji nidhamu na subira ya juu sana kuunganisha hizo hatua ili upate umbali mrefu.

Ukimuona mtu yupo mbali kwenye jambo fulani kuna uwezekano mkubwa alianza na hatua ndogo ndogo ambapo zikiwekwa pamoja ndio huo umbali alionao sasa.

Kudharau hatua ndogo ni nidhamu mbovu itakayokukwamisha kufikia hayo malengo yako makubwa uliyonayo na dharau hiyo ndio mwanzo wa kupoteza subira kwa sababu utataka uanze leo na ufike kesho.

Kuna watu wengi tu mpaka leo bado wanasubiri mitaji mikubwa ndio waanze ila wale ambao walianza na mitaji midogo waliyokuwa nayo tayari wako mbali sasa ila wewe unaendelea tu kusubiria upate huo mtaji mkubwa ndio uanze.

Wapo waliojaliwa kuanza kwa hatua kubwa (wachache) na kuna sisi ambao huo uwezo mkubwa hatuna bali tunatakiwa tuanze na tulichonacho kwa nidhamu ili tufike tunapotarajia

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako
Upo sahihi kabisa mkuu
 
haya mambo ya subira matokeo yake unaingia third floor huna ramani
Maneno ya kimotivation ni kwa ajili ya mataifa yaliyoendelea , huku kwingine ni kuchukua maamuzi kama simba awindavyo, pesa iliyopo kwenye mzunguko ni ndogo kuliko wahitaji hivyo hapo ni vita ya tatu ya dunia.
 
Back
Top Bottom