Usikubali kuwa mtu wa kukumbukwa na marafiki wakiwa na shida tu, wewe sio choo

Usikubali kuwa mtu wa kukumbukwa na marafiki wakiwa na shida tu, wewe sio choo

Jf kila mtu tajiri kasoro wanaoomba kazi na ajira tu😁
 
Ukiwa unatafutwa nyakati ngumu maana yake ur the chosen one .

MTU anapokufata umsaidie hasa anapokuwa broke -financially , or stressful maana yake kuna nguvu umebeba ya kuwa problems solver.


Unachobidi kufanya ni Ku-link na universe au ur higher power ili ikuletee New knowledge or revelation ili uwaisaidie.


Katika maisha you need to practice win to win situation in business and not in life .

So kuanza kuweka mipaka katika maisha yako ni kuamua kuzuia positive energy to flow in ur life.



Mimi nachojua watu wanotafutwa kutoa msaada ndo huwa wanainuliwa na universe /God

Ushauri wako umekaa kutengeneza watu wawe self-centered kitu ambacho kitawafanya wawe broke zaidi na kuishia kuwa na mediocre life.
 
UKIONA WANAKUKUMBUKA TU WAKIWA NA SHIDA JUA UMUHIMU WAKO NI MDOGO KWENYE MAISHA YAO MENGINE 😔

Ukitafutwa kwenye shida tu tafasiri ni kuwa muda mwingi wakiwa na raha hutumia na wengine ila kwenye majanga ndio wanakukumbuka wewe na baada ya utatuzi unasahaulika tena, Wewe sio Choo.

Hata Choo huwa kinakumbukwa kusafishwa kisha ndio kinasahaulika mpaka mtu apate haja ndio anakumbuka tena umuhimu wa Choo, ila wewe hata salaam hawakupi na siku ukiona tu meseji yao au mwito wao moja kwa moja akilini unajiandaa kutatua shida, kwanini wakukumbuke nyakati ngumu tu?

Tena sifa ya watu hao kubwa ni kuificha pindi wewe ukiwa unawahitaji na hapo utasikia vizingizio vya kila namna kutoka kwao.

Sasa kuna mtu akiwa anatafutwa kwenye shida tu hivimba kichwa na kujiona yeye ndio kila kitu mjini 😄 Janjaruka acha ujinga huo kwani wengine hutafutwa kwenye raha ila wewe unatafutwa kwenye shida na hulipwi chochote.

Kataa kabisa kuwa mtu wa kutafutwa kwenye majanga na sio kwamba wewe ni mtatuzi mzuri la hasha bali wamkuona wewe ni mdhaifu kwenye kipengele hicho ndio maana usipomsaidia zaidi ya mara mbili hutafuta pengine dhaifu kwa sababu tayari anakuona umekuwa mjanja sasa 😊

Mwanasayansi Saul Kalivubha

Mitandaoni kwa jina la Fikia Ndoto Zako.

+255652134707
🫡🫡
 
Back
Top Bottom