Usiku huu huku kwetu usiombe kabisa.....hatulali!

Usiku huu huku kwetu usiombe kabisa.....hatulali!

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Usingizi wenyewe umekata kabisa...pamoja na kuwa ni wa kuokoteza okoteza bado hamna kitu. Umewahi kusikia usingizi wa mang'amu ng'amu? Basi ndo uswahilini inavyokuwa yaani mtu kama kalala lakini dk mbili tu unakuta kashtuka kitandani amerusha teke katua chini anatafuta chupa au kakunja ngumi.... Yaani muda wote ni wa kujihami tu na maisha.maskini hapumziki ndugu yangu.

Imagine usingizi wenyewe ni wa kudunduliza sana...karibu week nzima hujalala unaweza lala siku moja tu nayo sasa ndo unakutana na usingizi wa mang'amu ng'amu. Mara wanga waje nao kukukaba.sasa unashangaa wao wameamua wenyewe kutolala why wanataka wakuamshe mkeshe wote?

Unalala kimachale machale sana maana jamaa wa kuvua simu n.k wanaingia nao night shift.uswahilini hakuna heri kabisa.mchana inzi usiku mbu.unalala unaona mtu katumbua mijicho yke dirishan anataka kuvua simu yako au nguo.ukicheck nguo zenyewe ulinunua kwa kujibana sana.

Umewahi mbembeleza machinga akupunguzie bei mpaka unamwambia asikuone vile umefiwa na ndugu woote umebaki peke yako tu, hujala siku mbili,una vidonda vya tumbo, una tb na wengine wanasema una ngoma... Yaani hapo unamwelezea hayo akuonee huruma akupunguzie bei.

Hapo jioni umekula hindi la kuchoma.na hapo usijichanganye ukawa umechagua laini... Linaisha mapema sana tumboni. Unachagua hindi kubwa na gumu hasa.hilo hata muuzaji anakupunguzia anakuuzia tsh 600 badala ya 700.

Hapo maneno mengi kweli..." Haya mahindi ya wapi?mbeya au iringa? Maana ya mbeya ndo matamu kinyama.... Ya leo haya ?yameletwa na bomber dear? Huku unageuza geuza hindi lipate moto.maana hilo hindi lilichomwa asubuhi kila mtu ashalitest so unakuta lina mapengo mapengo mengi sana. Hujali wala nini.

Baada ya hapo unachukua kipande cha ndimu unachovya kwenye pilipili chumvi na kusugua sana hindi lako.upate ladha.mpakaa muuzaji unaona anaanza kutengeneza matuta usoni.maana sasa unataka maliza ndimu zake na pilipili chumvi.

Unarudi home taratibu unatafuna hindi lako....unaenda shushia na maji mengi then ndo unaanza sasa kuutafuta usingizi.hapo unahangaika sana.akili haitaki...inaona kabisa unadanganya.unalalaje leo siku nzima hujaingiza kitu?

Maskini halali...kitandani ndo anaanza fanya discussion binafsi ya siku nzima na kesho inakuaje.hapo hujaanza sikia tumboni minyoo inalalamika...yaani unailisha chakula cha hovyo...mipilipili ,ndimu na chumvi.... Tumbo linanyongorota kinyama.

Ndani nako panya wanakimbizana kugombea kigunzi ulichokuja nacho...unasikia kabisa wanalia kugombea ....kama unge wacheck...wamekondaaa. wanaishi kwako basi tu sababu wewe hata muda wa kuwapa sumu huna.

Hiyo pesa ya kununulia sumu ungekuwa nayo si ungeshanunua ukanywa hata wewe mwenyewe ujifie tu kitandani.ila ndo huna sasa.so wanashukuru hilo.huwatilii sumu.

Hapo unalalaje? Nambie mwenyewe usingizi unatoa wapi?azima kwa watu kama akina mengi labda.unavuta hisia za kulala haziji kabisa.unavuta hisia za kulala unaona blank tu.

Sasa itokee siku ndo umedunduliza dunduliza usingizi week nzima siku hiyo umekubali.wanga nao hawa hapa... Wameleta na vitoto vyao kuvifundisha kukaba... Basi siku hiyo unakabwa shingoni mpaka miguuni.umkiamka unatokwa na jasho unahema juu juu.hasira,ghadhabu na fadhaa.

Ukicheck saa ni saa 10 na nusu alfajili inatakiwa uamke ujiandae kuwah kazini..maana saa moja na nusu unatakiwa uwe getini...umsubirie mdosi aje saa mbili hivi kufungua geti.

MASKINI HAMPUMZIKI.USIKU HUU KWETU... HATULALI...Tunakesha vitandani tu. Nyie wengine laleni bwana. Ndo maana mnatakiana usiku mwema.sisi wema wa usiku tutauona wapi? Mchana inzi usiku mbu.
 
Juhudi Hufata Mafanikio,,Good to Go,Yaani uswahilini ata uotaji wa ndevu kwa wanaume ni wa hovyo hovyo,Watu wanaota ndevu hadi maskioni!!Hadi ma'mamiloo wanauchebe wengine garden love kifuani kama wanaume.!!
 
Asee umenikumbusha mbali sana.....maisha haya!
 
Back
Top Bottom