Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

"Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha"
Mwanaume unatafuta maisha popote pale unapoona kuna fursa hata km hauna ndugu.
Mm mwenyewe ni mfano hai, hapa nilipo nilikuja sina ndugu wala rafiki. Nililipa chumba miezi 3 nikabakiwa na 2,000 tu mfukoni. Natandika boksi nakujifunika shati, nimeshalala na njaa mpk siku 2 lkn sasa najimudu maisha. Nalala sehemu safi na nimeoa.
Maisha popote haijalishi una ndugu au hauna huko.
Itaendelea
 
Sa mbona nawewe hujaleta stori yako inayohimiza watu waende sehemu wasizozijua kutafuta maisha
 

Huyu mjinga ni wakula ban haiwezekani hadi sasa unaendelea kuleta hadithi za uongo uongo ili uonekana shujaa
 
SEHEMU YA TISA

Ilipoishia,,,,,,,,,,,,

Basi home kwao walipogundua dingi yake akamfukuza aende kwa mwanaume alie mpa mimba, Basi akaenda kuishi kwa Anti yake kijiji cha jirani,

Endelea,,,,,,,,,

Field ikaenda poa, mchakato wa kurudi chuo ukaanza tena, mwaka wa tatu huo tunaingia, ila saivi nikasema skai tena campas, na mimi nataka saivi niende mtaani, Nikamcheki jamaangu Kidosho yeye alikuwa anakaa msewe, Nikamweleza na mimi nataka nipange mtaani , Akasema si bora uje tukae wote hapa tushirikiane kulipa kodi, Mi nikaona ni wazo zuri, tena ukizingatia wote tunasoma kozi moja itakuwa rahisi kufanya discusion,

Basi bumu lilivyotoka tukanunua kitanda kikubwa, jiko la gasi plate 2, meza nzuri ya kusomea, sabufa, basi geto likapendeza, shule ilienda vizuri sana, Getoni wakawa wanakuja wenzetu tunapiga discusion la maana pale,

Kifupi shule haikuwa ngumu sana kulinganisha na mwaka wa pili, Basi semista ikakata, mi sikwenda kijijini nikabaki pale geto tu maana wiki mbili si nyingi, Nyumbani Happy akajifungua mtoto wa kike, wakanitumia picha katoto keupe kama mama yake basi nikakapa jina Joyce kama bibi yake,

Tukafungua shule, semista ikaanza tukaikimbiza nayo ikakata, tukaenda field tena, Mimi kama kawa field yangu ni hapa hapa Dar, Basi tukamaliza field, tukaanza tena mwaka wa nne, tukawa tunaenda chuo kama kipindi ni asubuhi na kingine mchana basi tunakaa kwenye vimbweta tunajisomea paka kile cha mchana kifike tukitoka ndo twende nyumbani, kuliko nenda rudi,

Siku moja nimetulia zangu kwenye vimbweta vya NMB pale Coet nakula msuli taratibu, mara naona kimbweta cha mbele kakaa mdada mmoja bonge hivi alafu kavaa kimini, mbaya zaidi kageukia huku mimi nilipo, Basi kama kawaida yangu mzee chabo nikaanza kufanya yangu huku nazuga nasoma, Kumbe yule sista kanishtukia nna mla chabo, basi akawa anatanua mapaja alafu ana bana, anatanua anabana, ndani kavaa taiti nyeupe, kumcheki usoni naona ananiangalia alafu anatabasamu,

Basi mi nikajifanya nipo serious napiga msuli simwangalii, Sjakaa vizuri mara naskia "ulikuwa unachungulia nini?" Kucheki dada huyu hapa , kaja kwenye kile kimbweta changu, akaniambia soogea tukae wote, basi nikajisogeza akakaa, akaniuliza unasoma nini hapo? nikamwambia hii inaitwa engineering thermodynamics, Akasema we unasoma engineering nikamwambia ndio , akasema hongera, nikamuuliza kwanini? akasema naskia hiyo engineering ni balaa, upo mwaka wa ngap? nikamwambia wa nne, basi tukapiga stori pale, akasema yeye anaitwa Sity, yeye hasomi pale, bali pale kaja kujisomea tu, yeye anasoma chuo cha magogoni anasomea certificate of record management,

