Usije Ulaya

Usije Ulaya

Tape measure

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2015
Posts
1,981
Reaction score
3,604
Ni miezi mingi sana imepita sijaonekana kwenye huu mtandao wetu wa kijamii. Sijaona tena nyuzi nyingi za kusisimua kutoka kwa Mshana Jr habibu Pascal Mayalla ONTARIO... Nimekumbuka Uzi wa jinsi nilivotengeneza million 9 ndani ya mwezi mmoja.

Nimeanzia mbali sana kwani namkumbuka mwana FA na wimbo wake USIJE MJINI Leo hii nawaasa GenZ.. USIJE ULAYA. Kuna usemi usemaon huwezi kumtambua nyoka anapokuwa mjamzito, naamini sio rahisi sana kumtambua mkikutana porini.

Uzuri na utamu wa pesa wanaujua wenye pesa. Tajiri anaelewa kwa nini ni sahihi yeye kutumia milioni 2 mpaka 10 kwa siku moja tena kwa matumizi ya kula na kunywa tu.

Unaposikia fulan sijui Fernandez wa NALA alikataa mshahara wa zaidi ya 30 million kwa mwezi akaamua kurudi nyumbani masikini hawezi kuelewa hata umkate kichwa ...nmewahi kukaa mahali na mama mmoja aliacha kazi EAC ili awe free akaajiriwa sehemu analipwa haifiki hata robo na yuko na amani na furaha tele.

Kwa nini USIJE ULAYA, Asia, America.... Jibu rahisi Utajiri uko AFRICA 🌍 🌍 🌍. Rasilimali za Bure ziko Africa. Fursa za kutupa zipo Africa.

Kila leo walioko nje ya Africa wanaumiza kichwa kuweza kufanikisha kuwekeza Africa. Unaweza kuamua kwenda Ulaya likizo unarudi Africa kutembea. Wazungu wametuweza sana kutupymbaza waafrica tumekuwa watumwa wa fikra kwamba Ulaya Kuna maisha yaani Bora kuwa paka Russia kuliko kuzaliwa Africa 🌍.

Sio kweli narudia sio sahihi wametupumbaza na watazidi kutupumbaza. RIP JIWE/BULLDOZER/MWAMBA/CHUMA 17 March 2021. Nyota ilizima Gafla Giza likatawala. Hiki CHUMA sizani kama spea yake itakaa ipatikane tena !!!

Ukiwa na uwezo wa kupata 15k kwa siku Tanzania ni sawa na mtu anayepata 170k Marekani. Ngoja nikuchanganye kidogo uelewe. Barrack Obama akiwa Raisi alimwalika dinner Raisi wa India na ilitumika karibia 200$k ni kama 500m kwa chakula tu. Emmanuel Macron alipomwalika King Charles ilitumika karibia 560$K hizi ni zaidi ya 2 Billion za kitanzania.

Mama alipowaalika kufuturu ikulu mlitumia kiasi gani??
Tuendelee kwa nini Usiende Ulaya....Mwisho nitaeleza kwa nini kabla hujazeeka hakikisha angalau unatembelea nchi yeyote kati ya German, Spain, Italy, France, Poland, Russia, Norway, India, Japan, Iran, Saudi Arabia, China, Cuba, USA, Canada, Turkey Argentina, Cambodia na Australia.

Changamoto ya nchi nyingi hawajui kingereza, hii ni mada ingine ndefu sana niiruke ila kwa ufupi ukitembelea nchi isiyozungumza kingereza tembelea zaidi mji mkuu wa nchi utapata huduma nzuri.

Nichomekee tabia ya vijana wasomi wanaojiita chawa ni bomu kwa mustakabali wa nchi yetu ni kama kansa itatumaliza taratibu.

Tuendelee, Ni kweli kabisa maisha ya Ulaya au nchi nilizotaja hayafanani na ya Tanzania Kabisa, ni mazuri, uhakika, yanavutia, Usalama lakini nirudi nyuma kwa kuwa Tanzania haifanani na Ulaya hata kidogo kuifananisha ama kuilinganisha kijeshi, technology au vyovyote ni kutenda kosa la kukusudia....

Africa ina maisha ya aina yake ...Kuna siku nilisikia mchungaji mgogo anasimulia Kuna dhambi ni za Africa tu. Mtoto akiwa na njaa Akala chakula kwenye friji bila kupewa anaitwa mwizi/Mdokozi .,, hizo ni dhambi za Africa ambapo mtoto hawezi kutoa kinywaji kwa friji akanywa na kula bila mzazi kumpatia.

