Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
Rafiki yangu mwema yawezekana maisha unayoishi si maisha uyatamaniyo uje uyaishi
1. Yawezekana umeumizwa sana na yule mtu uliyemwamini sana, umepata hasara, umefail au yawezekana nuru na tumaini limepotea kwasababu ya hilo unalokabiliana nalo sasa.
2. Yawezekana nisivivae viatu vya hali yako uliyonayo sasa, yawezekana unajiona wewe uliumbwa kukosea tu. Yawezekana unahisi huwezi kusimama tena kwa hali hiyo uliyonayo
3. Yawezekana ndugu na watu wako wa karibu ukiwaeleza unachopitia hawakuelewi, wanazidi kukukandamiza na kukunenea maneno makali yanayokuumiza zaidi badala ya kukupa faraja
4. Yawezekana unaona umechelewa sana au umeshapoteza mwelekeo, umepoteza thamani, umepoteza muda wako na vitu vya thamani
Naomba nikuambie kuwa maisha ya siri zito, wakati mwingine kesho zetu njema zinajengwa katika maanguko tunayoyaona ni mwisho wetu.
Wakati mwingine Mungu Baba huwa anondoa ili kubadilisha na njia za Mungu za kuondoa ili abadilishe zinaweza kuwa njia zenye maumivu kweli ila Mungu huwa anayo sababu juu ya hilo
Unakumbuka Abigail yule aliyeolewa na Nabal (mume asiyefaa) Mungu aliamua kufanya kitu, mabadaliko kwenye kesho ya Abigail iwe njem
Unakumbuka Yusuph alipouzwa aliona huo ulikuwa ndio mwisho wake. Kumbe kuuzwa kwake ndio kulitengeneza ukuu wake ugenini
Rafiki wewe si wa kwanza wala hutokuwa wa mwisho, hutakiwi kabisa kujiinamia na kukata tamaa katika hilo. Nyanyuka bado lipo tumaini
Kesho yako njema wakati mwingine unapaswa kuilipia gharama. Inuka sasa, sogea utamanipo kuwa bado lipo tumaini la kesho yako njema. Usisuse, usiendelee kujiimania na kujilaumu sana. Kujilaumu hakutabadilishi chochote ila amua kufanya kitu kwa hiyo hatma uitamaniyo.