"Usijenge Familia kukiwa kumekuchwa" Vijana Zaeni na oeni mungali mna nguvu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Wakuu Kwema!

Leo sina mengi!
Ujumbe huu unawahusu zaidi wasomi hasa kutoka dini ya kikristo.

Vijana acheni kusubiri Embe kwenye Mnazi!
Msichelewe, ikiwa Una mwenza wako, na una miaka 27-30 amueni kuzaa ikiwa mnaona mambo Yenu bado hayajakaa Sawa.
Msisubiri embe dodo kwenye mnazi. Safari ya maisha haiwi Sawa Kwa kila mtu.
Sio Kwa sababu Fulani kafanya Harusi ndipo kazaa basi nawe ufanye Kama wao. Unaweza kuzaa halafu baadaye ukafanya Harusi kulingana na Hali itakavyotengemaa.

Kulea mtoto ukiwa na miaka 27-35 kuna utamu wake Kwa kijana wa Kiume, Kama ilivyokulea mtoto ukiwa na miaka 21-30 ilivyoraha Kwa mtoto wa kike.

Sio lazima mfanye Harusi, ongeeni na wazazi wenu wa pande mbili, kajitambulisheni, kisha zaeni hiyo inatosha,

Msisubiri mambo yakae poa ndipo muoe, Kwa mwenendo WA dunia ulivyo Hali itaendelea kuwa ngumu kadiri na kadiri siku zinavyoenda.

Vigezo vya kuoa uwe na Ghetto lako, kitanda na Godoro, jiko, sufuria nne, bakuli na sahani na vijiko. Basi! Kama utaweza weka na kasabufa kakuwafariji mkiwa nyumbani, vuta jiko endeleeni na maisha.

Msitake makuu, msitake vingi ambavyo hamjui ni lini mtavipata. Kama kuna Jambo la kulipata ukiwa na nguvu basi ni Mke na watoto ili ujenge familia yako.

Dada zangu, msisubiri muolewe na watu wenye magari na majumba, mtasubiri Sana. Maisha hayahitaji kusubiri, ukipata kijana umpendae, mwenye sifa za mwanaume, awe na Ghetto lake, na vitu vya kuanzia maisha Mwambie upo tayari kuwa mke wake na kufanya maisha pamoja.

Nimeona Jambo hili litawagharimu Vijana wengi hapo baadaye, watajifanya hawataki kuoa na kuzaa Kwa kusubiria siku mambo yakikaa Sawa. Mwishowe watajikuta wanakosa vyote na hata wakipata watoto watapata Kwa kuchelewa na watateseka mno.

Usimsikilize ya watu.
Usiangalie njia za wengine wanazopitia, kila mtu ana njia yake.
Usiwaige Wazungu na kujifanya mtu wa Kisasa wakati ulimwengu unaoishi ni Wakale.

Tafuta binti, nenda kwao kajitambulishe, kulingana na uwezo wako kama huwezi kutoa mahari sema, au lipa kidogo hata robo ya mahari, chukua mke Anza maisha na familia yako.
Usijenge familia kukiwa kumekucha.

Msiogope, msifuate mkumbo! Zaeni, ndipo mfunge Harusi ikiwa ndoto yenu ilikuwa kufanya Harusi kubwa.

Niwatie moyo Vijana wa kizazi hiki, naelewa mnapitia kipindi kigumu mno, wanaowatumaini walipaswa watumainiwe wao Kwa kuwapa Urithi mbali na kile wakiitacho Elimu.

Msiwafuatishe! Msiwasikilize! FANYENI maisha yenu mapema kungali mchana, zaeni na wanawake mnaowapenda mkaishi nao, msitake mambo makubwa.

Sio kila Jambo zuri na kubwa lazima lipitie mikononi mwako, mengine Acha Kwa ajili ya watoto wako.
Kuliko uchelewe kuzaa kisa kutafuta maisha huo muda ni Bora uutumie kuzaa na kuzichanga karata zako vizuri ili mwanao aishi vile ulivyotaka wewe.

Mfalme Daudi alitamani Sana kujenga nyumba ya Bwana, ndilo Hekalu lakini Mungu alimuambia yeye hatalijenga isipokuwa Suleiman mtoto wake.
Ndio maana nikakuambia sio kila Jambo zuri na kubwa ung'ang'anie lipitie kwako. Utapoteza muda wako bure na utaumia zaidi.

Ati sitaoa mpaka nijenge, au sitazaa mpaka nijenge, halafu ukiangalia mazingira hayakusapoti, tumia akili ndogo tuu. Angalia umri wako.