Kwa nini Usiende Ulaya!!
 
Ni miezi mingi sana imepita sijaonekana kwenye huu mtandao wetu wa kijamii. Sijaona tena nyuzi nyingi za kusisimua kutoka kwa Mshana Jr habibu Pascal Mayalla ONTARIO... Nimekumbuka Uzi wa jinsi nilivotengeneza million 9 ndani ya mwezi mmoja.

Nimeanzia mbali sana kwani namkumbuka mwana FA na wimbo wake USIJE MJINI Leo hii nawaasa GenZ.. USIJE ULAYA. Kuna usemi usemaon huwezi kumtambua nyoka anapokuwa mjamzito, naamini sio rahisi sana kumtambua mkikutana porini.

Uzuri na utamu wa pesa wanaujua wenye pesa. Tajiri anaelewa kwa nini ni sahihi yeye kutumia milioni 2 mpaka 10 kwa siku moja tena kwa matumizi ya kula na kunywa tu.
Unaposikia fulan sijui Fernandez wa NALA alikataa mshahara wa zaidi ya 30 million kwa mwezi akaamua kurudi nyumbani masikini hawezi kuelewa hata umkate kichwa ...nmewahi kukaa mahali na mama mmoja aliacha kazi EAC ili awe free akaajiriwa sehemu analipwa haifiki hata robo na yuko na amani na furaha tele.

Kwa nini USIJE ULAYA, Asia, America.... Jibu rahisi Utajiri uko AFRICA 🌍 🌍 🌍. Rasilimali za Bure ziko Africa. Fursa za kutupa zipo Africa.

Kila leo walioko nje ya Africa wanaumiza kichwa kuweza kufanikisha kuwekeza Africa. Unaweza kuamua kwenda Ulaya likizo unarudi Africa kutembea. Wazungu wametuweza sana kutupymbaza waafrica tumekuwa watumwa wa fikra kwamba Ulaya Kuna maisha yaani Bora kuwa paka Russia kuliko kuzaliwa Africa 🌍.

Sio kweli narudia sio sahihi wametupumbaza na watazidi kutupumbaza. RIP JIWE/BULLDOZER/MWAMBA/CHUMA 17 March 2021. Nyota ilizima Gafla Giza likatawala. Hiki CHUMA sizani kama spea yake itakaa ipatikane tena !!!

Ukiwa na uwezo wa kupata 15k kwa siku Tanzania ni sawa na mtu anayepata 170k Marekani. Ngoja nikuchanganye kidogo uelewe. Barrack Obama akiwa Raisi alimwalika dinner Raisi wa India na ilitumika karibia 200$k ni kama 500m kwa chakula tu. Emmanuel Macron alipomwalika King Charles ilitumika karibia 560$K hizi ni zaidi ya 2 Billion za kitanzania.

Mama alipowaalika kufuturu ikulu mlitumia kiasi gani??
Tuendelee kwa nini Usiende Ulaya....Mwisho nitaeleza kwa nini kabla hujazeeka hakikisha angalau unatembelea nchi yeyote kati ya German, Spain, Italy, France, Poland, Russia, Norway, India, Japan, Iran, Saudi Arabia, China, Cuba, USA, Canada, Turkey Argentina, Cambodia na Australia.

Changamoto ya nchi nyingi hawajui kingereza, hii ni mada ingine ndefu sana niiruke ila kwa ufupi ukitembelea nchi isiyozungumza kingereza tembelea zaidi mji mkuu wa nchi utapata huduma nzuri.

Nichomekee tabia ya vijana wasomi wanaojiita chawa ni bomu kwa mustakabali wa nchi yetu ni kama kansa itatumaliza taratibu.

Tuendelee, Ni kweli kabisa maisha ya Ulaya au nchi nilizotaja hayafanani na ya Tanzania Kabisa, ni mazuri, uhakika, yanavutia, Usalama lakini nirudi nyuma kwa kuwa Tanzania haifanani na Ulaya hata kidogo kuifananisha ama kuilinganisha kijeshi, technology au vyovyote ni kutenda kosa la kukusudia....

Africa ina maisha ya aina yake ...Kuna siku nilisikia mchungaji mgogo anasimulia Kuna dhambi ni za Africa tu..... Mtoto akiwa na njaa Akala chakula kwenye friji bila kupewa anaitwa mwizi/Mdokozi .,, hizo ni dhambi za Africa ambapo mtoto hawezi kutoa kinywaji kwa friji akanywa na kula bila mzazi kumpatia.......

