Salam,
Huu mnanda marehemu Lupozi bwana katuachia moja kati ya sanaa/ngoma isiyochuja sababu inazungumzia hali halisi ya miaka yote katika nchi hii kutoka kwa watu wenye vipato duni.
"Maharage yapo juu kama NYAMA, 🪘 SUKARI nayo imepanda, KODI za NYUMBA kila kukicha, umeme LUKU wa kuchangisha, AJIRA nyingi mjini zimetokaa, wanaokota MAKOPO kaka 🎹, unaweza ukaja kuwa CHOKORAA, wakatucheka USIJE KAKA!!!" 🎹 🎹
Moja ya mstari wa wimbo unaoishi MIAKA NA MIAKA.
Wasikilizaji wa hii sanaa nadhani mnaelewa. mnaweza kukumbushia walioshiriki kutengeneza huu umeme.
#KwaMaraNyingineTenaNatoaUgumuKwaWaleWasioelewa