"Usijenge Familia kukiwa kumekuchwa" Vijana Zaeni na oeni mungali mna nguvu

"Usijenge Familia kukiwa kumekuchwa" Vijana Zaeni na oeni mungali mna nguvu

Shughuli yoyote halali inayoingiza pesa mfukoni inaeleweka.

Sent from my CPH2349 using JamiiForums mobile app
chief nimemaanisha yani shughuli yoyote ya kukuwezesha kupata hela ya kutosheleza mahitaji makuu muhimu hususani chakula,malazi,mavazi,usafiri na matibabu
kumbuka kwamba sio kila shughuli Bali shughuli ya kueleweka ndo inaweza kukupatia hela ya kutosheleza vitu vya hapo juu
 
Yani Sina Kaz nitafute mtoto wa nini atakula nini ? Kama mimi baba mtu mlo wangu wa shida ?
 
Wrong..! Wanawake wanaupendo Ila hawana utii

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app

Wanawake hawapendi sio asili Yao Kupenda
Labda hujui maana ya Kupenda, upendo ni Kutoa, kati ya mwanamke na Mwanaume Nani anatoa?

Mwanaume ni provider
Mwanamke anapokea.

Kama ulikuwa unajidanganya mwanamke anapenda utakuwa upo wrong,

Acha kazi
Usimpe pesa,
Usitoe chochote alafu uje hapa useme tena Kauli yako.

Alafu yeye aache kazi,
Asiwe na pesa, alafu uone Kama hamtaendelea kupendana.

Ni logic ya kawaida hata Kwa mtu ambaye hafikiri vizuri
 
Wanawake hawapendi sio asili Yao Kupenda
Labda hujui maana ya Kupenda, upendo ni Kutoa, kati ya mwanamke na Mwanaume Nani anatoa?

Mwanaume ni provider
Mwanamke anapokea.

Kama ulikuwa unajidanganya mwanamke anapenda utakuwa upo wrong,

Acha kazi
Usimpe pesa,
Usitoe chochote alafu uje hapa useme tena Kauli yako.

Alafu yeye aache kazi,
Asiwe na pesa, alafu uone Kama hamtaendelea kupendana.

Ni logic ya kawaida hata Kwa mtu ambaye hafikiri vizuri
Vipii mwanamke akikwambia ana kupenda,Ana kuwa ana manisha nini
 
Nilipata mtoto nikiwa na miaka 18 sina godoro wala kijiko cha miambili asee asante Mungu saiz nafurahia
 
Kuoa ni ujinga fulani hivi. KUOA SIYO LAZIMA.
 
Wakuu Kwema!

Leo sina mengi!
Ujumbe huu unawahusu zaidi wasomi hasa kutoka dini ya kikristo.

Vijana acheni kusubiri Embe kwenye Mnazi!
Msichelewe, ikiwa Una mwenza wako, na una miaka 27-30 amueni kuzaa ikiwa mnaona mambo Yenu bado hayajakaa Sawa.
Msisubiri embe dodo kwenye mnazi. Safari ya maisha haiwi Sawa Kwa kila mtu.
Sio Kwa sababu Fulani kafanya Harusi ndipo kazaa basi nawe ufanye Kama wao. Unaweza kuzaa halafu baadaye ukafanya Harusi kulingana na Hali itakavyotengemaa.

Kulea mtoto ukiwa na miaka 27-35 kuna utamu wake Kwa kijana wa Kiume, Kama ilivyokulea mtoto ukiwa na miaka 21-30 ilivyoraha Kwa mtoto wa kike.

Sio lazima mfanye Harusi, ongeeni na wazazi wenu wa pande mbili, kajitambulisheni, kisha zaeni hiyo inatosha,

Msisubiri mambo yakae poa ndipo muoe, Kwa mwenendo WA dunia ulivyo Hali itaendelea kuwa ngumu kadiri na kadiri siku zinavyoenda.

Vigezo vya kuoa uwe na Ghetto lako, kitanda na Godoro, jiko, sufuria nne, bakuli na sahani na vijiko. Basi! Kama utaweza weka na kasabufa kakuwafariji mkiwa nyumbani, vuta jiko endeleeni na maisha.