Kwa nini Usiende Ulaya!!
Mkienda huko hamtaki kabisa wengine tupajue huko ulaya kila mtu afike huko ajionee yeye mwenyewe wacha kukatisha tamaa. Wanaijeria africa magharibi imejaa ulaya, wakenya wapo wa kutosha
Wanapeana konnekshen sisi wa bongo tuna roho mbaya sana ukiona wewe upo ulaya utaki wengine waje
 
min -me unaitwa huku😂
 
Ahahaha kitambo nilishasema humu
images (9).jpeg
 
Mara usije ulaya, mara usiende ulaya. Yani mtu mmoja una kauli mbili tofauti ambayo moja inaonesha kuwa upo ulaya unataka mtu asije ulaya. Na nyingine inaonesha upo Bongo unataka mtu asiende ulaya.

Anyway kwa muandiko wako inaonesha fika kuwa wewe upo zako bonyokwa Tanzania, ila unajaribu ku act kuwa upo ulaya ili uonekane kuwa na wewe ni miongoni mwa waliopanda ndege kwenda kuishi ukubwani.

Wasalimie washkaji hapo bonyokwa.
 
Nitaendelea mchana Wacha niende kujenga nchi za wengine. Ukisikia mtu anatumia kwa siku 100-200$ ambayo ni kama 500k Tz utaona ni nyingi but kwa Marekani ni pesa ya kawaida.
Mfano Japan yen 1 ni Tz 16 na kawaida chakula unaweza kupata kwa 1300yen ni 20k Tz. Mwanafunzi anaweza kuwa anapewa boom la 3m ambapo kitanzania ni pesa nyingi lakini yeye kwa siku anatumia wastani wa 60k zingine anunue maji, alipie bundle na mambo yake mengine. Asipojibana 3m haimtoshi kwa mwezi......
Ndio maana watu walikimbilia kulipwa 4m Israel wengine 6m Saudi Arabia but kiuhalisia ni kama 500-700K kwa Tanzania.
Canada ukiwa na iyo I billion ya Tanzania wewe ni wa kawaida tu huwezi kufungua ata supermarket ni kaela kadogo kukuwezesha kuishi huku unatafuta kazi ya kufanya lakini bongo utaweza kuwa mwekezaji?..

Inaendelea..... Kwanza niombe radhi kwa wale ambao hawakunielewa namna nilivyoanzisha uzi sio jambo la ajabu kwani hata mimi sijazoea aina hii ya uandishi ni namna mpya naendelea kujifunza njia bora na rahisi ya kuweza kufikisha ujumbe kwa ufupi. Lakini changamoto na faida ya namna yangu ni kuweza kufikisha jumbe nyingi pengine nusunusu ama pungufu ya nusu kwa wasomaji kwa wakati mmoja.

Tumeona Japan ndani ya kipindi cha miaka minne imeweza kuwa na mawaziri wakuu 4 ni kuonyesha siasa za kuogopesha sio jambo la kawaida lakini pia inaweka mizani sawa kuonyesha uwajibikaji pengine sio sawa na kwa historia Japan Mawaziri wake wakuu wengi tu wamehudumu kwa muda mfupi na wengine kukaa madarakani kwa siku moja tu Huyu Kishi Nobusuke alihujumu usiku mmoja kuanzia Julai 23, 1954 kuamkia Julai 24, 1954 (Siku 1). Kuna mawaziri wakuu wengi tu ambao walikaa madarakani kwa siku moja wengine 2 na wengine miezi 2 na chini ya mwaka mmoja.

Jambo moja la kukumbuka ni kuwa waziri mkuu wa sasa wa japan Fumio Kishida ambaye anatarajiwa kujiuzulu rasmi mwaka huu aliingia madarakani 2021 akiwa anakubalika kwa asilimia 55% na sasa ni 15% kwa lugha nyingine umaarufu wake umeshuka kupita maelezo na kushinda waziri mkuu yeyote aliewahi kuwa madarakani kwa muda kama wa kwake.

