Usikose vifaa hivi nyumbani kwako!

Hapo mwishoni ndipo uliponiacha hoi yaana mada ya likizo ila umetuwekea mpaka namba ya simu daaa..!!

.....😆😆😆😆😆😂😂😂
 
Kweli kuna vifaa sio vya kukosa, unakuta mtu hana nyundo, screw driver wala tester...kitu kidogo anamuita fundi alaf ni mwanaume [emoji3][emoji3]
Last time nimenunua driver set ya laptop, mimi mpka kitu nipeleke kwa fundi bas niwe nimehangaika nimeshindwa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwangu Sina sululu tu, kwangu vitasa hata kiwe Cha sylinda nabadilisha mwenyewe
 
Umenikumbusha,nilinunua nyundo na msumeno ghafla sivioni sjui hata nani nilimwazimisha

Huwa ninapenda kujifanyia vitu mwenyew sasa nikitaka kutengeneza baadhi ya vitu au kurekebisha siwez

Majirani wasio waaminifu wameshanipotezea vitu vingi,mwingine nilimwazimisha jembe akalipeleka shamban mpaka msimu unaisha kurudisha jembe limebak nusu
 
vifaa muhimu sana ni kwavile wengi wetu hatuhitaji kujitegemea zaidi.
kupanga chumba kimoja hakufanyi ww ukose zana muhimu ila haya mambo ni yakujifunza toka udogoni ,hukujifunza huwez elewa ukubwani.

wanasema hatuishi kujifunza
 
Kwa kifupi unahitaji kuwa na ghala dogo la kuwekea vitendea kazi vya msingi nyumbani kwako
 
Ndiyo hivyo wakishatumia wanaona hakina thamani tena, kuna jirani aliazima shoka kitambo kalipoteza,

Majembe/chepe/nyundo walishaazimaga na kupotea mazima na wanajisahau wakiwa wana shida tena wanakuja kuazima wanasahau kama vimepotelea kwao,

Now ni kuwanyima tu,wakija kuomba jibu ni hatuna sijui nani aliazima na hajarudisha.
 
Fundi aliniletea kitanda kaweka machaga marefu kusudi, na bawaba upande mmoja hajaweka,alitaka nimuite tena[emoji23]

siku ya pili nikachukuwa zangu tap na msumeno, bawaba zipo nikapima na kukata na kufunga,

ikapita miezi nikakutana nae nikamuuliza vipi mbona uliweka chaga mirefu?? Akasema niliweka kusudi hili siku nikija kufunga nipunguze[emoji16],,nikamjibu tu sawa nitakujulisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…