Usiingie kwenye biashara kwa mihemuko ya semina na mifano ya akina Jack Ma, Bii Gate na Jeff Bros

Usiingie kwenye biashara kwa mihemuko ya semina na mifano ya akina Jack Ma, Bii Gate na Jeff Bros

Ndio maana nikauliza, hakuna kitu kinachoweza kuniguide hata kama nimebadili biashara?
Mtu pekee wa kukuguide ni wewe mwenyewe!!!

Unatakiwa wewe mwenyewe uchunguze au ukatathmini eneo unalotaka kufanya biashara yako kulingana na eneo husika....!!!!

Alafu unaanza biashara na mambo mengine utajifunza kadri biashara inavyokwenda!!!!
 
Ninahamasika sana na Robert Kiyosaki na wengineo ambao kiukweli wananielimisha sana ktk biashara.

Sina la kusema kuhusu wahamasishaji wa Tanzania
 
Mtu pekee wa kukuguide ni wewe mwenyewe!!!

Unatakiwa wewe mwenyewe uchunguze au ukatathmini eneo unalotaka kufanya biashara yako kulingana na eneo husika....!!!!

Alafu unaanza biashara na mambo mengine utajifunza kadri biashara inavyokwenda!!!!
Sawa sawa kabisa mkuu
 
Kwani wanaitwa Business guider au Motivational speaker maana unachanganya watu sasa.

Kimsingi wanaitwa motivational speaker zumuni ni kuwa-motivate walio kwenye kiza kupata mwanga sasa sioni tatizo lipo wapi kama watu wanakuwa motivated tatizo lako wewe mtoa mada na wanajf wengi ni kwamba wamewazoea so ndio maana wanawaona wakawaida ila nikikuchukulia mtu ambaye amjui Anthony Luvanda na hana maJF akimsikia mara ya Kwanza atabadilika hemu tutumieni akili kidogo basi.

NB: usiakalili maneno ya mtaani motivacional speaker wengi wana-practice biashara wakina Luvanda, Shigongo nk
 
Binafsi naamini motivatinal speakers ni muhimu kuwatoa watu gizani nakuwaamsha huwa hawakufundishi kitu kipya unafundishwa vitu vile vile we unaamua uchukue kipi na kip ukiache ,hawawezi kufundisha kila kkitu kama ilivyo elimu hatufundishwi kila kitu darasani mengine utajifunza mtaani,hata jeshini hawafundishwi kila kitu mengine utajiongeza mwenyewe ,,hivyo sio motivatonal speaker ni reality angalia hata mifano wanayoitumia msingi ni ya marekani sio tz mfano nimesoma kitabu cha JOEL NANAUKA MIFANO MINGI SIO YA NCHI HII CHA MSINGI AKILI YA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO ,SIKILIZA BEBA KINACHOFAA HUDHURIA SEMINA KUJIFUNZA HAKUNA MWISHO
 
Habari za wapambanaji wenzangu katika jukwaa hili.
Leo napenda tujadili kidogo juu ya hawa watu wanao jiita wahamasishaji wa biashara na ujasiriamali au kujiajiri. Binafsi nimekuwa nawafuatilia sana kuona kama naweza kupata chochote chenye kuweza inisaidia katika ujasiriamali au biashara lakini kinyume na matarajio ni kwamba sioni jambo lamaana sana, labda kwakua wengi huongelea ambayo nimeyapitia kwa muda mrefu. Hawa watu wamekua na nadhalia nyingi kuliko uhalisia na zaidi wamekua ni watu wa kusimulia mapito ya Matajiri wakubwa wa dunia kama moja ya nyenzo za kufanya uhamasishaji wao. Pia wachache wanajaribu kujielezea mapito yao binafsi mpaka kufikia walipo leo ingawa hata wao wengi hawaonekani kuwa walio fanikiwa au labda kwakua walipo ndipo walipo tamani kuwa ili kujihesabu walio fanikiwa.

Mada zao kuu zimekua kama zifuatazo. 1. Kujitambua wewe umekuja duniani kufanya nini 2.Kuchukua hatua 3. Kuwa tofauti 4. kuwa mbunifu na maengine machache.
Pia wapo wengine hujifanya kuelimisha na mwisho wa siku hutangaza biashara zao za bidhaa na kuwataka nyie wasikilizaji mjiunge nao muwae wauzaji wao, yaani anatoka kukuhamasisha ujiajiri kisha hapohapo anataka umtumikie. Wengine wanakuuzia kitabu ambacho kimendikwa hayohayo aliyo kuelezea.
Sikumoja nilihudhulia semina moja na baada ya hapo nilimuuliza jinsi ya kukuza biashara katika hali ya ushindani na wapinzani wangu. Kiukweli jibu halikutoka na nikaamua kukausha tu nisije kuharibu dili la mtu maana huo nao ni ujasiriamali.

Kwa uchunguzi wangu, Unatakiwa kuhudhulia semina moja tu, inatosha kama wewe unahisi labda umepungukiwa morari ya kazi tu. Hizi semina huwa ni zakuongeza au kukupa morari tu na wala sio kukufundisha biashara. Biashara zina sura tofauti kwa kila mmoja ingawa kuna mambo yanapatiwa suluhisho kwa njia zinazo shabihina kwa ukaribu. Yapo mengi katika biashara zaidi ya morari na pia zipo changamoto kubwa sana ambazo ukikumbana nazo hata uwe umehudhulia semina laki moja lazima morari ipoe.
Kuna ulazima wa watu kuingia field na kuja na mbinu mpya ya kufundisha Biashara na chngamoto zake kuliko kuishia kupeana morari tu.

Wahamasishaji wengi sio wafanya biashara ambao wanaweza kumshauri mtu kuligana na uhalisia wa mambo bali wengi ni wasaka fursa kwa kutumia mioyo na akili za watu waoga. Sasa tumehamasishwa vya kutosha na leo tuko ulingoni ila tunayo kumbana nayo huku hakuna sehem ya kujifunza namna ya kutatua changamoto halisi.

Semina za hamasa zikome sasa njooni mtufundishe biashara maana tayari tumeingia ulingoni na kuna mambo hamkuyasema, labda mlisubiri tuingie huku na tuyaone ili somo lieleweke vema.

Ushauri wangu, Usiingie biashara kwa mihemuko ya semina na mifano ya akina Jack Ma, Bii Gate na Jeff Bros. Jitahidi kujifunza kwa wafanya biashara wenzako walio kutangulia katika ulingo.

Karibuni tujadili.
akili za kuambiwa changanya na zako
 
Biashara ni kitu cha ajabu sana!!!....

Mabadiliko na mafunzo unayapata kadri uanvyoifanya!!!!

Unaweza ukaanza na biashara hii ukajikuta baadae unabobea kwenye biashara nyingine ambayo hata hukuwaza kuifikiria
Kabisa yaan!
 
Back
Top Bottom