Sasa basi tukiwa tunazitazama mwingiliano na mgongano wa maisha barani Asia ni vizuri ukaweza kujua kwa nini wawekezaji wanaikimbia China na kuhamia India ambayo kwa sasa inategemewa kuwa mbadala wa China. Ingawaje kijeshi China anaumia pesa nyingi kiasi kwamba bajeti yake inazidi ya UK, France na Germany Ukizijumlisha kwa pamoja. Ni kweli inaidadi kubwa ya watu takribani 1.43billion ikizidiwa kidogo na India 1.47 bilion lakini bajeti ya India kwa ulinzi haifikii hata robo ya bajeti ya China 480Billion vs 84.B.

Nimalizie kwa haraka sana, maisha ya ulaya hapa kwanza ni tofauti sana na ya Afrika yanakuhitaji sio tu kujua lugha kama kijeruman au English lakini uwe mwelewa wa kutumia teknolojia kuanzia simu, google maps na mambo kama hayo. Pili atu wanajivunia kulipa kodi ni utamaduni wa watu wa ulaya, demokrasia tunayoihubiri na kusema ipi nchi za magharibi hiyo demokrasia haipo uongozi sio jambo ambalo kila mtu anaweza kupata ni mnyororo.

Akili za kumiliki nyumba sijui kununua kiwanja uaanze ujenzi hizo mentality ulaya hazipo watu nyumba zinajengwa na makampuni wewe unawapa tu lay out ya ndani unataka wamodify wapi kisha nyumba zote zitakazojengwa kwa nje na ukubwa katika eneo fulani zote lazima ziwe na ufanano wa aina fulani au asilimia 100. Kumiliki nyumba ulaya sio jambo dogo nyumba ni za matajiri bila kujalisha aina ya nyumba nikisema nyumba namaanisha kuanzia ya vyumba 3 huwezi kumiliki kirahisi kama tunavyomiliki kwetu bongoland.

Definition ya maisha kwa ulaya ni tofauti na Tanzania huku mafanikio sio kuwa na kiwanja ama kununua nyumba ama kununua gari. Mafanikio ni kitu kingine kabisa na ni namna mtu anavyofikiria yaani watu wengi kuwa na nyumba sio jambo la kipao mbele kwao hata kidogo. Watu wanafikiria kuishi na kuhama miji tofauti tofauti kulingana na uhitaji wala hawafikirii kumiliki nyumba eneo fulani.

Labda niendelee kidogo nitoe sababi fikiria nchi ya China, India, Russia ilivyo kubwa fikiria upo pale China katika mji wa Sanya (Hainan Province) unaelekea Mohe (Heilongjiang Province) ambapo ni kasikazini mwa China sasa kwa mto anaekaa eneo hilo hawezi kufikiria kujenga nyumba kwani ikitokea akahamishiwa eneo jingine ndani ya nchi ni mbali sana. Ni karibia kilometer 3500 ambapo ni sawa na umbali wa kusafiri kwa ndege kutoka Tanzania mpaka Cairo Misri, hio ni miongoni mwa sababu.

Pia watu wengi wanakuwa na ndoto za kununua nyumba nje ya nchi na sio ndani ya Marekani kama mtu yupo Russia basi lengo lake ni kununua nyumba Spain na kisha kuhamishia huko makazi yake kabisa.Ukiwa Japan utawaonea wazee huruma sana kwani unakuta familia ilikuwa na mtoto mmoja na sasa huyo mtoto amekuwa mkubwa anaishi UK na familia yake amewaachaa wazazi wake Tokyo wamestaafu wana miaka 80 au 90+ hawana mtu wa kukaa nao wala mtaani hawawezi kupata mtu wa kupiga nao stori. Unaweza kukuta kazee kamekaa beach ama public rest places kamepaki gari yake kali apo ana mafao lakini hana watu wa kuweza kuzungumza nao anaishi maisha ya upweke.

Ikimbukwe mzee huyo kipindi akiwa kijana alikuwa anafanya kazi kwa bidii sana han muda wa kupumzika likizo anaenda njee ya nchi hawana urafiki wala tabia ya ujirani sana kujuliana hali huku unaweza ukafia ndani na kukaa majuma kadhaa bia mtu kuwa na taarifa kwa sababu hata kama nyumba mnaishi watu 10 kila mtu na maisha yake sio rahisi uende chumba cha mwenzio kumsabahi labda muwe marafiki sana na iwe ni kwa ishuu maalum sio tu kumtembelea. Ni kawaida kutokujua hali ya jirani yako kama yupo ndani ama hayupo na hata ukijua yupo au hayupo haikuhusu.