Mtoto ni mzuri huyo, choclate flani hivi, ana vidimpo vya kuibia, kajaa kidogo alafu huko nyuma sasa ni masha allah si kitoto, tukapiga stori pale ikafika mchana nikampeleka cafteria ya block A pale tukapiga menyu,

Basi mi nikamuaga maana muda wa pindi ulikuwa umefika, alafu pindi lenyewe yombo hukoo, Basi tukapeana namba pale mi nikasepa,

Basi usiku nikiwa na kidosho tunapiga stori mara mtoto akaniendea hewani, akaniuliza kama kesho naenda chuo nikamwambia sina kipindi ntakuwa geto tu, basi akasema atakuja geto tusome, nikamwambia poa,

Moyoni nikasema huyu mtoto ananitaka nini!!!, Haya bana,kesho yake mida mida hivi kweli mtoto akatimba, kanipigia suruali hiyo imebana, nikasema khaah huu mzigo nitauweza kweli? Basi kidosho akajikataa zake akaniacha geto na mtoto,

Tukaanza kusoma, yeye kaja na kadaftari chake kameandikwa mambo ya register, sijui what is register, sijui importance of register, bana atajua mwenyewe, Mi najifanya nasoma ila msuli haupandi, yaani nikimcheki mtoto nahis kuchanganyikiwa, ukichanganya na perfum yake ndo ananimaliza akili kabisa,

Basi nikajikaza kidume ila uzalendo ukanishinda baaria, nikamwomba gemu mtoto, akagoma kata kata, akasema hawez kufanya mapenzi na mtu hata hamjui vizuri, akipata virusi je? Akasema kama nataka twende kwanza tukapime, basi mzee mzima nikawa sina jinsi nikawa mpole tukaendelea kusoma,

Basi tukapanga siku twende pale zahanati ya chuo tukapime, nikasema poa maana ile zahanati ya chuo naiamini, chochote utachopima pale utaambiwa hauna, kuna siku nilienda pale nnaumwa balaa, yaan nashikiliwa nisianguke, ajabu nikapimwa maleria nikaambiwa sina, kwenda kairuki kupima nakutwa na maleria za kufa mtu, basi nikasema pale ukienda kupima hata uzito si ajabu ukaambiwa hauna

Basi siku ikafika mi na Sity hao tukatimba pale zahanati, nikiwa na imani kabisa haitaniangusha, basi tukamwambia yule nesi kuwa sisi ni wapenzi kwaiyo tumekuja kujua afya zetu, Akatupa nasaha zake pale mwisho akatutoa damu akaweka kwenye kidude chake kile akatuambia tukasubiri nje atatuita, basi tukatoka,

Tukiwa tumekaa nje kwenye benchi tunapiga stori mara tukaitwa kule ndani, Basi nesi akatuambia majibu yenu tayari, ila kwa kuwa ninyi ni wapenzi na mna aminiana basi kila mmoja atasoma majibu ya mwenzake, tukasema sawa, basi mi nikapewa ya Sity na Sity akapewa yangu, Basi sity alipofungua majibu asome mara ghafla akashtuka kwa nguvu,

Itaendelea
 
Katika hali ya kawaida unawezaje kukumbuka vitu vya miaka zaidi ya 5 au zaidi iliyopita kwa 'detail' hivyo? Naona kama ni ngumu sana....

Vyovyote vile hadithi ni nzuri iwe ya utunzi au ya kweli. Nahisi wewe ni mtunzi maana unaishia sehem zenye 'suspense' ili msomaji ifuatilie kiliendelea nini kwneye muendelezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…