SEHEMU YA NANE
Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,,
Asubuhi wanakuja rafiki zake pale, ni wale nlikuwa nawaona pale wanajiuza, akawa anawatambulisha kuwa mi ni shemeji yao, basi sawa, nikakaa paka mchana tukala ugali fresh, Nikaondoka zangu kurudi chuo
Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Nikafika chuo nikalala sana siku hiyo maana hatukuwa na pindi, Nilipo kuja kushtuka nikaanza kutafakari yote yaliyotokea jana, Nikajilaumu sana maana hii yote ni sababu ya kuanza mapenzi ukubwani,
Basi ikawa ndo tabia yangu, usiku ukifika natinga kofia yangu najiachia buguruni, Nafanya yangu huko narudi room night kali nalala, Siku moja nikiwa na Jane kwenye vile vyumba vya short time mara mlango ukagongwa kwa nguvu, " Tokeni huko nyie washenzi" , Jane akaniambia hao ni polisi, Nikasema mbona hiki kisanga tena, sasa itakuwaje, itakuwaje sasa? Akasema kwa nyie hawana shida, kwa sisi ndo shida,
Basi mlango ukaendelea kugongwa, Jane akaenda kufungua, jamaa wakaingia wakatukamata na matusi kibao, tukatoka nje, kuna wengine nao wamekamatwa, Basi sisi wanaume tulikuwa kama sita, tukafungwa mashati wawili wawili, tukaswagwa na wale mademu paka kwenye gari ya polisi,
Tukazama ndani, tume kaa chini gari ikaamsha, Nikamuuliza Jane hapa tunaenda wapi? Akasema kituoni,
Basi tukazungushwa pale buguruni, mwisho tukapelekwa kituoni buguruni rozana , tukaambiwa vua mikanda,vua viatu, toa kila kitu weka mezani, tukafanya hivyo,
Haya kaa chini, tukaandikishwa majina pale, tuka kaa tunaskilizia, wale maaskari tuliokuja nao na gari wakawa wameondoka na gari, wakabaki wale tuliokuwa tumewakuta pale kituoni,
Baada kama lisaa tukiwa tumekaa pale nawaza sijui itakuwaje taarifa zilifika chuo, nikiwa bado nawaza, ndipo askari mmoja akasema oyaa, nyie semeni mna nini muondoke hapa, mkikaa hapa paka kesho tunawapeleka mahakamani, nikasema ukisikia kirangasi ndo hichi sasa,
Basi jamaa mmoja akasema mi nna elf 10 afande, Nikasikia we mwana haramu nini!! Yaan hao malaya uwape elf 10 na sisi utupe elf 10! Hanisi wewe, eeenh na nyie wengine, Mi nikasema nna elf 10 pia, Yule afande akasema nyie mna leta utani, ebu sogeeni hapa,
Basi tukaenda pale mezani, Akasema toeni hizo hela, Basi mi nikaomba walet yangu ilikuwa pale mezani, nikatoa buku ten, nikachukua vitu vyangu nikasepa, na wale wengine nao wakatoka tukawaacha wale mademu kule maana walikuwa chumba kingine, Basi nikatoka pale nikadandia gari nirudi zangu chuo, moyoni najiapiza sirudii tena yaan leo ndo mwisho, nikarudi room nikalala,
Ikapita kama wiki hivi sjatia maguu tena buguruni, Ila badae uzalendo ukanishinda, nikaona usintanie nikajiachia huyooo kama kawa, Nikakutana na Jane nikamuuliza siku ile ilikuwaje, akasema walilala paka asubuhi pale kituoni, kesho yake wakadeki mule ndani na kufagia nje alafu wakaachiwa,
Basi ikawa ndo tabia yangu, siku nyingine simtafuti Jane nabadilisha ladha, Nikaotea chimbo lingine mwanzoni huku kabla hujafika sheli kunasehemu wanauza mbao, basi pale ni chap kwa haraka, nyuma ya zile mbao tu mmna malizana unampa buku tatu yake unasepa,
Basi siku moja nipo room Happy akanipigia akaanza kuongea analia, analalamika siku hizi nimemtupa hata simpigii, Nikajitetea pale kwamba shule imekaba ndo maana, Alafu akaniambia kwamba ana miezi kadhaa haoni siku zake, Ukisha ambiwa hivyo unajua tu ni nini kinafata,
Basi akasema anahisi ana mimba maana dalili zote zimeshajionesha hadi home wameshamtilia mashaka, Basi nikampooza pale kuwa ntamtumia hela aende hospital akapime, Basi tukaongea mengi, nikaahidi bado nna mpenda na hata kama ana mimba mimi kwangu ni furaha kuitwa baba,
Basi siku zikaenda, test zikaja, UE hii hapa, tukapiga pale shule ikaisha watu wakasepa zao kwenye mafield huko, Mimi field yangu nikafanyia hapa hapa Dar, Happy nikamtumia hela akaenda kupimwa akakutwa na mimba ya miez mi nne, Kidume ukiskia mziki ndo huo, Basi home kwao walipogundua dingi yake akamfukuza aende kwa mwanaume alie mpa mimba, Basi akaenda kuishi kwa Anti yake kijiji cha jirani,
Itaendelea