Usiende F.5 ili uwahi kupata ajira mapema zaidi. Nawasanua kama hivi

siyo somehow, jamaa yuko sawa kabisa

Engineers hasa huko tanesco, wanamsomesha technician, akimaliza anarudi kuwa Engineer
technician(na artisan) nafasi za ajira nyingi maana yeye ni mzalishaji
Muache aendelee kuimba somehow
 
Umesema kweli lkn F 4 anasoma Dip kwa miaka 3 sio miwili
 
Hao wanapewa vipaumbele sababu ya vimishahara vinavyolipwa kwenye hio sehemu wanayotoa ajira, wanaona kabisa wewe na degree yako pamoja na huo mshahara watakaokupa lazima kazi utafanya kimagumashi
Ndio washakosa sasa, the end justify the mean.
 
Mimi chuo nilisoma na waliotoka diploma first class mbona walikuwa wanakula sup alafu tuliotoka 6 tunalala bweni tu na ma Gpa ya juu


Fuata mfumo F.6 inaadvantage yake
 
Hawatanielewa mpaka kitaa kiwape elimu kwanza live in hard way
 
Mimi chuo nilisoma na waliotoka diploma first class mbona walikuwa wanakula sup alafu tuliotoka 6 tunalala bweni tu na ma Gpa ya juu


Fuata mfumo F.6 inaadvantage yake
Hujaelewa kilichoandikwa. Unaonaje ukisoma tena na tena.

Hints: Kikawaida wanaokwenda Dip ni wale walioshindwa kufanya vizuri zaidi F.4. Siwazungumzii hawa.

Bali nawazungumzia vipanga wa Div 1 pt 7 mwisho 14 waende Dip. Sioni ni kwa namna gani wewe mwenye utakuwa na umaalum wa kusoma bwenini upige GPA kali umuache mwenye Dip na Div 1 yake ya pt 7? Sioni....labda itokee kazembea kimasomo tu ila sio eti umemzidi kwa akili za kimasomo
 
Upo sahihi mkuu...nimekumbuka mwaka fulani kuna kiwanda kilikua kijajengwa maeneo fulani pakahitajika

Engineer mmoja
Technician mmoja
Artisan saba
Project ilivyoanza baada ya mwezi mmoja Technician akapigwa chini kwa kua alikua alikula parefu halaf kazi anazofanya ni hizo hizo tulizokua tunafanya maartisans japo kielimu tulikua hatumfikii
 

Nimekuelewa
Kuna waajiri wana bias wanataka vyeti vya 6


div 1.7 or whatever chuoni ndio mnakutana wote , chuoni wengi unakuta nikawaida kabisa mnasota wote na mnachomoka wote wachache sana wanamaintain ufaulu ule ule
 
Ulichoandika ni sahihi sana kwa yule anayesoma aje apate ajira. Wazo lako halina tofauti na wale waliokuwa wamepiga vizuri six lakini wakaenda education kimakusudi ili wawe na uhakika wa ajira Magu akawashangaza. Form six faida yake kubwa ni kutambulika maeneo mengi.. scholarship kibao. Cheti cha diploma ni sawa na kujifungia fursa zingine. Cheti cha six unakuwa na uwanja mpana wa kusomea vitu vingi. Kuna jamaa yangu alisoma UDSM computer science akaona kitaa haimlipi akarudi Arusha Tech na kusoma civil. Sasa hivi ni mhandisi kwenye miradi ya maji. Cha muhimu pale six kijana afaulu vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…