Usiende kuoa Tanga

poleni

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2013
Posts
237
Reaction score
630
Mpwa wangu

Imeshapita miaka, toka liposhika peni.
Lile jambo silotaka, naona lipo mezani
Mtunzi atiririka, kwa beti zisizo kifani
Kijana mwana wa kaka, Tanga wenda fata nini?

Yanishangaza barua ndefu, uliyoiandika,
Akili ukazuzua, misemo kusikika
Tanga bahari ya nzoa, kwa huba yasifika
Bure utajisumbua, nenda oa lipotoka

Imekudatisha pishi, na kanga za mwilini
Wajuvi tushiriki, mpwa wangu watakani
Ni viuno tetemeshi, wawapo huko ngomani
Au umemfuata mishi, mwanangwa wa chumbageni

Wataka kwenda Korogwe, ukatafute mwandani
Akili ikavurugwe, umletapo mjini
Mchuzi kutiwa ngogwe, si utamu wa chumbani
Kwa mganga ukarogwe, hayo ndio mapenzi gani?

Siku hizi si wastara, wake wa Tanga mjini
Wanayabana madera, wakivaa na vimini
Midomo wanaifura, ati watoto wa pwani
Utajapata hasara, ututie lawamani

Naona nasema mengi, na wino meniishia
Ila jambo la msingi, fata nililokuusia
Ati maji yana rangi, ila huwezi ijua
Kaka yangu majimengi, salam tampatia
 
Jamani [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Mbona mnavuruga anayetaka kuja oa huku?? Hayo ndio mapenziye yalipo na kama ujuavyo moyo ukishapenda tena ni ngumu kubadili mawazo papo kwa papo

Mbaya halisi na wema hakosi bana!
 
Ya kale sio ya sasa,Tanga iliyosifika
Imejazwa na mikasa,na mambo yakuabika
ujinga wa mambosasa,Midume hina yapika
Tanga ya leo si jana,oa ulipozaliwa.

Ebu pita chumbageni,Ingia na ngamiani
Ona mambo ya kigeni,watu kama hayawani
Fatuma,Juma na Jeni,bwana wao ni Shabani
Tanga ya leo si jana,Oa ulipozaliwa.

Mambo ya pale La Casa,wala si yakusimulia
Kumejaa uhanasa,wamezingwa na dunia
umuachaje hamisa,Latifu akuvutia?
Tanga ya leo si jana,Oa ulipozaliwa

Hapa mwisho namaliza,nenda kaoe nyumbani
Usije ukatuliza,kwa mambo ya kishetwani
Jambo bora kuuliza,usije panda mwambani
Tanga ya leo si jana,Oa ulipozaliwa.
Kiminyio...29/11/2017.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…