Wazo hilo labda uwe na miaka 18-24 lakini ukivuka hapo ukiona mambo bado hayaeleweki sio vibaya kubadilisha mtazamo lakini lengo likiwa palepale.

Utasema; nitazaa na kuoa ndipo nijenge ikiwa muda wa kuoa umefika.

Nakuhakikishia nyumba haitakusaidia kitu hata uwe nazo kumi Kama hujui kucheza na nyakati,

Maneno yangu haya ni Kwa Vijana waliotokea familia Masikini wanaotamani kuwa na Maisha Fulani wayapendayo, lakini uwezo hawana na muda unaanza kuwatupa Mkono.

Zaa katoto kamoja kabla ya 30 na Kama bado Hali unajiona ni ngumu malizia katoto kengine kabla ya miaka 40.

Zaidi; Maneno yangu sio sheria, Ila ushauri tuu Kwa jinsi huko mbeleni kulivyo.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Wakuu Kwema!

Leo sina mengi!
Ujumbe huu unawahusu zaidi wasomi hasa kutoka dini ya kikristo.

Vijana acheni kusubiri Embe kwenye Mnazi!
Msichelewe, ikiwa Una mwenza wako, na unamiaka 27-30 amueni kuzaa ikiwa mnaona mambo Yenu bado hayajakaa Sawa.
Msisubiri embe dodo kwenye mnazi. Safari ya maisha haiwi Sawa Kwa kila mtu.
Sio Kwa sababu Fulani kafanya Harusi ndipo kazaa basi nawe ufanye Kama wao. Unaweza kuzaa alafu baadaye ukafanya Harusi kulingana na Hali itakavyotengemaa.

Kulea mtoto ukiwa na miaka 27-35 kuna utamu wake Kwa kijana wa Kiume, Kama ilivyokulea mtoto ukiwa na miaka 21-30 ilivyoraha Kwa mtoto wa kike.

Sio lazima mfanye Harusi, ongeeni na wazazi wenu wa pande mbili, kajitambulisheni, kisha zaeni hiyo inatosha,

Msisubiri mambo yakae poa ndipo muoe, Kwa mwenendo WA dunia ulivyo Hali itaendelea kuwa ngumu kadiri na kadiri siku zinavyoenda.

Vigezo vya kuoa uwe na Ghetto lako, kitanda na Godoro, jiko, sufuria nne, bakuli na sahani na vijiko. Basi! Kama utaweza weka na kasabufa kakuwafariji mkiwa nyumbani, vuta jiko endeleeni na maisha.

Msitake makuu, msitake vingi ambavyo hamjui ni lini mtavipata. Kama kuna Jambo la kulipata ukiwa na nguvu basi ni Mke na watoto ili ujenge familia yako.

Dada zangu, msisubiri muolewe na watu wenye magari na majumba, mtasubiri Sana. Maisha hayahitaji kusubiri, ukipata kijana umpendae, mwenye sifa za mwanaume, awe na Ghetto lake, na vitu vya kuanzia maisha Mwambie upo tayari kuwa mke wake na kufanya maisha pamoja.

Nimeona Jambo hili litawagharimu Vijana wengi hapo baadaye, watajifanya hawataki kuoa na kuzaa Kwa kusubiria siku mambo yakikaa Sawa. Mwishowe watajikuta wanakosa vyote na hata wakipata watoto watapata Kwa kuchelewa na watateseka mno.

Usimsikilize ya watu.
Usiangalie njia za wengine wanazopitia, kila mtu ananjia yake.
Usiwaige Wazungu na kujifanya mtu wa Kisasa wakati ulimwengu unaoishi ni Wakale.

Tafuta binti, nenda kwao kajitambulishe, kulingana na uwezo wako kama huwezi kutoa mahari sema, au lipa kidogo hata robo ya mahari, chukua mke Anza maisha na familia yako.
Usijenge familia kukiwa kumekucha.

Msiogope, msifuate mkumbo! Zaeni, ndipo mfunge Harusi ikiwa ndoto yenu ilikuwa kufanya Harusi kubwa.

Niwatie moyo Vijana wa kizazi hiki, naelewa mnapitia kipindi kigumu mno, wanaowatumaini walipaswa watumainiwe wao Kwa kuwapa Urithi mbali na kile wakiitacho Elimu.

Msiwafuatishe! Msiwasikilize! FANYENI maisha yenu mapema kungali mchana, zaeni na wanawake mnaowapenda mkaishi nao, msitake mambo makubwa.

Sio kila Jambo zuri na kubwa lazima lipitie mikononi mwako, mengine Acha Kwa ajili ya watoto wako.
Kuliko uchelewe kuzaa kisa kutafuta maisha huo muda ni Bora uutumie kuzaa na kuzichanga karata zako vizuri ili mwanao aishi vile ulivyotaka wewe.