Msitake makuu, msitake vingi ambavyo hamjui ni lini mtavipata. Kama kuna Jambo la kulipata ukiwa na nguvu basi ni Mke na watoto ili ujenge familia yako.

Dada zangu, msisubiri muolewe na watu wenye magari na majumba, mtasubiri Sana. Maisha hayahitaji kusubiri, ukipata kijana umpendae, mwenye sifa za mwanaume, awe na Ghetto lake, na vitu vya kuanzia maisha Mwambie upo tayari kuwa mke wake na kufanya maisha pamoja.

Nimeona Jambo hili litawagharimu Vijana wengi hapo baadaye, watajifanya hawataki kuoa na kuzaa Kwa kusubiria siku mambo yakikaa Sawa. Mwishowe watajikuta wanakosa vyote na hata wakipata watoto watapata Kwa kuchelewa na watateseka mno.


Usimsikilize ya watu.
Usiangalie njia za wengine wanazopitia, kila mtu ana njia yake.
Usiwaige Wazungu na kujifanya mtu wa Kisasa wakati ulimwengu unaoishi ni Wakale.

Tafuta binti, nenda kwao kajitambulishe, kulingana na uwezo wako kama huwezi kutoa mahari sema, au lipa kidogo hata robo ya mahari, chukua mke Anza maisha na familia yako.
Usijenge familia kukiwa kumekucha.

Msiogope, msifuate mkumbo! Zaeni, ndipo mfunge Harusi ikiwa ndoto yenu ilikuwa kufanya Harusi kubwa.

Niwatie moyo Vijana wa kizazi hiki, naelewa mnapitia kipindi kigumu mno, wanaowatumaini walipaswa watumainiwe wao Kwa kuwapa Urithi mbali na kile wakiitacho Elimu.

Msiwafuatishe! Msiwasikilize! FANYENI maisha yenu mapema kungali mchana, zaeni na wanawake mnaowapenda mkaishi nao, msitake mambo makubwa.

Sio kila Jambo zuri na kubwa lazima lipitie mikononi mwako, mengine Acha Kwa ajili ya watoto wako.
Kuliko uchelewe kuzaa kisa kutafuta maisha huo muda ni Bora uutumie kuzaa na kuzichanga karata zako vizuri ili mwanao aishi vile ulivyotaka wewe.

Mfalme Daudi alitamani Sana kujenga nyumba ya Bwana, ndilo Hekalu lakini Mungu alimuambia yeye hatalijenga isipokuwa Suleiman mtoto wake.
Ndio maana nikakuambia sio kila Jambo zuri na kubwa ung'ang'anie lipitie kwako. Utapoteza muda wako bure na utaumia zaidi.

Ati sitaoa mpaka nijenge, au sitazaa mpaka nijenge, halafu ukiangalia mazingira hayakusapoti, tumia akili ndogo tuu. Angalia umri wako.

Wazo hilo labda uwe na miaka 18-24 lakini ukivuka hapo ukiona mambo bado hayaeleweki sio vibaya kubadilisha mtazamo lakini lengo likiwa palepale.

Utasema; nitazaa na kuoa ndipo nijenge ikiwa muda wa kuoa umefika.

Nakuhakikishia nyumba haitakusaidia kitu hata uwe nazo kumi Kama hujui kucheza na nyakati,

Maneno yangu haya ni Kwa Vijana waliotokea familia Masikini wanaotamani kuwa na Maisha Fulani wayapendayo, lakini uwezo hawana na muda unaanza kuwatupa Mkono.

Zaa katoto kamoja kabla ya 30 na Kama bado Hali unajiona ni ngumu malizia katoto kengine kabla ya miaka 40.

Zaidi; Maneno yangu sio sheria, Ila ushauri tuu Kwa jinsi huko mbeleni kulivyo.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Kila jambo na wakati wake, yupo atakayewahi yupo atakayechelewa. Kikubwa uamuzi huo ufanyike mwili na akili vikiwa na utayari
 
Kila jambo na wakati wake, yupo atakayewahi yupo atakayechelewa. Kikubwa uamuzi huo ufanyike mwili na akili vikiwa na utayari

Umesema kweli Kabisa.
Upo Wakati WA asiyesoma na aliyesoma mwenye uhakika wa kuajiriwa Kwa Dani aliyosomea muda wowote hata ipitie miaka 20
 
Back
Top Bottom