poleni
JF-Expert Member
- Mar 9, 2013
- 237
- 630
Mpwa wangu
Imeshapita miaka, toka liposhika peni.
Lile jambo silotaka, naona lipo mezani
Mtunzi atiririka, kwa beti zisizo kifani
Kijana mwana wa kaka, Tanga wenda fata nini?
Yanishangaza barua ndefu, uliyoiandika,
Akili ukazuzua, misemo kusikika
Tanga bahari ya nzoa, kwa huba yasifika
Bure utajisumbua, nenda oa lipotoka
Imekudatisha pishi, na kanga za mwilini
Wajuvi tushiriki, mpwa wangu watakani
Ni viuno tetemeshi, wawapo huko ngomani
Au umemfuata mishi, mwanangwa wa chumbageni
Wataka kwenda Korogwe, ukatafute mwandani
Akili ikavurugwe, umletapo mjini
Mchuzi kutiwa ngogwe, si utamu wa chumbani
Kwa mganga ukarogwe, hayo ndio mapenzi gani?
Siku hizi si wastara, wake wa Tanga mjini
Wanayabana madera, wakivaa na vimini
Midomo wanaifura, ati watoto wa pwani
Utajapata hasara, ututie lawamani
Naona nasema mengi, na wino meniishia
Ila jambo la msingi, fata nililokuusia
Ati maji yana rangi, ila huwezi ijua
Kaka yangu majimengi, salam tampatia