Usikose vifaa hivi nyumbani kwako!

Usikose KOROBA, baadae utanishukuru. Lile dude ukimgonga nalo kibaka hatembei mita kumi.

Yote kwa yote hivi ni vifaa muhimu majumbani.
 
Ni kweli mkuu...Mimi naishi pembezoni mwa mji enzi hizo ukihamia sehemu nyingine ni pori tu so wadudu hawakosekani,chumbani kwangu niliweka koleo (lile mafundi wanachoteaga mchanga).
Siku moja asubuhi ya jmosi mapema naingia washroom ile nimemaliza kumwaga maji namwona nyoka..salama yangu ilikuwa ni hilo koleo tu...nilichukua kolea nikaanza pambana na nyoka kama dk 12 hivi mpaka nikamjeruhi baadae akafa.
Toka siku hiyo naishi na koleo +fimbo ngumu ndefu chumbani.
 
Mjini jembe sio la muhimu sana, hiyo namba 6 mjini ndio kila kitu, inaweza kukupa ajira ya ghafla usiyoitarajia usife njaa, hizo bisibisi/tester wengine wanatembea nazo mfukoni kabisa.
 
1. Washing machine
2. Mashine ya kusaga
3. Mashine ya kujaza upepo tairi la gari
4. Duka la dawa hapo home
5. Tractor dogo la kubota
6. Mashine ya kurandia mbao
7. Mashine.ya kufyatulia tofali


Endelea kuorodhesha vitu muhimu vya kuwa navyo home.
 
Mkuu vyote ulivyotaja, nimejikuta nakosa ngazi tu! Ha ha ha haaaa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…