Afrika tuna tabia ya kulea mtoto na kutengeneza uhusiano mzuri kati ya mtoto na mzazi huku mtoto anajitegemea hatambui umuhimu wa mzazi katika maisha yake mtoto anaweza kuwa anawakumbuka na kuwapenda marafiki zake anaochezaga nao boarding school kuliko mzazi wake .... kwenda kumtembelea mtoto wako mpaka umpe taarifa kwa muda mrefu na akuambie kama atakuwa na nafasi ya kuweza kuonana na wewe kwa dakika chache mnywe angalau kikombe cha kahawa kisha urudi zako ulikotoka ama akupe chumba ulale kisha jioni mtoke wote dina baada ya hapo utakula nini saa ngapi wapi utaendelea kujiongeza kadiri ya mahitaji yako sio jukumu lake kutambua hayo yotee.

Maendeleo yana faida zake na hasara ndio maana tunasema tamaduni za ulaya zibaki ulaya waheshimu za kwetu. Watu wengi wanapenda kufuga Mbwa na paka unakuta mtu hajaoa lakini rafiki yake mkubwa ni paka ambae anatumia ata nusu ya mshahara wake kwa mwezi kwa miaka kadhaa huyo paka ana thamani kuliko wewe immigrants/mzamiaji ndio kila kitu chake anamtoa matembezi jioni ....Hizo ni tamaduni zao....Kwa wale wasiojua kumiliki paka ama mbwa ama mnyama mwingine ni mpaka uwe na uwezo fulani huwezi kupata kibali cha kufuga mbwa kama unaishi kwa chumba kimoja na kipato chako hakieleweki kuweza kumuhudumia ipasavyo ikiwemo kumtembeza na kumpatia haki za huduma za afya na kuonana na mtaalamu wa wanyama kwa kila baada ya muda fulani au uhitaji unapotokea.

Kwa kupata vijisenti kisha urudi nyumbani ni sawa unaweza kufikiria kukaa ulaya lakini jua sio kuwa tu ulaya eti mwafrika ama ngozi nyeusi ndio anabaguliwa hapana hata mrusi ana mbagua mchina na kumuheshimu mmarekani hivyo hivyo watu kutoka Philiphness wanabaguliwa wakiwa nchi fulani wakati wa jamii fulani kama vile wajerumani unakuta wanaheshimika kuliko watu wa nchi fulani ya ulaya ama Asia.

Sitaki kuongelea ubaguzi wa nyumbani au majirani zetu apo 254 au +250 hio ni kitu ambao isikutingishe sana ukiwa na ndoto za kuzamia ulaya. Pia kupata kazi ya kuajiriwa na kupata kibarua ni vitu viwili tofauti tunaposema ulaya kazi zimejaa tuna maanisha vibarua au part time jobs sio kazi za mikataba ya kudumu. Unahitajika kuwa na vigezo vya ziada kupata kazi za kudumu pia tukumbuke kuna suala la udini hata kama hulitaki ila nchi nyingi kama wewe ni Abdul au Aisha kuna uwezekano mkubwa pia ukapata vizuizi vya wazi wazi nikushauri usikaze sana fuvu ukajitia mfia dini na mengineno.

Waliokaa China na Korea Kaskazini wanafahamu tukisema maendeleo na dini tunamaanisha nini uhuru wa kuabudu hauzidi ila upo na pia kwa China ukiwa mwanachama wa Labour party hutakiwi kwenda msikitini au sinagogi kwa buddissim. Na watu ukimuuliza kuhusu dini ata akikuambia yeye ni mkristo ukimuuuliza mstari hata mmoja wa biblia haufahamu sio kazi yake kuufahamu ni kazi ya mchungaji au Padre...Na atakuambia ana amini Mungu yupo lakini sio kihivyooo.....NOT THAT MUCH BUT WE DO BELIEVE ON HIS EXISTENCE.
 
Nimejitahidi kutaka kutaka kujua unaongelea nini kiukweli sijaelewa hata kidogo

Hebu jikite zaidi kwenye msingi wa kusudio lako ni nini ,maana umejitahidi kutaka kuelezea mifano bado pia kwa sehemu kubwa hai-relate kbs na kichwa cha habari
 
Mkuu mimi Ulaya nitakuja tu.

Bado hujaeleza kwanini tusije Ulaya, upange uzi vizuri na ujaze nyama tuelewe.

Pia usisahau kuelezea kwanini umesema kabla ya uzee mtu atembelee nchi ulizotaja?

Come back vizuri Mkuu huwenda una madini.
 
Back
Top Bottom