Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Wadau!
Kama kichwa cha huu uzi kinavyosomeka hapo juu.
Swali la kujiuliza 🤔
Kwa nini binadamu aliyeifanyia makubwa Chadema, aliyejenga wasifu wa kipekee na uliotukuka kwenye siasa za upinzani na kupigania demokrasia Tanzania, Freeman Aikaeli Mbowe, jana alfajiri aliangushwa aliyekuwa msaidizi wake, Tundu Antipas Lissu?
Majibu ya swali hilo yanajibiwa na hoja mbili hizi hapa chini
1. Chama cha siasa kina mapenzi ya majira.
Leo kitakupenda sana, kesho kitakupuuza, keshokutwa kitakuchukia. Chama cha siasa kinaweza kukupamba kama shujaa asubuhi, jioni kikatangaza kuwa adui, usiku kikakufukuza.
2. Wanasiasa hukosea kuegemeza maisha yao kwenye vyama vyao.
Chama cha siasa hakina utu, kinaweza kukung'ang'ania mfe wote kisiasa, kama Prof Ibrahim Lipumba na Cuf, au kikakuua kwanza, kisha chenyewe kikaenda kufa sehemu nyingine, mithili ya James Mbatia na NCCR-Mageuzi.
Fanya siasa kwa akili. Wanachama na viongozi wenzako kwenye chama, siyo familia yako.