Huu mchezo umeanza tena kuharibiwa kama mwanzo. Yaani kweli wadhamini wanaweka pesa zao na watu wanalipa kiingilio kwenda kuangalia bondia feki kabisa yule mmisri. Jamaa hata kurusha ngumi hawezi kabisa. Halafu kesho utamsikia Mfaume anasema namtaka Mwakinyo ulingoni.
Kwa hivi karibuni mchezo wa ngumi ulianza kushika kasi sana na kuwa na wapenzi wengi na hata wadhamini wengi pamoja na kutoa ajira kwa vijana wengi lakini kwa haya yanayofanyika sasa huu mchezo utarudi kaburini tena. Ni wakati sasa wa serikali kuingilia kati kama ilivyozuia mabondia kujiondokea tu kwenda nje kupigwa halafu wanapewa pesa wanawapandisha watu viwango huko nje basi sasa hivi iingilie kati iwe na udhibiti wa mabondia kutoka nje wanaokuja kucheza hapa nchini. Vinginevyo itakuwa tu mtu anaokota kinyozi au mlevi huko nje ya nchi anampa dili anamleta hapa nchini anamkungúta "knock out" ya uwongo uwongo biashara imeisha wakati watu wamelipa viingilio.
Mkuu Naona kama Mwarabu alikuwa anatumika kumrudisha Mfaume mchezoni maana alishapotea
Usikute mmsiri amelipwa ili apoteze pambano.
.
Maana naona kapigwa kirahisi sana.
.
Unajua huyo Mfaume alipotea kwenye ramani so inabidi atafute Lonya ashinde ili aweze kurejesha imani kwa mashabiki zake.
.
Hakuna cha CV kubwa Hapo Jamaa Ni Lonya Tu.
.
Mkiwa Kama Watu Wa boxing na mkitaka boxing iendelee Kama kweli mna nia ya kuupeleka mbele mchezo wa boxing bongo.
.
Basi waambieni Wacheza Ndondi wenu waache kupigana na aina hii ya wapinzani, hawatawapeleka popote.
.
Mtu ana loss 24 unapigana naye ili iweje, ili akupeleke wapi?
.
He is nobody kwenye boxing, hata ukishinda no one cares.
.
Kwenye boxing watu wa namna hii tunawaita
Journeyman
Sent from my Infinix X657 using
JamiiForums mobile app