Usifanye Makosa haya, ili kuepuka madeni yasiyo ya lazima

KJ07

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2021
Posts
2,370
Reaction score
5,381
Salaam wakuu.

Wahenga walisema Tahadhali ni bora kabla ya hatari, na umakini unalipa kuliko uzembe, na akili ni njema kuliko ujinga, na utoshelevu ni bora kuliko kupungukiwa.

Mpendwa kama utaweza jiepushe na yafuatayo ili uweze kuepuka kero za madeni

1: Epuka kukopa pesa ili ununue WANTS (yani kitu ambacho unaweza kuishi hata bila kuwa nacho kwa wakati huo)

2: Epuka kuchangia michango yoyote kwa pesa ya kukopa. Kuwa muwazi, maana imeandikwa "ikiwepo nia, mtu hukubaliwa kwa kile alichonacho na siyo asichokuwa nacho".

Kamwe usitafute umaarufu na heshima na sifa ambazo haziendani na hali uliyonayo sasa.

Usikope pesa kuchangia harusi, send off, wala michango mingine.

Kuwa mkweli tu kwamba, kwa sasa bajeti yangu hairuhusu, mwambie kwamba utachangia kwa wakati mwingine.

Wema haulazimishwi, wala baraka hazipambaniwi kwa kufanya mambo yaliyo nje ya uwezo wako.

Epuka kufanya kitu ambacho una uhakika kipo kinyume na nafsi yako, kuwa mkweli usipingane na hali yako.

Ushauri.
Usiishi maisha ya maigizo eti kisa unaogopa kuchukiwa.

Ombi la mchango siyo sheria ambayo ukiivunja unafungwa jela.

Toa sehemu ya kile ulichonacho, usilazimishe kutenda mema ambayo wakati wake haujaufikia.

Pengine uelewa wangu ndio unaniambia hivyo, lakini natamani kila mtu aishi ndani ya uwezo wake na siyo kinyume na hali yake.

3: Usitumie zaidi ya unachoingiza. Hii itakufanya ulazimike kuishi kwa madeni.

4: Usiishi bila kuweka akiba kwa ajiri ya dharura, maana tatizo likitokea itakulazimu kuingia kwenye madeni.

5: Usiishi bila kuwekeza pesa yako: kwa sababu ipo siku nguvu zako za kutafuta pesa zitaisha, hapo utalazimika kuishi kwa madeni.

Ukiyazingatia hayo, utaepuka karaha za kuishi kwenye dimbwi zito la madeni mabaya.

Mimi kwa leo naishia hapo, nakukumbusha kulipa madeni uliyonayo, usijisahaulishe ukaja kukosana na hao wanaokudai yamkini kuna siku utawahitaji tena.

Tokomeza madeni yote.........

20250121_143155.jpg
 
Mimi nafuata sana hayo na ninajitahid kuzuia maden lakin nimeshindwa kweny utelezi aise mimi nikipata dem wa kumla utelez alafu sina hela mimi ntakopa kwa gharama yoyote ile iwe jua au mvua ntakopa tu
 
  • Kicheko
Reactions: M45
Salaam wakuu.

Wahenga walisema Tahadhali ni bora kabla ya hatari, na umakini unalipa kuliko uzembe, na akili ni njema kuliko ujinga, na utoshelevu ni bora kuliko kupungukiwa.

Mpendwa kama utaweza jiepushe na yafuatayo ili uweze kuepuka kero za madeni

1: Epuka kukopa pesa ili ununue WANTS (yani kitu ambacho unaweza kuishi hata bila kuwa nacho kwa wakati huo)

2: Epuka kuchangia michango yoyote kwa pesa ya kukopa. Kuwa muwazi, maana imeandikwa "ikiwepo nia, mtu hukubaliwa kwa kile alichonacho na siyo asichokuwa nacho".

Kamwe usitafute umaarufu na heshima na sifa ambazo haziendani na hali uliyonayo sasa.

Usikope pesa kuchangia harusi, send off, wala michango mingine.

Kuwa mkweli tu kwamba, kwa sasa bajeti yangu hairuhusu, mwambie kwamba utachangia kwa wakati mwingine.

Wema haulazimishwi, wala baraka hazipambaniwi kwa kufanya mambo yaliyo nje ya uwezo wako.

Epuka kufanya kitu ambacho una uhakika kipo kinyume na nafsi yako, kuwa mkweli usipingane na hali yako.

Ushauri.
Usiishi maisha ya maigizo eti kisa unaogopa kuchukiwa.

Ombi la mchango siyo sheria ambayo ukiivunja unafungwa jela.

Toa sehemu ya kile ulichonacho, usilazimishe kutenda mema ambayo wakati wake haujaufikia.

Pengine uelewa wangu ndio unaniambia hivyo, lakini natamani kila mtu aishi ndani ya uwezo wake na siyo kinyume na hali yake.

3: Usitumie zaidi ya unachoingiza. Hii itakufanya ulazimike kuishi kwa madeni.

4: Usiishi bila kuweka akiba kwa ajiri ya dharura, maana tatizo likitokea itakulazimu kuingia kwenye madeni.

5: Usiishi bila kuwekeza pesa yako: kwa sababu ipo siku nguvu zako za kutafuta pesa zitaisha, hapo utalazimika kuishi kwa madeni.

Ukiyazingatia hayo, utaepuka karaha za kuishi kwenye dimbwi zito la madeni mabaya.

Mimi kwa leo naishia hapo, nakukumbusha kulipa madeni uliyonayo, usijisahaulishe ukaja kukosana na hao wanaokudai yamkini kuna siku utawahitaji tena.

Tokomeza madeni yote.........

View attachment 3215480

loud and clear. umesomeka mkuu! 5/5
 
Back
Top Bottom