Usilazimishe kuwa na vigezo, achia wenye vigezo nawe nenda unapofaa

Usilazimishe kuwa na vigezo, achia wenye vigezo nawe nenda unapofaa

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
Usifanye hili kosa la kulazimisha uwe na vigezo ili ufae sehemu usiyo stahili ilihali kwa vigezo vyako kuna sehemu ungefaa tu na kufurahia.

Madhara yake ni makubwa sana kwa sababu utalazimika kudanganya au kujivisha vazi ambalo linakupwaya ili tu uonekane mwenye vigezo sehemu usipostahili, Kwa kufanya hivi utaonekana unafaa ila ni lazima utaumbuka na kufilisika pia.

Kwa sifa ulizonazo nenda unapostahili kuwa ikitokea kuna nafasi nyingine inayokuhitaji ila huna sifa hizo basi ongeza vigezo huku ukiwa sehemu yako unayofaa hapo utakuwa umetumia utaratibu unaotakiwa na asili .

Kwenye mahusiano ukilazimisha ufae utajikuta ukiishi maisha ya mtu mwingine ambaye ndiye alistahili hiyo nafasi kitu ambacho utakimudu awali ila baadaye utarudi tu kwenye uhalisia wako na hapo ndio mwanzo wa mahusiano kufa na kuaibika.

NENDA UNAPOSTAHILI KULINGANA NA SIFA ZAKO, ACHA KULAZIMISHA KUFAA USIPOSTAHILI.

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#fikia Ndoto Zako.
 
Kwamba nisitongoze madem matawi ya juu kwa kuhofia vigezo?

niache wewe
 
Back
Top Bottom