Usihangaike na Mwanamke asiyeonesha juhudi kuwa Nawe

Usihangaike na Mwanamke asiyeonesha juhudi kuwa Nawe

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Hii inawakuta wanaume wengi.

Hata mimi ilishawahi nipata kabla.

Lakini ni muhimu kutambua thamani yako. Na unastahili upendo na furaha.

Ubaya wa kumng'ang'ania asiye kutaka ni kukosa kuwa anayekutaka.

Mana muda mwingi utautumia kwake badala ya kuwa na anayekukubali.
.
Kuna muda unataka kuachana naye lakini inakua ngumu.

Kinachosababisha inaweza kuwa, una upweke moyoni na unatamani upate upendo.

Au umezoea kuwa na maisha ya kung'ang'aniza wanawake.

Hivyo, ni muhimu ukakaa chini ukajiuliza kwanini unang'ang'ania usipopendwa?

Kwanini huwezi kujitoa kwa huyo mwanamke?

Je, ulikua na uhusiano mzuri na mama yako? Au ndo unatafuta mama ukubwani?

Je, aina hiyo ya mahusiano ndio unayotaka?

Kisha anza kujiheshimu.

Heshimu muda wako. Usiupoteze kwa mwanamke asiye na juhudi juu yako bali kuza thamani yako na utapata urahisi kumvutia mwanamke. Itakufanya uweze kuwa na uchaguzi na sio kumg'ang'ania mwanamke mmoja kama vile mama ako.
.
Unapomng'ang'ania mwanamke mmoja anakuona huna thamani.

Anakushusha heshima.

Maana yake ni kwamba hata wanawake wengine hawakutaki.

Kiasi kwamba unaona umepata bahati kuwa naye.

Na kama tunavyojua, wanawake ni watu wa kijamii. Akiona wenzie hawakutaki na yeye hatoona sababu ya kukutaka.

Ndiyo mana unakuta ukiwa na mwanamke wanawake wengine pia wanakutaka. Ila ukiwa bachela wanawake wanakukwepa kama ukoma.
 
Umeandika ujumbe mrefu, mwanamke anapenda mwanaume mwenye self respect, sefl respect kuondoka unapoona hueshimiki, huthaminiki, unachukuliwa powa.
Hiyo self respect mwingine ukienda kumtongoza anasema alikuwa anakuheshimu .Kwahiyo mtu akitongozwa self respect huondoka au?
 
Hiyo self respect mwingine ukienda kumtongoza anasema alikuwa anakuheshimu .Kwahiyo mtu akitongozwa self respect huondoka au?

Akili za wanawake huzifahamu. Mwanamke anakujaribu once, ukiona anakujaribu constant ujue ana list anafanya comparison.

The best man ni yule ambae atakataa kufanywa comparison, eith akukubali or not. Maintain frame yako

Uking’ang’ania dharau zinaanza hapo
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana na hua hayanaga muongozo...
 
Back
Top Bottom