safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
TUSIKATE TAMAA.
Ukijiona upo duniani basi jua tayari wewe ni mshindi,usiseme huwezi chochote.uwepo wako hapa duniani ni ishara tosha wewe umeshinda ndio maana uko hapa.
Wakati baba alipomwaga maji ya uzazi yenye ujazo wa kijiko kimoja basi ujazo huo ulikuwa na seli zaidi ya milioni moja wakati huo seli moja tu ndio inayotungisha mimba na seli zilizobaki zinakufa.
Punde baba akimwaga maji yenye seli zaidi ya milioni ikiwemo na seli yako wewe,seli hizi kila moja ilijitegemea kukimbia na kutafuta yai la mama katika fuko lake la uzazi.
Mamilioni ya Seli hizi hukutana na na vikwanzo vingi katika uke wa mama na kupelekea seli nyingine kufa njiani kabla ya kulifikia yai
Seli moja inafanikiwa kulifikia yai na kukumbatiana nalo na yai hili hujifunga na kuzuia seli nzigine zisiweze kuingia.
Seli hii ambayo imeingia pengine ilichelewa kufika yaani kuna seli zilikuwepo hapo zikimeng'enya yai ili zipate kuingia ndani lakini hazikufanikiwa,lakini ilipofika seli yako ikafanikiwa.
Kitendo cha seli yako kufanikiwa kuingia katika yai la mama huu ni ushindi tosha kwa sababu zingine hazikufanikiwa.
Seli yako ilipoingia katika yai la mama vikaungana pamoja na kuwa kiseli kimoja ambacho huwezi kukiona kwa macho.
kiseli hiki kikaanza kujigawagawa vikawa viwili,vitatu,vinne,makumi mamia na maelfu na kadri kinavyozidi kujigawa ndio kinazidi kuwa kikubwa na kuanza kuonekana kama mimba katika tumbo la mama.
Huu mchakato wote ni baada ya wewe(seli)kushinda kuingia katika yai la mama na huku ukiwaacha wenzio(seli zingine)kwenye mataa na kushindwa kupata fursa ya kuonekana hapa duniani (yaani mimba)
Kwa nini unajidharau wakati umezaliwa ukiwa ni mshindi ?
Wewe hapa duniani no cheti kwamba ulishinda mamilioni ya seli huko tumboni.
Kama uliweza kuzishinda seli zingine ukiwa katika mbio kule tumboni kwa mama kwa nini ukate tamaa katika tumbo hili la dunia ?
Hukumbuki chochote wakati ukiwa seli unakimbilia yai na ukashinda,kwa nini USISHINDE wakati huu ukiwa na kumbikumbu zako ?
Usikate tamaa,wewe ni mshindi.
Asubuhi njema.