Usije ukapoteza muda na rasilimali zako kutaka kumbadilisha mtu ili awe kama wewe

Usije ukapoteza muda na rasilimali zako kutaka kumbadilisha mtu ili awe kama wewe

Joined
Dec 11, 2024
Posts
94
Reaction score
240
Kuelekea 2025 .

Kauli mbiu ni "Protect your Energy" (Linda nguvu yako).

Katika maisha kuna mambo mengi Sana ambayo huleta destruction , disappointment and heart fainted.

Katika mahusiano
Usihangaike kumbadilisha mwanamke / mwanaume ili aendane na wewe utaumia Sana Ila wewe unaweza kubadilika kuendana na yeye . hapa unachofanya unaangalia Kama unaweza kuufatisha mfumo wake wa maisha ukiona yes unaweza kukaa nae na ukiona NO huyo muache fahamu tu Kuwa hayupo Kwa ajili yako.
So "protect your energy"

ukimkuta mwanamke au mwanaume anapenda mambo Fulani usipoteze muda kumbadilisha muache aaendelee na kile anachoamini na kupenda kufanya .


Wanaume wengi wanapoteza Sana nguvu na rasilimali Kutaka kuwabadilisha WANAWAKE ambao ni uncivilized and they are comfortable na hali zao za MAISHA. Don't do it


Tukija katika ndugu , marafiki n.k

Wewe hauna uwezo wa kuwafanya ndugu zako wafanikiwe na wawe financial stable

Ila ulichonacho ni uwezo wa kuwasaidia na kuwaonesha njia tu ,either waifate au waipuuze .

So unapoingia mwaka 2025 just keep this in your mind kwamba unaweza kumsapoti mtu kimaisha Ila hali yake ya maisha hauna uwezo wa kuibadilisha mpaka muhusika apende kuwa responsible


2025 protect your energy.
 
FB_IMG_17352182522296268.jpg
 
Muhimu hapa ni ku stop being mama/baba huruma
Huruma Kama binadamu ni muhimu Sana kuwa nayo.

Hapa nimezungumzia kulinda energy na sio kuitapanya .

Kusaidia mtu au kumsapoti ni jambo linaloleta baraka na kukufungilia njia zaidi Ila kutaka kulazimisha kumbadilisha mtu awe Kama wewe hiyo ndo haifai.
 
Huruma Kama binadamu ni muhimu Sana kuwa nayo.

Hapa nimezungumzia kulinda energy na sio kuitapanya .

Kusaidia mtu au kumsapoti ni jambo linaloleta baraka na kukufungilia njia zaidi Ila kutaka kulazimisha kumbadilisha mtu awe Kama wewe hiyo ndo haifai.
Ni kweli ila huruma zikizidi ndio tunarudi kwenye uzi
 
Hatuambiliki tunalazimisha tuwabadilishe 😀😀😀.

Huwezi amini nikiwa nacheza na mtoto akilia utasikia anasema "Tayari mmeishapigana".

Leo katoka kwenda kazini, Mimi nipo mapumzikoni anasema nipike yeye atachelewa kurudi..😀😀😀😀
Badilika wewe sawa...


Cc: Mahondaw
 
Nilikuwa katika mahusiano na mwanaume ambae yeye hamna anachofanya kinaeleweka. Kila kazi anafukuzwa akianzisha biashara inakufa, ikafika mahali nakopa kazini nampa yeye afanye biashara niliishia almost losing my
Houses kwa mikopo nayompa yeye ila hajawahi badilika ila nilijifunza somo gumu sana. Kuna maisha nje ya mapenzi! Kamwe kamwe usimpe nafasi mtu ambae hana maono kwa maisha yako, anaweza akaua hadi ndoto zako! Protect ur energy for real
 
"Wewe hauna uwezo wa kuwafanya ndugu zako wafanikiwe na wawe financial stable"
 
Your energy is better spent on things you can change like Your health, Finances and Habits.

Don't give people more than you take from them.
 
Nachoamini mwanamke ni msaidizi wa mwanaume , mwanaume Una maono yako na unajipa muda yatimie, ukikutana na hawa wanawake ambao hataki kuishi maono yako , yeye anapanga mambo yake na anahisi analipambania hakikisha unaachana nae mapema , mwanamke Anatakiwa aboreshe wazo lako kwa ushauri na sio yeye ajipangie yake hapo utakua umekutana na malaya mwenye tamaa hatokuja kua msaada kwako
 
Back
Top Bottom