Mfalme Daudi alitamani Sana kujenga nyumba ya Bwana, ndilo Hekalu lakini Mungu alimuambia yeye hatalijenga isipokuwa Suleiman mtoto wake.
Ndio maana nikakuambia sio kila Jambo zuri na kubwa ung'ang'anie lipitie kwako. Utapoteza muda wako bure na utaumia zaidi.

Ati sitaoa mpaka nijenge, au sitazaa mpaka nijenge, alafu ukiangalia mazingira hayakusapoti, tumia akili ndogo tuu. Angalia umri wako.
Wazo hilo labda uwe na miaka 18-24 lakini ukivuka hapo ukiona mambo bado hayaeleweki sio vibaya kubadilisha mtazamo lakini lengo likiwa palepale.
Utasema; nitazaa na kuoa ndipo nijenge ikiwa muda wa kuoa umefika.

Nakuhakikishia nyumba haitakusaidia kitu hata uwe nazo kumi Kama hujui kucheza na nyakati,

Maneno yangu haya ni Kwa Vijana waliotokea familia Masikini wanaotamani kuwa na Maisha Fulani wayapendayo, lakini uwezo hawana na muda unaanza kuwatupa Mkono.

Saa katoto kamoja kabla ya 30 na Kama bado Hali unajiona ni ngumu malizia katoto kengine kabla ya miaka 40.

Zaidi; Maneno yangu sio sheria, Ila ushauri tuu Kwa jinsi huko mbeleni kulivyo.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Endelea kudanganya vijana, mambo kwenye field ni tofauti sana na unachoandika, usifikiri mtoto ni kuingiza jinsia yako ukeni na kutungisha mimba? Kuna mengi kwenye ndoa, okay ukikua utaelewa.
 
endelea kudanganya vijana, mambo kwenye field ni tofauti sana na unachoandika, usifikiri mtoto ni kuingiza mbegu ukeni na mimba , kuna mengi kwenye ndoa, okay ukikua utaelewa.

😀😀

Kwa hiyo hawa vijana ambao hawajasoma na wanaendelea na maisha Yao unawazungumziaje.
Wengine hata miaka 25 hawaijui lakini wanajitahidi kutunza familia zao.

Tatizo Vijana wa siku hizi ninyi mliosoma mnamawazo ya kitoto😀😀 mnawaza makubwa Kama vitoto vya mbuni,

Mkija kuamka mmeshazeeka na ndoto zenu zikiwa angani mbawa za kupaa na kuzinyakua hamna!

Ndoa ipo Kwa ajili ya watu walioamua kuishi sio nyie mliongia na ndoto za mbuni ndio maana mnaziona ni ngumu.
 
Tatizo lako ni moja tu, kuna muda fasihi zako wewe mwenyewe zinakinzana kwa mfano uliwahi kuandika fasihi ukisema kuwa mwanamke hapendi ila anatii, na hawezi kukupenda kama hauna kitu. Leo umebadilika na kuanza kuwaambia wanawake wasisubiri kuolewa na wenye majumba na magari bali waangalie zaidi kama amempenda kijana. Sasa inakuaje tena mwanamke huyu huyu anapenda wakati mwanzo ulisema wao hawapendi ? [emoji848][emoji848]
 
Wanawake hawana Upendo WA dhati. Hiyo haibadiliki, isipokuwa Kwa watoto wao
 
Nilipata watoto wawili nikiwa sitaraji kuwa na mtoto kipindi hicho wala sikuhitaji mtoto wala kuishi na mwanamke nikiwa na miaka 23 tayari na watoto wawili nilijichukia, mawazo kichwani niliogopa hata kuwaambia home nilijiona kama ni mkosi kwenye maisha yangu ule mwaka nilipata stress ya hatarii hadi nikapata vidondaa vya tumbo.

Aisee usione watu wanajiua ukaona ni wangese msongo WA mawazo ni Jambo Baya sana Ila huyu bidada niseme Tu amenisaidia sana kuituliza akili yangu Mungu akikujaalia kupata mwanamke mpole mkimya na anayekujali shukuru sana Mungu kwenye nyakati ngumu ni msaada mkubwa sana kwako, wanakupa Moyo na kukufanya matatizo uyatatue kiutulivu sana naingia 30 nikiwa strong sana from nothing now namalizia kibanda Changu, biashara zinakwenda na mwaka huu wamekuja wawili wengine thanks Allah Kwa zawadi hiii.
 
Sio mashindano ya NBC league kwamba usipofuzu pointi unatolewa 😊😊😊😊

Waza mengi sana before hujazaa .
 
Back
Top Bottom